Bukobawadau

SBL inalaani kusambazwa kwa video isiyo na maadili kwenye mitandao ya kijamii

TAARIFA KWA UMMA Dar es Salaam Januari 12, 2017- Kampuni ya Bia ya Serengeti inapenda kuwataarifu wateja wake na umma na kwa ujumla kuwa kuna video isiyo na maadili inaiyosambazwa katika mtandao ya kijamii ikionesha msanii akiigiza na kuimba wimbo wenye mahadhi ya taarabu mbele ya bango lenye nembo ya bia Serengeti Premiur Lager. Tunapenda kuweka bayana kuwa onesho la msanii huyo halikuidhinishwa wala kudhaminiwa na SBL Pia msanii huyo sio sehemu na hajawahi kuwa mmoja wa mawakala wetu wanaotoa huduma za kutangaza bidhaa zetu. Video hiyo ambayo haizingatii maadili ya sanaa inatoa picha mbaya jambo ambalo ni kinyume na sera ya SBL ya kuzingatia maadili mema katika shughuli za kutangaza bidhaa zake. Aidha ikumbukwe kwamba SBL imekuwa mstari wa mbele katika kulinda na kusimamia maadili katika shughuli zake za kijamii ikiwa ni pamoja na kuhamasisha unywaji wa pombe kistaarabu. Tunauhakikishia umma na wateja wetu kuwa SBL inafanya shughuli zake za kijamii kwa kuangalia mambo yenye tija kwa jamii na sio vinginevyo. Tunapenda kuwashukuru sana wateja wetu na umma kwa ujumla kwa kuendelea kushirikiana nasi. Imetolewa na Mkurungezi wa Mahusiano Serengeti Breweries Limited.

Next Post Previous Post
Bukobawadau