Bukobawadau

KUCHANGIA UJENZI WA MSIKITI WA JAMIA BUKOBA ULIOATHIRIWA NA TETEMEKO LA ARTHI

Uongozi wa Msikiti wa Jamia Bukoba unatumia fursa hii kukuomba wewe Msomaji na Muumini kuchangia Mradi wa Msikiti Jamia,ambao ni Msikiti Mkuu wa Manispaa ya Bukoba  uliobomolewa baada ya kuathiriwa Vibaya na tetemeko la Ardhi lililotokea Mkoani Kagera Septemba 10,2016.
 Hivyo basi kama muumini uliyeguswa na suala hili unaombwa kuchangia katika manunuzi ya Vifaa vya Ujenzi au kuchangia Ujenzi wa Msikiti huo kupitia akaunti ya UJENZI WA MASJIDI JAMIA BUKOBA,NAMBA YA AKAUNTI ;0152249397200 CRDB BUKOBA
 Sheikh Haruna Kichwabuta ,Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Kagera akionyesha athari zilizojitokeza katika Msikiti huo kutoka na tetemeko na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera Sep 10,2016
 Kipande cha nguzo kilichobomoka kutoka sehemu ya Juu ya Msikiti huo.
 Ofisi za Bakwata Mkoa Kagera zilizopo Jirani na Msikiti wa Jamia Bukoba zikiwa zimeathiriwa na tetemeko hilo ambapo mpaka sasa Mchango wa Ujenzi wa miundo mbinu ya Msikiti huo inahitajika.
 Baadhi ya waumini wa kiislamu walikiendelea kujitolea kusaidia shughuli ya kukusanya baadhi ya Vifaa katika Msikiti Mkuu wa Ijumaa Manispaa BUKOBA Msikiti wa Jamia ,Mdau Msomaji unaombwa kuchangia Ujenzi wa Msikiti huo kupitia akaunti ya UJENZI WA MASJIDI JAMIA BUKOBA,NAMBA YA AKAUNTI ;0152249397200 CRDB BUKOBA
 Waumini wakiendelea kusaidia shughuli mbalimbali zinazoendelea katika hatua za awali za kurejesha Jengo la Msikiti wa Jamia Bukoba.
Kama umeguswa tafadhali unaombwa kuchangia Ujenzi waMsikiti huo kupitia akaunti ya UJENZI WA MASJIDI JAMIA BUKOBA,NAMBA YA AKAUNTI ;0152249397200 CRDB BUKOBA
Sehemu mbalimbali za Msikiti huo zilivyoathirika vibaya
Muonekano wa ndani baada ya kutokea kwa tetemeko la ardhi
UONGOZI WA MSIKITI WA JAMIA UNATOA SHUKRANI KWA WOTE MLIO CHANGIA NA MTAKAO ENDELEA KUCHANGIA KWA HALI NA MALI , kwa Pamoja TUIJENGE NYUMBA YA IBADA MALIPO YAKE AKHERA NI MAKUBWA ZAIDI NA DUNIANI PIA UNAPATA.
Waumini wakifatilia zoezi la Ubomoaji wa Jengo la Msikiti huo uliopo katika ya Mji wa Bukoba
BUKOBAWADAU MEDIA kama balozi wa kulitangaza jambo hili tunatoa shukrani kwa Watanzania wote na Waumini na wasio kuwa hao kwa Upamoja wao kwa Michango yao ya hali na Mali inayoendelea katika Kuimarisha Mradi wa UJENZI WA MSIKITI WA JAMIA Ulioathiriwa vibaya na tetemeko la ardhi kama inavyo onekana pichani.
Daima Jamii ya watu huwa Nzuri zaidi na ikishikamana na IBADA na KUMTAMBUA MUUMBA kama Ni hivyo basi kwa PAMOJA TUUJENGE MSIKITI HUU tupate kuwa na Jamii Njema.
 Wabillahi Taufiqh!!


.
Next Post Previous Post
Bukobawadau