Bukobawadau

YALIYOJIRI MULEBA MADC WATAKIWA KUJIAMINI KUELEZA MAENEO YENYE NJAA

Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema na waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa akizungumza  na mamia ya Wananchi na Wanachama wa Chadema waliojitokeza kwenye Mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kimwani,Uliofanyika Jana Jumamosi Jan 14,2017.
  Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa na Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema akizungumza wakati wa akimnadi Mgombea wa Udiwani wa Kata ya Kimwani kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Leonard Ntimanyi pichani kulia kwenye Mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kimwani Jimbo la Muleba kusini uliofanyika Jana Jan 14,2017.
Wananchi wa Kata ya Kimwani  wakimsikiliza Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema na Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa katika Mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani Kata ya Kimwani uliofanyika Siku ya Jana Jumamosi  Jan 14,2017.
Akiongea na Wananchi waliohudhuria Mkutano Mjumbe wa Kamati Kuu ( Chadema ) Edward Lowassa amewashauri Watanzania wasipingane na misimamo ya Rais Magufuli kuwa nchi haijakumbwa na janga la njaa ispokuwa watangulize maombi kwa Mungu ajalie  mvua inyeshe  kunusuru mazao yanayonyauka mashambani. 
Lowasa alisema Wananchi wasitishike kumchagua kiongozi atakayewatetea kupata haki na huduma za kijamii na kwamba viongozi wa chama hicho kutoka majimbo ya Muleba Kusini na Kaskazini, wahusike kuwasikiliza wananchi ambao wanapuuzwa kwa kauli na vitendo kutoka kwa Rais Magufuli katika kubeza changamoto zinazowakabili watanzania.
Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee CHADEMA Roderick Lutembeka Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema akiongea na Wananchi waliohudhuria Mkutano huo

Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee CHADEMA Roderick Lutembeka na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa Chadema akiwaonyesha Wananchi wa Kata ya Kimwani mfano wa karatasi ya kupigia Kura kwa wagomebea Udiwani  katika Mkutano huo uliofanyika Jana Jumamosi Jan 14,2017

MADC WATAKIWA KUJIAMINI KUELEZA MAENEO YENYE NJAA
Anaandika Shaaban Nassibu, Ndyamukama

Wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa Halmashauri za wilaya kote nchini wametakiwa kuwaongoza wananchi bila kuhofia kutumbuliwa na Rais John Magufuli wakitanguliza uzalendo wa kuwatetea wanaokabiliwa na janga la njaa kwenye halmashauri za wilaya zao
Kada wa zamani wa Chama cha Mapinduzi mkoani Shinyanga Hamisi Mgeja ambaye sasa ni mjumbe wa kamati ya ufundi ya Chadema ,ametoa wito huo wiki hii kwenye mkutano wa kampeni za udiwani uliofanyika kata ya Kimwani Wilayani Muleba na kwamba viongozi hao wateule wa Rais wanahitaji kutumia nafasi zao kuwasemea watanzania 
Mgeja amesema viongizi wengi wanafanya kazi bila kujiamini kwa kuwa Rais anadai ndiye msemaji wa mwisho kuhusu tatizo la njaa lakini maeneo mengi yaliyo na wawakilishi wake yanakabiliwa na ukame hivyo wateule wake wanatakiwa kutaarifu hali halisi juu ya suala hilo

“Watanzania tunahitaji mabadiliko na utawala bora kuepuka ukandamizaji wa kidemokrasia na kubainisha changamoto ili kutafutiwa ufumbuzi kwa kuwa nchi hii imejaa vitendo vya Rushwa na ubadhilifu wa rasilimali pia kupewa huduma sio uhisani”. Alisema Mgeja 
 MEYA wa Manispaa ya Bukoba, Chief Kalumuna akiwa Jukwaani Kimwani.
Aidha meya wa manispaa ya Bukoba kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Chief Kalumuna alisema serikali ya awamu ya tano haina budi kuwatetea wanyonge kwa vitendo badala ya kuwakebei majukwaani katika kuwapatia huduma bora za kijamii

Alisema mkoa wa kagera umekuwa na tetemeko la ardhi mwaka jana lakini serikali bado haijaonesha machungu kwa wakazi wa mkoa huo kwa vitendo angalau kuwapunguzia gharama za vifaa vya ujenzi badala yake misada inayochangwa imekumbatiwa bila kuwafikia walengwa
Katika tetemeko hilo watu 17 walifariki dunia na wengine kadhaa kujeruhiwa wakati nyumba nyingi zilianguka na nyinge kupatwa na nyufa ambapo serikali misada ya wahisani ilielekezwa kukarabati miundombinu katika taasisi zake kama barabara na shule

“Mimi nimekaa jeshi la polisi masaa mane nikitakiwa kujieleza nilikuwa na lengo gani la kuhoji misaada inayoletwa na wahisani kusaidia wahanga wa tetemeko katika manispaa ya Bukoba lakini sitateteleka nawatetea wananchi wangu” Alisema Chifu Kalumuna
 Meya huyo akiungana na Mbunge wa jimbo la Bukoba Wilfred Rwakatale walihimiza serikali kuwa sikivu kwa kilio cha watanzania waishio mkoani kagera kupunguziwa vifaa vya viwandani waweze kujeng na kukarabati nyumba zao kwa kuwa baadhi yao bado wanaendelea kulala nje
Kwenye mkutano huo wa kampeni za mgombea udiwani leonard Nchimani kupitia Chadema viongozi waliosimama jukwaani walihimiza amani na utulifu na kuwataka kujihadhari na vitendo vya rushwa na kupoteza haki zao za msingi kumchagua kiongozi atakaye watetea kwa usahihi katika vikao vya maamuzi kulingana na changamoto zinazowakabili

Mgombea udiwani kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Leonard Nchimani amesema iwapo atachaguliwa atashirikiana na wananchi kutatua changamoto zinazowakabili wakazi wa kata hiyo hasa barabara maji na zahanati pamoja na uboreshaji vyumba vya madarasa
Hata hivyo Mjumbe wa Kamati Kuu ( Chadema ) Edward Lowassa amewashauri Watanzania wasipingane na misimamo ya Rais Magufuli kuwa nchi haijakumbwa na janga la njaa ispokuwa watangulize maombi kwa Mungu ajalie kunyesha mvua kunusuru mazao yanayonyauka mashambani

Lowasa alisema wananchi wasitishike kumchagua kiongozi atakayewatetea kupata haki na huduma za kijamii na kwamba viongozi wa chama hicho kutoka majimbo ya Muleba Kusini na Kaskazini, wahusike kuwasikiliza wananchi ambao wanapuuzwa kwa kauli na vitendo kutoka kwa Rais Magufuli katika kubeza changamoto zinazowakabili watanzania.
 Taswira mbalimbali kutoka Kijijini Kimwani Muleba, Kampeni cha Uchaguzi Mdogo Udiwani
“Wananchi wasipuuzwe kuna tatizo la njaa kwenye maeneo ya nchi na baadaye vifo vinaweza hata kutokea lakini tupingane kwa hoja bila kuumizana na kutakiana mabaya, tuwasaidie wananchi wanaopata matatizo bila kuwapuuza” Alisema Lowassa Katibu Mkuu wa Baraza la Wazee CHADEMA Roderick Lutembeka
Awali Lowasa akiwa wilayani Muleba asubuhi alifanya kikao cha ndani na viongozi wa Chadema wa jimbo la Muleba kusini na kaskazini ,kwa kuwahimiza kushikamana kuwatetea watanzania dhidi ya vitendo vya ukandamizwaji wa Demokrasia na utawala bora, pamoja na kuwapatia huduma bora za kijamii ambazo ndio mahitaji ya walio wengi.
 Mbunge wa Bukoba Mjini kupitia CHADEMA, Wilfred Lwakatare akihutubia katika Mkutano wa Kampeni wa Uchaguzi Mdogo wa Diwani Kata ya Kimwani uliofanyika jana Jan 14,2017
 Mh. Lwakatare mara baada ya kuwatunza Vijana waliokuwa wakitoa burudani katika mkutano huo
 Waziri mkuu mstaafu Edward Lowassa na Mjumbe wa kamati kuu ya Chadema mara baada ya Mkutano huo.
Mgombea udiwani kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Leonard Nchimani akiagana na Mh.Lowassa mara baada ya mkutano huo uliofanyika Jana Jumanosi.
 Wananchi wa Kata ya Kimwani wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa Udiwani wa Chadema.

Next Post Previous Post
Bukobawadau