Bukobawadau

WAWILI WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KWA TUHUMA ZAMAUAJI MKOANI KAGERA

Na Mwandishi wetu..
BukobaWadau

JESHI la polisi mkoani Kagera linawashikilia watuhumiwa wawili ambao ni Msafiri Samson(41) na Marciana Kaila kwa makosa ya mauaji uliosababishwa na ugomvi na kusababisha kifo cha mtoto Elizabeth Msafiri mwenye umri wa miezi 14 na mke wa Matokeo Kaila .
Hayo yamesemwa na kamanda wa Polisi mkoani Kagera Agastine Ollomi, alisema kuwa matukio hayo yalitokea Wilayani Biharamulo maeneo mbalimbali ambayo yalisababishwa na ugomvi wa kifamilia.
Kamanda Ollomi alisema mtuhumiwa Msafiri Samsoni aliyesababisha kifo cha mwanae, Elizabeth Msafiri alimpiga na fimbo begani mkewe Pudensiana Daniel(29) mkulima wakati amebeba mtoto huyo mgongoni.
Aidha Kamanda alisema awali mtuhumiwa huyo alimpiga mkewe fimbo ya kwanza begani na ya pili ilimfikia mtoto ambae alikuwa amebebwa na mama yake mgogoni na kumfikia sehemu za kichwa na kusababisha kifo papo hapo .
Katika tukio la pili Kamanda alisema kuwa mtuhumiwa anae shikiliwa kwa niaba ya ndugu yake Matokeo Kaila aliyekimbilia kusikojulina alimvamia mkewe ambae walikuwa wameachana kipindi kirefu, na kumvamia kwa kuvunja mlango na kuingia ndani.
Aliongeza kuwa baada ya kuingia ndani ya nyumba ya Bi Sikujua Maungomu (36) usiku wa saa 9 wakati amelala na wanae Alphonce Matokeo na mwingine  Abdallah Matokeo Miwili mtuhumiwa alianza kumkatakata kwa panga sehemu mbalimbali za mwili wake ambapo zilitoka damu nyingi na kusababisha kifo chake.
pia alisema chanzo cha matukio hayo hakijajulikana upelelezi wa Polisi bado Unaendelea ili kubaini chanzo, na kuwafikisha mahakamni kwa makosa yanayowakabili.
"Katika hali hii hakuna mtu yeyote anaeruhusiwa kuchukua sheria mkononi hivyo hatima ya mtu anaefanya hivyo anatakiwa kuchuliwa hatua kali za kisheria"alisema Kamnda huyo
Mwisho.
Next Post Previous Post
Bukobawadau