Bukobawadau

ASIMIKWA KUWA ASKOFU DAYOSISI YA LWERU KAGERA

Askofu mteule wa Dayosis ya Rwelu mkoani Kagera Godfrey Mbelwa (katikati) akiapa kutumikia dayosisi hiyo kulia  ni AskofuLugendo Julius wa Dayosis ya Mbeya na kushoto ni Askofu George Okoth kutoka Dayosisi ya Mara 
 Askofu mteule wa Dayosis ya Rwelu mkoani Kagera Godfrey Mbelwa akisaini kiapo
Picha Zote na Shaaban Ndyamukama
Maaskofu mbalimbali wa kanisa la Anglikana Tanzania wakimuwekea mikono Askofu mteule wa Dayosisi ya Rwelu mkoani Kagera Godfrey Mbelwa ambaye alikuwa katibu wa dayosis ya Kagera  katika ibada ya kumsimika iliyofanyika jana (leo) katika viwanja vya kanisa kuu la Anglikana muleba mjini  
Askofu wa kanisa kuu la Anglikana Tanzania Dr Jacob Chimeledya amewataka maaskofu wenzake wa kanisa hilo nchini kutumia nafasi zao za kichungaji kulinda maadili ya jamii kisha kuwapenda waumini kwa kutanguliza mapenzi ya Yesu Kristu katika kulitangaza neno la Mungu.
Askofu Dr Chimeledya alitoa kauli hiyo Februari 5 katika ibada takatifu ya kumsimika Mchungaji Kanoni Godfrey Mbelwa kuwa askofu mteule wa pili wa Dayosisi ya Rwelu Mkoani Kagera baada ya aliyekuwa akilongoza dayosisi hiyo kufikisha umri wa miaka 60 na kustaafu kwa mujibu wa kanuni za kanisa la Anglikana
Alisema kuwa Askofu mteule Godfrey Mbelwa anatakiwa kujitoa kuwasaidia wachungaji na waumini katika kuwaondolea changamoto zinazowakabili katika masuala ya kiroho kijamii na kwamba awahimize kufanya kazi kuongeza mapato ya familia badala ya kulalamikia ugumu wa maisha 
Alisema kazi ya uchungaji wa kondoo wa Mungu unahitaji kujitoa kwa kutumika kama alivyofanya Petro aliyekuwa hana chochote mbele ya mungu lakini alimsifia Mungu akiambatana na Yohana mtakatifu wakimtanguliza Yesu kristo
“Watu wamekosa mapenzi ya Mungu na kuanza kuteseka wakisumbuliwa na mapepo na kupoteza imani zao hatimaye kusababisha mifarakano baina ya jirani hatimaye kukisekana kwa amani Duniani” Alisema Dr Chimeledya
Aidha alisema askofu mteule kwa kushirikiana na wachungaji  na hata maaskofu wengine wachunge watu wa Mungu kwa kuwapa ujumbe wa kina katika kanisa la Mungu ambalo wamepewa na Mungu kwa heshima kubwa 
“Askofu Mbelwa, chungeni kundi la Mungu ikiwa ni pamoja na nyie mapadre, katika kanisa katoliki na mashekhe kwa waislamu maana watu mliokabidhiwa wanahitaji kumtumainia Mungu katikaMaisha yao”Aliongeza
Awali Askofu mstaafu wa Dayosisi ya Rwelu  Jackton Lugumira alisema dayosisi hiyo ilianza Agost mwaka 2006  ambapo ilikuwa na waumini 900 kwa makanisa 36 na sasa imefikia waumini 15,400 walioko katika makanisa 155.
Alisema katika mafaniko yake ni pamoja na kuanzisha shule ya sekondari ya Katoke Rwelu inayofadhiliwa na marafiki wa Dayosis kutoka nchini Australia na kwamba askofu anayemrithi atangulize ngao kuu ya kufanya ushirikishaji waumini na viongozui wengine kulitumikia kanisa
“Changamoto  katika jamii ni nyingi kinachotakiwa ni kusimamia maadili, kuleta mafunuo,  kwa kutatua migogoro na kuhamasisha ukuzaji uchumi wa kifamilia ili waliokosa matumaini  warudi ndani ya zizi la Mungu” Alisema Askofu Luhumira
Alimshauri Askofu mteule kutumia hekima na busara kuwasikiliza wauimini wake na kukubali kuwa mtumwa wao katika daraja la alilopewa la kuwa Askofu, akihusisha malengo ya serikali katika kudumisha utawala bora demokrasi kulinda amani na mshikamano wa kitaifa
Akila kiapo mbele ya Askofu mkuu wa Anglikana Tanzania mteule huyo alisema kwamba ataangalia misingi sheria na masharti ya dayosisi hiyo kama itakavyoundwa marakwama mara na sinodi ys Dayosisi hiyo
“Nitaitisha vikao vya Sinodi ya Dayosisi kwa nyakati kadri itakavyotakiwa na nitajiuzulu wakati wowote kama ikiazimiwa na Askofu mkuu wakanisa la Anglikana Tanzania kwa mujibu wa katiba, Mungu nisaidie.
Sherehe za kumsimika Askofu Godfrey Mbelwa zimehudhuriwa na maaskofu wa Anglikana kutoka mikoa mbalimbali nchini wachungaji na waamini na kwaya mbalimbali zikitumbuiza  huku Marafiki wa Dayosisi ya Rwelu kutoka Australia wakiahidi kusaidia Dayosis hiyo katika miradi ya kielimu na kiroho.

Credir:Shaaban Ndyamukama
MULEBA
 Pata habari mpya Za uhakika na kilahisi zaidi kwa kudownload Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka play store BOFYA HAPA >>BUKOBAWADAU APP FOR ANDROID
Next Post Previous Post
Bukobawadau