Bukobawadau

VIDEO/PICHA WABUNGE WA UPINZANI WALIPOTOKA BUNGENI DODOMA FEB 7,2017

 Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT) Zitto Kabwe akizungumza na Wanahabari baada ya Wabunge wa Kambi ya Upinzani kutoka nje ya Bunge baada ya Naibu Spika wa Bunge kuamuru Mbunge wa jimbo la Serengeti Mkoa wa Mara, Marwa Ryoba (Chadema) kuamuriwa kutoka nje kufuatia kelele alizokuwa akipiga baada ya Naibu Spika kukataa Bunge kujadili mwongozo wa Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe aliyetaka ufafanuzi kuahusiana na kukamatwa kwa Wabunge wakiwa katika majukumu yao ya kazi za kibunge pasipo Ofisi ya Spika kujua.
 Wabunge wa Kambi ya Upinzani wakiinuka kutoka nje
Wabunge wa Kambi ya Upinzani wakiinuka kutoka nje 
 Wabunge wa Upinzani wakiwa nje ya Ukumbi wa Bunge
 Eneo wanaloketi Wabunge wa Upinzani likiwa wazi ispokuwa kiti kimoja ambacho Mbunge wake hakutoka.  
Kutokea bungeni Dodoma leo February 7 2017 Wabunge wa kambi rasmi ya upinzani bungeni walitoka nje ya jengo la bunge wakati mkutano ukiendelea kwa madai kwamba Naibu spika Dr. Tulia Ackson amekataa mwongozo wa kujadili tukio la kukamatwa kwa Mbunge wa Singida 
 DOWNLOAD Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka play store BOFYA HAPA KUDOWNLOAD APP YA BUKOBAWADAU FOR ANDROID Kwa habari mpya za uhakika kilahisi zaidi
Next Post Previous Post
Bukobawadau