Bukobawadau

Baadhi ya viongozi wa Msumbiji waliolelewa na kukulia Tanzania: 

 
 Baadhi ya viongozi wa Msumbiji waliolelewa na kukulia Tanzania:
1. #EdwardoMondlane Kiongozi wa kwanza na muasisi wa chama cha FRELIMO. Alikiunda chama cha FRELIMO mwaka 1962 nchini Tanzania na makao makuu ya FRELIMO yakawa jijini Dar es Salaam kwa miaka 13, tangu mwaka 1962 hadi mwaka 1975. Ilikua ukitaka kuwapata viongozi wa Kitaifa wa FRELIMO walikua wanapatikana Dar. Mwalimu Nyerere aliwapa ofisi na kuwalipa mishahara. Marehemu Mondlane na viongozi wenzie wa FRELIMO walikua wakilipwa mishahara na serikali ya Tanzania. Hebu imagine ni upendo wa aina gani huu? Yani mje kwetu tuwape makambi ya kujificha, tuwape mafunzo ya kijeshi, tuwape ofisi za makao makuu ya chama chenu, tuwape nyumba za kuishi viongozi wenu afu bado tuwape na mishahara? Nyerere was blessed. He did all that with expectation of no return. Hakuwa na interest yoyote na Msumbiji zaidi ya kuwasaidia waafrika wenzetu.  
2. #SamoraMachel Alizaliwa kijiji cha Chilembene, mkoa wa Gaza huko Msumbiji. Baada ya kuhitimu elimu ya sekondari na mafunzo ya uuguzi alikimbilia Tanzania kuanza mapambano ya kudai uhuru. Alianzia Dar es salaam katika makao makuu ya FRELIMO ambapo alikutana na viongozi wenzake wa Msumbiji waliokua wakidai Uhuru. Baadae alihamia kwenye makambi ya wapigania uhuru wa Msumbiji yaliyokua maeneo mbalimbali mwa Tanzania ikiwemo Tunduru, Dodoma na Iringa. Alishiriki vita vya kuikomboa Msumbiji akitokea kambi ya Liwale na nyingine iliyokua Tunduru, kwa msaada mkubwa wa JWTZ.  
3. #DrJoachimChisano Rais wa pili wa Msumbiji tokea mwaka 1986 hadi mwaka 2005. Ameishi Tanzania, amefanya kazi Tanzania katika mashamba ya mkonge Tanga akiwa kama daktari wa binadamu (MD). Baada ya kuhitimu shahada yake ya udaktari huko Ureno aliamua kushiriki harakati za kisiasa za kuikomboa Msumbiji akitokea Tanzania. Anazungumza Kiswahili kwa ufasaha kwa sababu ameishi muda mrefu Tanzania. Mwaka 2004 akiwa Mwenyekiti wa AU alihutubia mkutano mkuu wa AU kwa Kiswahili. 
4. #ArmandoGuebuza Alizaliwa huko Nampula nchini Msumbiji na akiwa na umri wa miaka 20 tu alikimbilia nchini Tanzania ili kushiriki katika harakati za kupigania uhuru wa taifa lake. Alijiunga na kambi ya Tunduru na baadae Liwale na Kongwa mkoani Dodoma. Baada ya uhuru mwaka 1975, Rais Samora Machel alimteua Armando kuwa Waziri wa mambo ya ndani. Anazungumza Kiswahili kwa Ufasaha japo hapendi kukitumia sana hadharani.
5. #FilipeNyussi Rais wa 4 wa Msumbiji. Alizaliwa mwaka 1959 huko Mueda, mkoa wa Cabo Delgado nchini Msumbiji. Vita vya kudai Uhuru vilipoanza (Mozambique war of Independence), Filipe alikua na umri mdogo sana (miaka 8 tu) na hivyo wazazi wake kukimbia nae kuja kutafuta hifadhi nchini Tanzania.  Alisoma shule ya msingi Frelimo iliyopo wilayani Tunduru.
 Alipomaliza elimu ya msingi mwaka 1975 tayari Msumbiji ilikua imeshapata uhuru na hivyo kurudi kwao kuendelea na elimu ya sekondari, lakini mwaka 1976 alirudi Tanzania na kujiunga na elumu ya Sekondari shule ya wamisionari Ndanda ambayo kwa sasa ni shule ya serikali. Kabla ya hapo mwaka 1973 akiwa na umri wa miaka 14 tu alijiunga na kikosi cha Frelimo na kupewa mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Nachingwea. Anazungumza Kiswahili kwa ufasaha kutokana na kusoma na kulelewa Tanzania. Kwa kifupi ni kwamba huwezi kutaja historia ya Msumbiji bila kuitaja Tanzania. Bila kumtaja Nyerere. Marais wote wa Msumbiji wamelelewa, kusoma, kufanya kazi au kupata mafunzo ya kijeshi wakiwa Tanzania. Hakuna Rais yeyote wa Msumbiji ambaye hajaishi Tanzania.  Kila Rais wa Msumbiji ana uwezo wa kuandika kitabu zaidi ya kimoja kuhusu Tanzania. Lakini leo watanzania waishio Msumbiji wanapigwa, wanateswa, wananyang'anywa mali zao walizozipata kwa jasho, kisha wanapakizwa kwenye malori na kwenda kutupwa mpakani. Inauma sana. History is our best teacher!  
Malisa GJ

 Pata habari mpya za uhakika kilahisi zaidi kwa kudownload Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka play store BOFYA HAPA BUKOBAWADAU APP
Next Post Previous Post
Bukobawadau