Mkuu wa wilaya ya Ngara mkoani Kagera Luteni Kanali Michael Mtenjele
aking'oa bangi leo katika shamba la mwananchi mkazi wa kijiji cha
Kazingati kata ya Keza wilayani humo ambaye alitegemea kuvuna magunia 80
na kilo moja angeuza Sh 1700 kwa wateja kutoka nchini Burundi
NGARA:
Jeshi la polisi katika wilaya ya Ngara mkoani Kagera, linamshikilia
mkazi wa kijiji cha Kazingati kata ya keza wilayani humo baada ya
kumkuta anamiliki shamba la ekari mbili za bangi ambayo ni aina mojawapo
ya dawa za kulevya
Mkuu
wa wilaya ya Ngara Luteni Kanali Michael Mntenjele ambaye ni Mwenyekiti
wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya amesema mkazi huyo ni Fabian
Kasigo (45) ambaye alikamatwa jana katika kijiji hicho
Kanali
Mntenjele alisema mkulima huyo alipohojiwa alikiri kulima kilimo hicho
tangu mwaka 2001 na kwamba mwaka huu angevuna magunia 80 ya bangi
akitarajia kuuza kila kilo moja kwa Sh17,000 kwa wateja wake wa nchini
Burundi
Alisema
kilimo cha bangi wilayani Ngara kimeshamiri kata zilizopo mpakani na
nchi jirani za Rwanda na Burundi has kata ya Ntobeye Nyakisasa Keza na
Muganza ambapo jeshi la polisi limekuwa likiwakamata na kuwafikisha
mahakamani.
“Tunajitahidi
kuwasiliana na wananchi wenye uzalendo raia wema kutupatia taarifa za
walimaji wa zao hili, kuweza kuwakamata kwani kilimo cha bangi
hakitakiwi kwa mujibu wa sheria za nchi yetu” Alisema Kanali Mntenjele.
Akitoa
maelezo kwa kamati ya ulinzi na usalama kwenye shamba hilo Fabian
Kasigo alisema amekuwa akiuza bangi kutoka kwa wateja mbalimbali na
kuitumia kama kinga ya magonjwa kwa kutumia majani yake na kuinywa
kwenye maji
Alisema
kwa umri wake hawawahi kuugua na akitumia bangi huwa mwili unaimarika
na kwamba tangu mwaka 2001 ametumia faida ya bangi kujiinua kiuchumi kwa
kununua zaidi mashamba na mifugo
Kamati
ya ulinzi na usalama katika kulifikia shamba hilo ilitumia muda wa
masaa mawili kwani aliingia katikati ya pori ambako kunakaa wafugaji
jamii ya wasukuma na wanyarwanda na kupata mbolea ya samadi na
kustawisha zao hilo
Askari
polisi walilazimika kung'oa miche ya shamba la bangi ambapo ndani ya
nyumba ya mtuhumiwa kulikuwa na kilo mbili za mbegu ya zao hilo ikidaiwa
kulikuwa na maandalizi ya kulima ekari tatu nyingine.
Na Shaaban Ndyamukama
Pata habari mpya Za uhakika kilahisi zaidi kwa kudownload Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka play store BOFYA HAPA KUDOWNLOAD
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment