Bukobawadau

DIWANI KIMWANI AAPISHWA NDANI YA BARAZA LA MADIWANI WILAYANI MULEBA

Diwani wa kata ya Kimwani Wilayani Muleba mkoani kagera Daudi Kiluma kupitia Chama cha mapinduzi ameapishwa leo na kupewa hati ya ushindi wa kuwa diwani wa kata hiyo baada ya kushinda uchaguzi  mdogo uliofanyika januari 22 mwaka huu
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Muleba Chrizant Kamugisha amemtaka diwani huyo kutumia uzalendo kuongoza wananchi wa kata yake bila kujali itikadi za kisiasa katika kuhakikisha anasimamia maendeleo kupunguza changamoto zinazowakabili 
Kamugisha  (mwenye joho jekundu) amesema uchaguzi huo uliofanyika kimwani ulikuwa wa amani na utulivu  na kwamba kasoro zilizojitokeza hazikusababisha uchaguzi huo kukwama  na kwamba wananchi wanahitaji huduma bora za kijamii kutoka kwa diwani Kiluma 
Aidha amesema viongozi wa CCM na halmashauri kwa ujumla watoe ushirikiano katika kumuelekeza jinsi ya kusaidiana na wakuu wa idara kuwasilisha changamoto za watu wake katika sekta ya afya elimu maji na mtandao ya barabara bila kuacha mkakati wa kutunza mazingira 

"Wilaya yetu baadhi ya maeneo yanakabiliwa na upungufu wa chakula hivyo madiwani tuhimize wananchi wetu kutumia mvua zinazoendelea kunyesha walime na kupanda mazao yanayostahimili ukame na kukosa kwa muda mfupi" Alisema Kamugisha 
Diwani Kiluma akiapa mbele ya Hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya ya Muleba Cleophace Waane amesema atailinda katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  sheria za Tanzania maadili ya madiwani na kanuni za kudumu kisha kutumikia wananchi kwa uhuru na usawa 
Amesema atashirikiana na madiwani wenzake na ofisi ya mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Muleba kuwasilisha mahitaji ya wananchi wa kata hiyo akianza na vipaumbele alivyojiwekea kutimiza ahadi zake wakati wa kampeni alipokuwa akinadi Sera za Cha cha Mapinduzi
"Kwa Wadhifa wangu wa udiwani nitahifadhi , nitailinda na kuitetea akiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa utii uaminifu , kwa uwezo na uwezo wangu wote ikiwa ni pamoja na kutekeleza kanuni za kudumu za halmashauri hii ya Muleba " Alisema Kiluma 
Uchaguzi wa udiwani katika kata ya Kimwani Wilayani Muleba ulifanyika baada ya aliyekuwa amechaguliwa mwaka 2015 Silvesta Faustine Muliga kupitia chama cha Wananchi ( CUF) kuuawa mwaka  jana na watu wanaosadikiwa  kutofautiana katika itikadi za kisiasa 
Next Post Previous Post
Bukobawadau