BI ZAHARA A.RAMADHAN AFADHILI NA KUJENGA MSIKITI KIJIJINI KWAO ITOMA-KATORO BUKOBA!
Bi Zahara Abdullah Ramadhan pichani kulia amefadhili kikamilifu ujenzi wa msikiti katika kijiji chao anachozaliwa Katoro -Itoma Bukoba Vijijini,Bi Zahara amejitolewa kuwajengea waumini wa Kiislam msikiti huo ikiwa ni baada ya ule wa awali kuathirika vibaya kufuatia tetemeko la ardhi lililotekea,September 10 2016 Mkoani Kagera.
Baadhi ya Viongozi wa Kidini waliohudhuria Ufunguzi wa Masjid Taawanul uliopo Itoma-katoro Bukoba Vijijini
Muonekano wa Sehemu ya mbele ya Msikiti huo
Muonekano wa sehemu ya pembeni ya Masjid
Masjid Taawanul uliopo Itoma-katoro Bukoba Vijijini
Baadhi ya waumini wakiswali ndani ya Msikiti huo uliozinduliwa juma lililopita Kijijini Itoma Katoro
Kwa niaba ya Waumini na kwa niaba ya Viongozi wa Kiislam ''Bukobawadau media tunatoa shukrani kwako Bi Zahara kwa sadaka yako na tunamwomba Mwenyezi Mungu akuongezee pale ulipotoa, maana Quran inasema ajengaye msikiti anajijengea nyumba peponi"
Mwanzo wa Shughuli ya kisomo cha maulid katika uzinduzi wa Masjid Taawanul uliopo Itoma-katoro Bukoba Vijijini
Pichani kutoka kushoto Bi Zahara Abdullah Ramadhan ,Mama yake mzazi hajat Mastura Abdallah (103) na Hajat Johari ambaye ni Dada mkubwa wa Bi Zahara Abdallah
Waumini wakifatilia kinachoendelea...
Mtoto mdogo mwenye umri wa miaka mitatu anayesoma madarasa ameweza kuwashangaza watu namna alivyohifadhi baadhi ya maneno ya Quruan
Hajjat Hindu akimtunza mtoto huyo mwenye umri wa miaka mitatu (3)
Taswira mbalimbali eneo la tukio
Taswira mbalimbali eneo la tukio hakika watu ni wengi kweli kweli..
Sheikh Farid Maulana akitoa mawaidha katika shughuli ya maulid ya Uzinduzi wa Masjid Taawanul uliopo Itoma-katoro Bukoba Vijijini
Viongozi wa Meza Kuu wakimpongeza Sheikh Farid Maulana mara baada ya kutoa mawahidha.
Burudani ya Kaswida kutoka Kanazi Bukoba Vijijini
Wanafunzi wa Madarasa ya Kanazi wakitumbuiza
Wakati Kamunana Dufu wakitumbuiza.
Wadau wakifuatilia kinachoendelea katika shughuli hiyo.
Muonekano wa Meza Kuu
Ustaadhi ambaye ni mwalimu wa Madarasa akitolea jambo ufafanuzi
Risala ikisomwa kwa mdhamini kutoka kwa Umoja wa Wanawake wa Kiislam wa Kijiji cha Itoma Katoro.
Bi Zahara Abdallah Ramadhan akitoa neno na kuwashukru wote walioshiriki katika shughuli ya Uzinduzi wa Msikiti huo,Bi Zahara Abdallah ametoa wito kwa watu wote wenye mapenzi mema kusaidia mahali popote misikiti inapojengwa ili kuwawezesha waumin kupata mahali pa kuswali jambo ambalo litawapa thawabu kwa Mwenyezi Mungu.
Mwanafunzi wa Madarasa akitoahadithi ya Mtume Muhammad(swalla Allahu alayhi ...alayhi wasallam)
Burudani ya Dufu ikiendelea
Wanafunzi wa Madarasa wakitumbuiza.
Sehemu ya Waumini walioweza kushiriki kikamilifu, shughuli ya uzinduzi wa msikiti huo
Maandalizi yakiendelea upande ya Jikoni
Sehemu ya wanafunzi wa Madarasa wapatao 180 wa eneo hili ya Itoma Katoro wakiwa nje ya Jengo la Msikiti wa zamani Kijijini hapo
Umati wa Waumini kutoka maeneo mbalimbali wameweza kushiriki Shughuli hii ya Uzinduzi wa msikiti huo
Msemo wa katoro muda kama huu, utasikia 'sheikh zinga batano' kwamba mkao ni duara la watu watano watano
Kinachoendelea ni wadau wote waliohudhria shughuli hii kupata Sadaka iliyo andaliwa
Huduma ikiendelea..
Baadhi ya wadau wakipata mulo..
Huduma ya maji ya kunywa ikitolewa kwa watu wote walioweza kujumuika na waumini wengine katika shughuli hiyo iliyofanyika Kijijini Itoma-Katoro
Baadhi ya waumini wakipata Sadaka iliyo andaliwa.
Pichani anaonekana Hajath Mastura Abdallah mwenye miaka 103 kwa maelezo ya wanae, Mama huyu aliyekuwa mwenyekiti wa UWT Katoro zamani,pamoja na kiongozi wa Vikundi mbalimbali vya kusaidiana katika Kata ya Katoro alibahatika kufanya hijja yake mwaka 1986
Endelea kuwa nasi kwa matukio zaidi ya picha...
Ikafika muda wa Waumini kuswali...
Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri katika shughuli hiyo
Wa pili pichani kushoto ni Bwana Abdulrazak Dattan ambaye ni mme wa Bi Zahara.
Hajath akielekea kumtunza mtoto aliyesomo mlango wa tatu wa Quruan..
Huyo mwanafunzi atakaendelea kunufaika na Madarasa mpya iliyojengwa pamoja na msikiti
Raha ya Dufu pale inapomkolea mdau na kushindwa kujizuia
Hivi ndivyo mambo yalivyokuwa katika uzinduzi wa Msikiti huo .
VIA BUKOBAWADAU MEDIA