Bukobawadau

KUNA MWENENDO MZURI KATIKA SOMO LA KISWAHILI-TWAWEZA

Na Hassan Silayo
Mwenendo wa somo la Kiswahili nchini umeendelea kuimarika na hii ni kutokana na jitihada mbalimbali ziliwekwa na serikali katika somo hilo.
Akitoa ripoti matokeo ya utafiti wa Uwezo,Meneja wa Uwezo Tanzania Zaida Mgalla alisema kuwa kwa watoto walikuwa darasa la tatu walioweza kufauli majaribio ya Kiswahili mwaka 2011 walikuwa asilimia 29 tofauti na asilimia 56 ya mwaka 2015.
Bi. Zaida Aliongeza kuwa kwa darasa la saba kumekuwa na ongezeko la watoto kujifunza na kufanya vizuri zaidi ikiwa kwa mwaka 2011 asilimia 76 walifaulu majaribio ya Kiswahili ikilinganishwa na asilimia 89 ya mwaka 2015.
“Tunaipongeza Serikali ka jitihada zake za kuhakikisha watoto wanapiga hatua katika somo la Kiswahili tunaona ongezeko la ufaulu limeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na hii inatia moyo na serikali inatakiwa iendelee kuweka jitihada katika kimarika zaidi na kuacha kuridhika na matokeo haya”.Alisema Zaida.


Aidha Zaida aliongeza kuwa Taarifa ya Tafiti ya Uwezo inaonesha kuwa uwiano kati ya Wanafunzi na vitabu umeendelea kuboreka kutoka wanafunzi 30 kutumia kitabu kimoja mwaka 2013 hadi wanafunzi 8 kwa mwaka 2014, hadi kufikia wanafunzi 3 kutumia kitabu kimoja kwa mwaka 2015.
Akiongelea kuhusu ufaulu katika somo la Kiswahili Mkurugenzi Mtendaji wa Twaweza Aidan Eyakuze alisema kuwa inatia moyo kuona watoto wetu wanapata matokeo mazuri zaidi kuliko miaka ya nyuma kwenye somo la Kiswahili.
Wakichangia mijadala katika halfa hiyo baadhi ya wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wameishauri serikali kuendelea kuweka mazingira mazuri ya watoto kufanya vizzuri katika masomo pamoja na kuboresha maslahi ya walimu ili kuwajengea morali katika kufundisha
Next Post Previous Post
Bukobawadau