Bukobawadau

TASWIRA MCHANA WA PASAKA MJINI BUKOBA

Pata matukio ya picha yaliyojiri mchana wa Pasaka Mjini Bukoba ,Kwa walioamini Pasaka  ni sikukuu ya kufanya ukumbusho wa kufufuka kwake Yesu Kristo
 Umati mkubwa wa Watoto na Vijana wa Umri mbalimbali wakielekea fukweni kufurahia Pasaka
 Wageni kutoka Ughaibuni wakifurahia siku yao katika fukwe za Bukoba Coop Hotel
 Fukweni Kiroyera Vijana wakiendelea kufurahia siku hii
 Kwa mahitaji yako ya Maji safi na salama basi Tanica drinking water ni Chaguo sahihi
Pembezoni mwa ziwa Victoria hapa ni Bukoba Coop Hotel ,zamani Yaasila
Utaratibu wa kuchukua matukio ukiendelea pande za fukweni ..
Swadakta kabisa unapata kujionea taswira mchana wa Pasaka mjini hapa April 16,2017.
Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri mchana wa pasaka Mjini Bukoba
Shangwe za pasaka zikiendelea kwa wadau kama wanavyo onekana wakiwa katika Mtumbwi wa ingine wakibalizi
Wadau wakiendelea na mizunguko ziwani.
Hakika sherehe hizi zimeweza kukusanya vijana wengi kama inavyo onekana pichani.
Fursa kwa wajasiriamali...
Makundi ya Watoto wakiwa wamejitokeza kwa wingi kufurahia sherehe ya pasaka
Maeneo ya Bukoba Coop Hotel, wadau wakiendelea kufurahia sherehe za pasaka
 Mpambanaji akiwa tayari kuwajibika kwa kutumia mtumbwi wake.
Eneo maalum kwa ajili ya watoto kucheza lililopo pembeni ya Kiroyera.
Muonekano wa Viwanja vya Bukoba Club
Bampa to pampa, Darajani Bukoba Club
Binti akicheck na Camera yetu, maeneo ya Walkgard Hotel ambayo kwa sasa ipo chini ya Kolping
Moja kwa moja kutoka kiwanja cha Walkgard Mlimani Kashura Bukoba
Wanyange hawa kama walivyokutwa na Camera yetu pande hizi za Walkgard Bukoba
Ms Parvin pichani
Mr Prospal na mwanae pichani wakiwa wametulia pande za Walkgard Hotel.
Mjini kati mtaa wa tupendani hali ikiwa ni tulivu sana.
Uso kwa uso na Mdau Linus pichani
 Mdau Linus akishow love mbele ya Camera yetu mchana wa pasaka April 16,2017
Stendi kuu ya Mabasi Mjini Bukoba
Mtaa wa tupendani, mtaa wa msambazi na muuzaji maarufu wa simu aina ya Tecno Omg Abdul (Koma) Galiatano
 Stendi kuu ya Mabasi yaendayo mikoani
Taswira mjini kati Bukoba...mchana wa pasaka April 16,2017
 Kuelekea mtaa ya Rwamugira mitaa maarufu kama Uswahili
 Katikati ya Mji,barabarani hali ni shwari kabisa
Mzee Ramadhani King kama alivyokutwa na Camera yetu mtaani
Jamhuri road kuelekea halmashauri
Transit Hotel The Walkgard.
Mwisho unaweza kupata habari mpya za uhakika kilahisi zaidi kwa kudownload Application ya Bukobawadau kwenye simu yako kutoka play store, Gonga hapa kudownload>>BUKOBAWADAU APP
Next Post Previous Post
Bukobawadau