Bukobawadau

UJUWE MJI MDOGO WA KATORO BUKOBA VIJIJINI

 Katoro (Bukoba) ni jina la kata ya Wilaya ya Bukoba Vijijini katika Mkoa wa Kagera, Tanzania. Kwa mujibu wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2002, kata ina wakazi wapatao 11,076 waishio humo.

Katoro ni kijiji chenye umaarufu wa kiimani kali,pamoja na mambo mengine Yupo Sheikh maarufu anaitwa Shekh mustapha Khalid,huyu ni kiongozi mwenye sifa kubwa humu duniani ,yeye na familia yake walipata kufungua chuo kikuu cha elimu ahela ambacho ni maarufu sana mpaka sasaNa Shule Za seminary Za kidini ukifika Katoro hakika unaziona harakati za hapa na pale,chuo hicho kina wanafunzi kutoka nchi mbalimbali za duniani na inasemekana products za chuo hicho ni perfect,Hivyo katika mkoa mzima wa Kagera Katoro ni sehemu iliyo dominated na Muslims,lakini dini zote zinaishi kwa amani na kuheshimiana kupo na kushirikiana katika harakati za kimaendeleo hiyo Ni moja ya sifa ya wanakagera

 Lugha kubwa kwa watu wa Katoro ni Kiswahili ,Kiganda ,Kihaya Na utawasikia watu wakiongea Kiarabu
Bukobawadau Media tumepata kutembelea mji huo wa kihistoria Kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ,kujua historia na kutunza tamaduni zetu wanakagera

Kutoka Katoro kwenda Kyaka ni umbali wa km 12 ,Ni mji mdogo unaokua kwa kasi na Idadi kubwa ya watu,Ukiwa Umezungukwa na Parokia ya ngarama, vijiji vya Musira,Ishenbulilo, ruhoko,ngalama ...🙌na Idadi ya misikiti ipatayo 15.
 Kwa taarifa mpya kutoka Ofisi ya Mkoa Kagera zinaonyesha kwa sasa Idadi ya watu imeongezeka katika kata ya Katoro na kufikia   13648 (M-6440 & F-7208)
 Siku maarufu ya gurio ni jumamosi, ambayo hukusanya watu toka vijiji vya karibu pamoja na wafanyabiashara toka nchini Uganda Kwa Kaggutta ukizingatia kata hiyo ipo jirani kabisa na Kyaka na ukitoka hapo unaelekea border ya mutukula Wilayani Missenyi na ni mwendo wa masaa 3 kwenda bukoba kwa usafiriwa wa Abiria au lisaa na nusu kwa Usafiri binafsi (Private) Katoro Ni Mji wa wakulima,wafanyabiashara na wafugaji changamoto kubwa ni miundombinu ya Maji na barabara.
 Muonekano wa Mitaa mbalimbali  ya Mji wa  katoro
 Waumini Wakiwa katika shughuli ya Maulid iliyofanyika hapo Katoro.
 Bango la moja wapo ya Shule ya Kiislam iliyopo Katoro Bukoba Vijijini

Kama tulivyoeleza awali Dini wao wanasema hapo ndipo kuna kijiji cha Itoma ulipo anzia Uislam kwa kutokea nchini Uganda.

 Sunset,Katoro Bukoba.
 Katikati ni Bi  Zahara Ramadhani Mrs bdulrazak (Rajesh) akiwa mbele ya Jengo la msikiti aliojitolea kuwajengea waumini wa Kijiji Cha Itoma-Katoro baada ya ule wa awali kuathirika kufuatia tetemeko la ardhi lililotekea,September 10 2016  Mkoani Kagera
 Napata kubadilishana mawazo na baadhi ya wazee Maarufu wakazi wa Mji wa Katoro nikipata machache kutoka kwa Mzee Adam Kabao.
Sheikh Farid Maulana akitoa mawaidha katika moja ya shughuli ya Kidini iliyofanyika Katoro pembeni yake wanaonekana viongozi mbalimbali wa Dini, Mzee Soud Fresh, mwenyekiti wa mkoa wa jumuiya Hajji Hashim Kamgunda (katikati)
 Kama unalolote kuhusu katoro ama kutoka eneo lolote ulilopo share nasi,tuandikie kupitia Email bukobawadau@gmail.com Whatsaap 0784505045

 #oldtown #touristlife #culture #history #tourist #photooftheday #bukobawadau #kagera #travel #historical #photography #life #lifestyle #lifestyleblogger
Next Post Previous Post
Bukobawadau