Bukobawadau

HABARI ZAHIVI PUNDE KUTOKA HOSPITALI YA MERCY,SIOUX CITY IA

Latest UPDATE:Mei 18, Alhamisi
Saa 4:30 Usiku (Masaa ya Afrika Mashariki)

Habari za HIVI PUNDE kutoka Hospitali ya Mercy, Sioux City IA
MTOTO Doreen amemaliza KUFANYIWA UPASUAJI wa UTI wa MGONGO, kwa KILE ambacho MADKTARI wamesema kumefanikiwa kwa UFANISI Mkubwa, KUPITA matarajio yao. MTOTO Doreen alikuwa afanyiwe UPASUAJI kwa makadrio ya MASAA 5:30, LAKINI zoezi HILO lilikamilika kwa muda wa MASAA 4:00, Huku TEAM ya "Surgical Support" IKIWA na watu 6, na kwa PAMOJA wakiongozwa na MADAKTARI BINGWA 2, Dr. Meyer na Dr. Durward. MTOTO Doreen amehamishwa KUTOKA chumba cha UPASUAJI na kupekewa ICU, na MADAKTARI wamesema KWAKUWA hali yake imeridhisha SANA, BAADAYE Leo watamtoa ICU ambako wamempumzisha baada ya UPASUAJI, na kumrudisha WODI ya WATOTO ambako ataendelea na MAPUMZIKO. MUNGU amesikia
MAOMBI ya WATANZANIA na WOTE waliotoa SALA na DUA zao kwa ajili ya MTOTO Doreen POPOTE Duniani.

 UPDATE:Mei 18, Alhamisi Saa 2:05 (Saa za Afrika ya Mashariki)
HIVI PUNDE, kutoka hospitali ya Mercy, Sioux City, IA
MTOTO Wilson kwa mara KWANZA ametoka NJE ya Jengo Kuu la Hospital ya Mercy akiwa kwenye "wheelchair", huku Mama na Daktari wake wakiwa na TABASAMU***
UPDATE:Mei 18, Saa 1:54 (Saa za Afrika Mashariki)
HIVI PUNDE, Mercy Hospital, Sioux City IA:
MTOTO Sadia akiwa na Dkt. Steve Joyce, ambaye ni Daktari wake wa "Internal Medicine". MADAKTARI wanasema Binti Sadia ni MUUJIZA wa Mungu kutokana na HALI aliyokuwa nayo KABLA ya huduma ya UPASUAJI. Asanteni SANA kwa DUA na SALA zenu
Next Post Previous Post
Bukobawadau