Bukobawadau

Kampuni ya Wazawa, yakamilisha hatua za Msingi kuuza hisa zake kwa watanzania - Maxmalipo

Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom  Africa Dr,Donalth Ulomi akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa kutangaza hati iliyopewa kampuni hiyo na Soko la hisa la Dar es salaam (Dar Es Salaam stock Exchange ) na kuanzia sasa itauza hisa zake kwa umma na kubadili jina lake kuwa Maxcom Africa PLC Maxmalipo ni Moja ya Kampuni zilizoanzishwa na kuendeshwa na wazawa watanzania ambayo imeifikia hatua za Mwisho katika kuuza hisa zake kwenye soko la hisa. Leo hii wametambulisha hati yao inayowafanya kuwa tayari kwa kuuza hisa kwa watanzania . Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2008 na mpaka leo imefika nchi zaidi ya 5 barani Africa.Hafla hiyo ya  uzinduzi wa uuzaji wa  hisa ulifanyika mapema leo katika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.

Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom  Africa Dr,Donalth Ulomi (kulia )  akikata utepe wa kuzindua rasmi uuzaji wa hisa za Maxcom Africa PLC anayeshuhudia ni Mkurungezi wa Uendeshaji wa Maxcom Africa Bw.Ahmed Lusasi mapema leo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.


Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom  Africa Dr,Donalth Ulomi (kulia )  akionesha nembo ya jina jipya Maxcom Africa PLC  kuzindua rasmi uuzaji wa hisa za kampuni hiyo kushoto kwake ni  Mkurungezi wa Uendeshaji wa Maxcom Africa Bw.Ahmed Lusasi mapema leo katika hafla ya uzinduzi iliyofanyika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaamwaandishi wa habari wakichukua matukio wakati wa hafla ya uzinduzi wa uuzaji wa hisa za Maxcom Africa mapema leo.
Mjumbe wa Bodi ya kampuni ya Maxcom  Africa Dr,Donalth Ulomi akifanya mahojiano na mwandishi wa habari mara baada ya uzinduzi rasmi wa uuzaji wa hisa za Maxcom Africa PLC.Maxmalipo ni Moja ya Kampuni zilizoanzishwa na kuendeshwa na wazawa watanzania ambayo imeifikia hatua za Mwisho katika kuuza hisa zake kwenye soko la hisa. Leo hii wametambulisha hati yao inayowafanya kuwa tayari kwa kuuza hisa kwa watanzania . Kampuni hii ilianzishwa mwaka 2008 na mpaka leo imefika nchi zaidi ya 5 barani Africa mapema leo katika hafla ya uzinduzi zilizofanyika makao makuu ya Maxcom Africa Kijitonyama Jijini Dar Es Salaam.

Next Post Previous Post
Bukobawadau