Bukobawadau

*YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 46 CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 LEO TAREHE 13 JUNI 2017*

#Katika kuongeza ari kwa Watumishi wa Umma Serikali imepunguza kiwango cha kodi ya mapato kwenye mshahara(PAYE) kutoka *asilimia* 14 Mwaka 2010/11 hadi *asilimia 9* Mwaka 2016/17.
#Serikali imeongeza kima cha chini cha mshahara kutoka *shilingi 100,000* Mwaka 2010/11 hadi *shilingi 300,000* Mwaka 2015/16
#Serikali imeanzisha *"Watumishi Housing Company Ltd"*kwa ajili ya kujenga nyumba za gharama nafuu na kuwauzia au kuwakopesha Watumishi.
#Serikali ina utaratibu mahususi wa kuangalia dawa,vifaa,vifaa tuba na vitendanishi kabla ya kuvitoa katika Bohari ya Dawa na kuvisambaza kwenda vituo vya Afya.
#Serikali inasimamia zoezi la kukifufua kiwanda cha Dodoma Wine Co. Ltd (DOWICO) cha mjini Dodoma.
#Serikali imepanga kujenga vituo vya Polisi,Magereza na nyumba za kuishi askari katika Wilaya zote nchini kwa awamu.
#Katika kipindi cha Oktoba,2015 hadi Aprili,2017 Jeshi la Polisi lilifanikiwa kukamata jumla ya watuhumiwa 9,140 wa dawa za kulevya.
*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO*
Next Post Previous Post
Bukobawadau