Bukobawadau

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 48 CHA MKUTANO WA SABA WA BUNGE LA 11 LEO TAREHE 15 JUNI 2017

#Serikali imeanza kutoa posho kila mwezi kama motisha kwa Walimu Wakuu,Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata ili kuimarisha uongozi na usimamizi wa elimu.
#Serikali inafanya mapitio ya majukumu ya watumishi wote wakiwemo walimu ili kuboresha maslahi ya watumishi wote kwa kuzingatia uzito wa kazi.
#Serikali imechapisha na kusambaza vitabu,chati na miongozo mbalimbali ya kufundishia na kujifunzia 8,359,868 kwa ajili ya darasa la 1 na 2.
#Serikali inaendelea na zoezi la kuviondoa vitabu visivyo hitajika katika matumizi kwenye shule za msingi na sekondari.
*IMEANDALIWA NA IDARA YA HABARI-MAELEZO*
Next Post Previous Post
Bukobawadau