Bukobawadau

KATIKA KONGAMANO LA KIISLAMU LA AFRIKA MASHARIKI WILAYANI MULEBA LEO JULY 29,2017

Jamii imetakiwa kuwatambua na kuwathamini wanawake kwenye ngazi mbalimbali kwa lengo la kuwatumia kuepukana na matendo yanayoweza kuhatarisha usalama na matukio yanayoangamiza dunia ya kuvunja amani
Wito huo umetolewa leo hii Julai 29, 2017 na Sheikh Kassim Yusufu Husein kutoka Mombasa nchini Kenya wakati akitoa mada ya thamani ya Mwananme kwenye kongamano la dini ya kiislamu lililoandaliwa na Taasisi ya Ansary Muslimu iliyoko hapa nchini  ambalo limejumuisha masheikh kutoka nchi za Afrika Mashariki.
Sheikh Kassim Yusufu Husein amesema wanawake wanayo majukumu makubwa katika kulea familia hasa watoto wa jinsia zote lakini wamejaliwa na Mungu kulea hata waume zao kiuadilifu iwapo mwanaume huyo naye atakuwa amelwlewa kwa misingi ya kiimani katika matendo yanayokubaliwa na Mwenyezi Mungu
Amesema katika kuwathamini wanawake hao wanatakiwa kuwa na sifa  kadhaa mojawapo kuwa na elimu ya dini  ya kiislamu kutambua miiko na mafundisho dini ikiwemo ya elimu dunia kwa ajili ya kudhibiti matukio ya kuwanyima haki zao katika familia na kwenye mazingira yanayomzunguka.
Amesema sifa nyingine ni kuwa na hekima katika kuweka vitu mbalimbali kwa kila kimoja kuwa katika mahali pake na hekima hiyo itamsaidia kuwalea watoto wake na  mumewe na upatikanaji wake hutegemea mazingira katika utoaji wa malezi.
Aidha Naibu Mudil wa baraza la Wanasuna Tanzania (BASUTA) Sheikh Ally Zuberi kutoka mkoani Tanga nchini Tanzania  amewataka waumini wa dini ya Kiislamu kuitafuta elimu kama alivyoamrishwa amtume Mohamadi SAW ili kujihadhari na kubeba pipa laa moto siku ya Kiama baada ya kuondoka duniani
Kongamano hilo lililoanza jana Ijumaa  limehudhuriwa na masheik na waumini mbalimbali kutoka ndani na nje ya Tanzania wakiwa pamoja wilayani Muleba mkoani Kagera huku baadhi yao wakifanya biashara ya dawa za maradhi yanayomsibu mwanadamu, lakini kukiuzwa mavazi ya kislamu kwa wqanaume na wanawake.
Mgeni rasmi katika mihadhara ya kongamano hilo ni Sheikh Alif Nahad ambaye ni  Mkurugenzi wa Taasisi ya The Islamic Foundation Makao Makuu yaliyopo Mkoani Morogoro inayomiliki kituo cha TV , Radio Imaan na gazeti la Kiislamu la Imaan. 
 Wanafunzi wa kiislamu wa Jakaya English medium school iliyoko muleba mjini wakiwa jukwaani kwenye kongamano hilo
Muonekan wa baadhi ya Wanafunzi wa kiislamu wa Jakaya English medium school iliyoko muleba mjini wakiwa jukwaani kwenye kongamano hilo
Picha zote Kwa hisani kubwa ya Mwanahabari wetu Shaaban Ndyamukama, MULEBA
Next Post Previous Post
Bukobawadau