Bukobawadau

WAZIRI MAHIGA APOKEA NAKALA ZA HATI ZA UTAMBULISHO ZA BALOZI MTEULE WA UGANDA NCHINI TANZANI MKOANI KAGERA

• Kikao cha Ujirani Mwema Kati ya Tanzania na Uganda chafanyia Mjini Bukoba
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Augustine Mahiga akiwa Mkoani Kagera apokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule wa Uganda nchini Tanzania Richard Kabonelo ` ambaye anachukua nafasi ya Balozi aliyemaliza muda wake Doroth Hyuha.
Waziri Mahiga mara baada ya kupokea nakala za hati za utambulisho za Balozi Mteule Richard Kabonelo alisema zoezi hilo limefanyika kwa mara ya kwanza nchini mkoani ambapo limefanyika hapa Kagera ambapo mara zote hufanyika Jijini Dar es Salaam. 
Balozi Mteule kabla ya kuwasilisha hati zake za utambulisho kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani kwanza huwasilisha nakala za hati hizo kwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo Balozi Mteule Richard Kabonelo anatarajia kuwasilisha hati za utambulisho kwa Rais Magufuli tarehe 01.08.2017
Aidha Waziri Mahiga alitumia nafasi hiyo kueleza juu ya mkutano wa ujirani mwema kati ya Tanzania na Uganda ambao unafanyika leo Julai 29, 2017 katika Hoteli ya ELCT Bukoba ambapo upande wa Tanzania unawakilishwa na wajumbe 42 na kuongozwa na yeye Waziri Mahiga na Upande wa Uganda wenye wajumbe 35 unaongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo Sam Kutesa.
Kabla ya Mkutano wa Mawaziri Julai 29, 2017 upande wa Tanzania Ukiongozwa na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Likuvi ulitembelea mpaka wa Tanzania na Uganda eneo la Kakunyu na Mtukula na kutembelea mawe namba 27, 28, 29 ya mipaka na kuona changamoto zake na kuongea na wananchi wan chi mbili wanaoishi karibu na mpaka huo.
Waziri Mahiga akitoa ufafanuzi alisema kuwa mpaka huo uliwekwa na Wakoloni mwaka 1902 zaidi ya miaka 100 iliyopita na kadri miaka inavyoendelea watu wanazidi kuongezeka pamoja na mifugo jamabo amabalo linapelekea kuwepo kwa changamoto za uhamiaji haramu na mifugo kuingia nchini kuharibu mazingira.
Aidha, Waziri Mahiga alisema kuwa mipaka iliyowekwa na wakoloni kwenye ramani ni mistari iliyochorwa lakini kihuhalisia kuna changamoto mipaka hiyo ilipo kwenye ardhi. “Tunataka kuweka alama nyingi za mipaka ili ionekne wazi japo kuwa sisi ni Wanajumuiya ya Afrika Mashariki lakini lazima mipaka yetu ionekane na iendelee kuheshimika.” Alifafanua Waziri Mahiga.
Baada ya Mkutano wa leo Julai 29, 2017 Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi mbili Tanzania na Uganda wanatarajia kusaini makubaliano ambapo Makatibu Wakuu wa Wizara kutoka Tanzania na Uganda tayari wamefanya vikao kwa siku tatu na kuwasilisha mapendekezo yao kwa Mawaziri ambayo yakikubalika pande zote mbili yanasainiwa kama makubaliano rasmi.
Next Post Previous Post
Bukobawadau