Bukobawadau

MZEE GOTFRIED RWELA MKAZI WA KARAGWE ASHEREKEA MIAKA 100 YA KUZALIWA KWAKE!

Mkazi wa Kijiji cha Kinyinya, wilayani Karagwe mkoani Kagera, Gotfried Rwela akikata keki wakati akisherehekea kutimiza umri wa miaka 100 , katika hafla iliyofanyika nyumbani kwake, jana. Gotfried amezaliwa mwaka 1917 ana wake wawili, watoto 18, wajukuu 49 na vitukuu 19.
KARAGWE:Jamii imetakiwa kuwalea  watoto na mama zao kwa  kuzingatia  misingi ya imani zao za kiroho katika kufundisha maadili mema na kuwafanya watoto hao kuwa na tabia njema ya kuthaminiana baina yao na walezi wanaowazunguka.
Wito huo umetolewa na mzee mmoja mkazi wa kitongoji cha Kinyinya  katika kijiji cha Kituntu wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Mzee Gotfried Ruyumbu Rwela ambaye alikuwa akifanya sherehe  ya kufikisha miaka 100 ya kuzaliwa wilayani humo na kwamba upendo  na maadili vimemsaidia kuishi maisha marefu
Mzee Rwela amesema katika kufanya kazi za kijamii watumishi wa sekta mbalimbali  wanatakiwa kutanguliza uaminifu ,utiifu na ubunifu kwa kuhakikisha yanapatikana  maendeleo kwa kila mmoja kutimiza wajibu na   majukumu yake.
Aidha mzee huyo alizaliwa mwaka 1917 na kuanza shule mwaka 1935 kisha kuanza kazi ya ualimu wa shule za msingi mwaka 1952 amejaliwa kuwa na  wanawake wawili na watoto 18,  wajukuu 49 na vitukuu 19 
Katika utumishi wake kama mwalimu alifundisha wanafunzi wengi akianzia mkoani Shinyanga mwaka 1962 na amestaafu mwaka 1982  akiwa wilayani Karagwe ambaye amedai kwamba  katika mfumo wa maisha ya familia msingi mkubwa ni upendo, nidhamu na kuunganisha umoja kwa watoto jinsia zote
Baadhi ya viongozi na watu  wa  rika tofauti wakiwemo watoto wake,  wajukuu na vitukuu wamempongeza mzee huyo kufikisha umri wa miaka 100 ya kuzaliwa wakimuombea maisha marefu kuendeleza hekima, upendo na  malezi ya kiroho
 Mzee Gotfried Rwela akiwa katika picha ya pamoja na watoto wake wa kuwazaa.
 Pichani wapo wanafamilia na baadhi ya wazee waliobahatika kusima na Mzee Gotfried Rwela
 Pichani ni Vitukuu wa Mzee Gotfried Rwela wakati wa utambulisho
 Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri katika sherehe hiyo
 Picha zote kwa hisani ya Shaaban Ndyamukama
 Pongezi zikiendelea kutoka kwa wazee mbalimbali aliosoma nao na kufanya nao Kazi akiwemo Askofu Mstaafu ya ELCT Dayosisi ya Kagera
Next Post Previous Post
Bukobawadau