Viongozi wa Dini wakiwaongoza Maelfu ya wananchi kushiriki Dua maalum ya kumuombea Alhaji Abbakari Rajabu Galiatano kabla ya shughuli ya mazishi yaliyofanyika nyumbani kwake kijijini Buganguzi Muleba siku ya Jumapili Julai 9,2017.
Shukrani:Familia ya Al hajji Mzee Abubakari Rajabu Galiatano inapenda kutoa
shukrani nyingi sana na za kipekee kwa ndugu,Jamaa ,marafiki,majirani na
viongozi wa Dini na siasa wote kwa kujitoa kwa hali na mali
kufanikisha shughuli za mazishi ya Mzee Abubakari Rajabu Galiatano
aliyefariki siku ya Jumamosi tarehe 8 Julai,2017 na kuzikwa siku ya
Jumapili Julai 9,2017 nyumbani kwake kijijini Buganguzi Muleba.
Ni vigumu kushukuru mtu mmoja mmoja kutokana na wingi wenu na kwa jinsi kila
mmoja alivyojitoa na kuonesha upendo wa dhati kabla na baada ya
mazishi. Tunaweza kujaza kurasa 200 kama hizi na tusiwe tumehitimisha
robo tu ya shukrani zetu kwa kila mmoja wenu.
TUNAWAOMBEA KWA MOLA AWAJALIE KATIKA KILA JAMBO.
Pamoja na hayo shukrani za kipekee ziwaendee uongozi na madaktari wa
hospitali zifuatazo :Hospital Aga Khan,Hospitali ya St.John
Bukoba,hospitali ya Mkoa Kagera, Rabinisia Dar es Salaam,CCBRT na
Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Asanteni! Asanteni! Asanteni! na Mungu awabariki katika maisha yenu.
Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un..!!
Shekh wa Mkoa wa Kagera Sheikh Haruna Kichwabuta akitoa nasaha zake katika msiba huo mkubwa kwa wanakagera
Ndugu Al Amin Abdul na Bwana Sued Kagasheki wakielekea eneo la makaburi kwa ajili ya kushiriki mazishi ya Mzee Abubakari Rajabu Galiatano
Mamia ya waombolezaji wakiongozana kuelekea eneo la makaburi
Waombolezaji wakielekea eneo la makaburi kwa ajili ya kushiriki mazishi ya Mzee Abubakari Rajabu Galiatano
Endelea kuwa nasi kwa matukio zaidi ya picha....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comment:
Post a Comment