BALOZI KAMALA ATEMBELEA KATA KITOBO NA KUZINDUA MRADI WA DARAJA LA KYANKOKO
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala pichani wakati akizindua Daraja hilo lililogharimu kiasi cha shilingi milioni kumi na nne za kitanzania (Tsh 14,000,0000)kulia pichani ni Diwani wa Kata ya Kitobo Mh.Willy Mtayoba.
Muonekano wa Daraja la Kyankoko lililopewa jina la Novati Rutegaruka Memorial Bridge Daraja linalovikutanisha Vijiji vya Msibuka na Kayanga katika Kata ya Kitobo Wilayani Missenyi
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala (pichani) akiongea na wananchi wa Kijiji cha Kashasha kata Kitobo waliohudhuria katika mkutano wake wa hadhara,Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala ameweza kuchangia miradi ya maendeleo inayoendelea katika kata hiyo na pamoja na kuahidi kuzifanyia kazi kero mbalimbali kama Uhaba wa wauguzi katika Zahanati na vituo vya Afya,Utaratibu wa Bima ya Afya kwa Wazee na watu wenye Ulemavu kwa kuwapunguzia changamoto wanazokutana
Sehemu ya wananchi wakifatilia kwa umakini wakati mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiendelea kuwahutubia na kufanya majumuhisho ya changamoto alizozibaini katika ziara yake ya Siku 17 Jimboni Mwake.
Baadhi ya wananchi waliohudhurio mkutano wameweza kupata nafasi ya kuelezea Kero zinazowakabili licha ya kuwepo mafanikio katika utatuzi wa baadhi ya kero kupitia kwa Mbunge wao Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
Muonekano wa baaadhi Baadhi ya wananchi waliohudhurio mkutano wameweza kupata nafasi ya kuelezea Kero zinazowakabili licha ya kuwepo mafanikio katika utatuzi wa baadhi ya kero kupitia kwa Mbunge wao Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
Kama kawaida Balozi Dr. Diodorus Buberwa anakua karibu na wananchi wake na kuhakikisha anatoa nafasi ya kupokea kero zao kama wanavyo onekana pichani baadhi ya wananchi wakitoa hoja mbele ya Mbunge wao
Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiendelea kuwahutubia wananchi wa Kata Kitobo walihudhurio mkutano wake uliofanyika Jana katika Viwanja vya Shule ya Msingi Kashasha Kitobo
Mwanahabari Respicius John wa Radio Karagwe akiwajibika katika Mkutano wa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala.
Wananchi wakifurahia jambo katika mkutano huo uliofanyika Jana katika Kijiji cha Kashasha kata Kitobo Wilayani Missenyi,Picha kwa hisani ya #bukobawadaumedia
Afisa Maendeleo Kata Kitobo Saudi Crispian wakati akisoma taarifa ya maendeleo ya kata kwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Balozi Dr. Diodorus Buberwa alipotembelea kata hiyo, Balozi Dr.Kamala amehitisha ziara yake kwa kutembelea maeneo mbalimbali kwa kukagua miradi ya maendeleo na kubaini namna miradi mingi ya Maji Wilayani Missenyi ilivyotekelezwa chini ya kiwango.
Baadhi ya wananchi waliohudhurio mkutano wameweza kupata nafasi ya kuelezea Kero zinazowakabili licha ya kuwepo mafanikio katika utatuzi wa baadhi ya kero kupitia kwa Mbunge wao Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
Taswira mbalimbali eneo la mkutano wa Mbunge wa Balozi Balozi Dr. Diodorus Buberwa uliofanyika jana Aug,2017 katika kijiji cha Kashasha Kata Kitobo Wilayani Missenyi
Mzee Rweyemamu Kabandwa akielezea kero yake
Wanaonekana Vijana katika hali ya umakini wakimsikiliza Mbunge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala.
Diwani wa Kata ya Kitobo Mh.Willy Mtayoba akitolea jambo ufafanuzi katika mkutano wa Mbunge uliofanyika jana Aug,2017 katika Viwanja vya shule ya msingi Kashasha
Wananchi wakifatilia maelezo kutoka kwa Diwani wao.
Kabla ya Mkutano wa hadhara Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala aliweza kuzindua Chumba cha Darasa kilichojengwa na Michango ya wadau na fedha kutoka mfuko wa Mbunge wa Jimbo la Nkenge
Muonekano wa Bango mlangoni mara baada ya uzinduzi rasmi kufanyika.
Wadau wakisogea eneo la tukio kumsikiliza Mbunge wao Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala.
#BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045,0754 505043