Bukobawadau

MAMIA WAMZIKA HAJJAT MASTURA ABDALLAH KIJIJINI KATORO BUKOBA

 Mamia ya waombolezaji wameweza kushiriki maziko ya aliyekuwa mhamasishaji wa maswala mbalimbali ya maendeleo,Mhasisi wa Chama na Muumini mzuri wa dini yake ya Kiislam Hajjat Mastura Abdallah Kagangane (102) Nyumbani kwake Kijijini Itoma Katoro -Bukoba
 Marehemu Hajjat Mastura Abdallah pichani enzi za Uhai wake,Inshallah Mwenyezi mungu ampokee
Bukobawadau Blog media tunakufikishia mtiririko wa matukio ya picha yaliyojiri katika  msiba huu mkubwa kwa wanakatoro.
Sehemu ya Waumini waliohudhuria maziko hayo yaliyofanyika Jumamosi Aug 12,2017 Kijijini Itoma katoro
 Sheikh Farid Maulana akitoa mawaidha katika shughuli ya mazishi ya Marehemu Hajjat Mastura Abdallah Kagangani yaliyofanyika siku ya Jumamosi Aug 12,2017 Nyumbani kwa marehemu Itoma-katoro Bukoba Vijijini.
Sheikh Farid Maulanaakiendelea kutoa mawahidha kwa mamia ya waombolezaji walihudhuria shughuli ya maziko ya Hajjat Mastura Abdallah.
Taswira mbalimbali eneo la tukio ,Mazishi ya Hajjat Mastura Abdallah.
Umati wa waombolezaji wakiendelea kusikiliza mawahidha yanayotolewa
Muendelezo ya matukio ya picha kutoko msibani hapo
Wanaonekana baadhi ya waombolezaji upande wa wanawake.
Ni simanzi kubwa kwa wanafamilia wote.
Poleni sana wanafamilia kwa kuondokewa na mpendwa wetu Hajjat Mastura Abdallah
Muda mchache kabla ya kusalia jeneza la Hajjat Mastura Abdallah.
Jeneza la Hajjath Mastura Abdalla likiwa linasaliwa..
 Waumini wakisalia Jeneza la Hajjat Mastura.
Jeneza la Hajjat Mastura Abdalla likiwa limebebwa kuelekea eneo la Kaburi lilipo shambani kwake.
 Jeneza likiwa likiingizwa kwenye Kaburi
Hivi ndivyo ilivyokuwa safari ya mwisho ya Maisha ya Hajjat Mastura Abdallah
Eneo la kaburi Shughuli ya Maziko ikiendelea.

 Utaratibu wa kuweka Udongo ukiwa unaendelea.
Sehemu ya wanafamilia wakiwa eneo la kaburi kwa ajili ya kumstiri Mzazi wao mpendwa Marehemu Hajjat Mastura Abdallah
Pichani katikati anaonekana Kijana Moha Mzee Nyundo
Utaratibu wa kuweka Udongo kumstiri mzazi wetu, Bibi yetu Hajjat Mastura Abdallah
Mtoto pekee wa kiume wa kuzaliwa na Marehemu Hajjat Mastura akiweka udongo kwenye kaburi.
 Muonekano wa waombolezaji wakiwa eneo la kaburi kushiriki Maziko hayo
Shughuli ya maziko ikiwa inaendelea
Inshallah mwenyezi Mungu ampokee amsamehe makosa yake amuondolee adhabu ya kaburi na ampe makazi yalokua mema peponi 

Eneo la kaburi shughuli ya maziko ikiendelea
Neno la shukrani kutoka kwenye familia ya Marehemu Hajjat Mastura Abdalla aliyefariki akiwa na Umri wa miaka 102.
Mawadha kutoka kwa Sheikh.
Mjomba wa Marehemu Hajjat Mastura Abdallah akitoa neno na kuwashukuru watu wote walioweza kushiriki maziko hayo.
Katikati ni Msanii Najima Dattan akiwa ameungana  na wanafamilia kufuatia msiba wa Mpendwa Bibi yake Hajjat Mastura Abdallah.
Wadau wakibadilishana mawazo
Picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu kupitia Bukobawadau Media
 Mama Abdallah pichani mmoja kati ya watoto 6 wa kuzaliwa na Marehemu Hajjat Mastura
 Katika hili na lile mara baada ya maziko kukamilika
 Shukrani kwako wewe msomaji kuendelea kufatilia Mtandao wetu wa Bukobawadau
 Muendelezo wa matukio ya picha
 Vilio na machozi wakiendelea kuwatoka wafiwa.
 Poleni sana wafika pole sana ndugu kwa kumpoteza mzazi .
 Naam hivi ndivyo Mamia ya waombolezaji kutoka maeneo mbalimbali walivyoweza kushiriki maziko ya aliyekuwa mhamasishaji wa maswala mbalimbali ya maendeleo,Mhasisi wa Chama na Muumini mzuri wa dini yake ya Kiislam Hajjat Mastura Abdallah Kagangane (102) Nyumbani kwake Kijijini Itoma Katoro -Bukoba siku ya Jumamosi Aug 12,2017
 Wanafamilia wakibadilishana mawazo mara baada ya shughuli ya maziko hayo
 Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri msibani hapo
 Baada ya Maziko kinachofuata ni kupata ubani ulioandaliwa....
 Kama unavyojionea hapa chakula kikiwa tayari kimepakuliwa...!
 Upande wa jikoni maandalizi yakiendelea wakati huo
Matukio ya watu kupata ubani ulioandaliwa kabla na baada ya mazishi ya Hajjat Mastura Abdallah
 Wanafamilia muda mchache baada ya kuwasili Mjini Bukoba tayari kwa safari kuelekea Kijijini Katoro kushiriki maziko ya mpendwa Wao Hajjat Mastura
Kushoto ni Sheikh Farid Maulana akiwa ameongozana na Alhaji Sheikh Hashim Hassa Kamugunda Mwenyekiti wa Jumuiya ya Imamu Shafii Mkoa Kagera na makamu Mwenyekiti Taifa waislamu madhehebu Shafii ,Kuwapokea wafiwa waliokuwa wakiwasili Uwanja wa Ndege mjini Bukoba
Bi Zahara wakati anawasili kwa ajili ya kushiriki mazishi ya Mama yake mzazi hajjat Mastura Abdallah (102.) aliyefariki baada ya kuugua kwa muda mfupi
Ndugu Abdulrazak Dattan akiwa ameongozana na mke wake pamoja na wanafamilia.
BUKOBAWADAU tunatoa pole kwa wafiwa wote, Mwenyezi Mungu awepe nguvu, na pia tunamuombea Marehemu apumzike kwa amani...!!

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un!! 
Matukio ya picha zaidi ya 200 yanapatikana katika ukurasa wetu wa facebook,jiunge nasi kwa ku'share na ku - like >>BUKOBAWADAU MEDIA
Next Post Previous Post
Bukobawadau