Bukobawadau

UZINDUZI WA BODI YA NNE YA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA KAGERA ULIOAMBANA NA UZINDUZI WA DUKA LA DAWA LA HOSPITALI

 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (mst) Salum M.Kijuu azindua Bodi ya Nnne ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kagera ulioambatana na Duka la Dawa la Hospitali.
Duka hilo ni maalumu kwa ajili ya kuuza dawa hasa zile ambazo zinahitajika lakini hazipatikani katika Bohari ya Dawa (Medical Stores Department - MSD).
Lengo ikiwa ni kuhakikisha dawa za msingi zinapatikana ndani ya Hospitali na hivyo kumpunguzia mgongwa usumbufu wa kwenda nje kununua dawa tena kwa bei ya Juu.

Rc Kijuu ametoa pongezi kwa Katibu Tawala wa Mkoa,Mganga Mkuu wa Mkoa na timu nzima ya Hospitali pamoja na Bodi ya Hospitali iliyomaliza muda wake kwa kusamia na kuhakikisha Duka hilo linakuwepo na linaanza kutoa huduma
 Baadhi ya wajumbe wapya na wajumbe wastaafu katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa
 Aidha Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (mst) Salum M.Kijuu ametoa wito kwa Viongozi wa Hospitali kuhakikisha kuwa duka hilo linaendelea kuwepo na kuboreshwa ili litoe huduma nzuri zaidi #Orodha ya Wajumbe wapya wa Bodi ya nne waliochanguliwa ni Bw. Pius Ngeze mwenyekiti,wengine ni Askofu Method Kilaini,Sheikh Haruna Kichwabuta,Bw. Amir Hamza,Bw.Hamis Edward Mwisa,Bi Esselina K. Rugakingira ,Bw Elias J.Mashasi ,Bi Prucheria Stanslaus, Bi Pudensiana Rwezaula,Bw. Philberth G. Nyamututu,Bw. Murshid Ngeze, Mh. Oliva D.Semuguruka, BW. Hashim Ngole,Dr. Thomas Rutachunzibwa na Dr. John Mwombeki.
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (mst) Salum M.Kijuu akihutubia katika hafla fupi ya tukio muhimu la Uzinduzi wa Bodi ya Ushauri ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
 Bw. Philbart Gosbart mmoja wa wadau waliohudhuria uzinduzi wa Bodi ya nne ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera sambamba na Uzinduzi wa Duka la Dawa la Hospitali
 Bw. Pius Ngeze Mwenyekiti mpya wa Bodi ya nne ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera
 Muongozaji mshereheshaji wa shughuli ya Uziduzi huo uliofanyika Jana Alhamis Agosti 17,2017
 Muonekano wa Jengo la Duka la Dawa lililotengenezwa kwa matengenezo ya miundombinu kwa takribani shilingi Milioni ishirini na mbili (Tsh 22 M) na kiasi cha shilingi milioni thelathini (Tshs. 30m)
 Muda mchache kabla ya Uzinduzi rasmi wa Duka la Dawa la Hospitali ya Mkoa
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali (mst) Salum M.Kijuu akizundua Duka la Dawa la Hospitali ya Mkoa Kagera
  Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wakiendelea kufatilia matukio yanayojili katika tukio hilo.
 Sehemu ya wafanyakazi wa Hospitali na baadhi ya wanahabari wakifatilia kinachojiri
Baadhi ya wafanyakazi wa hospitali ya Mkoa Kagera
 Taswira mbalimbali eneo la tukio
 Mmoja wataja wa kwanza walioweza kupata huduma katika Duka la Dawa la Hospitali ya Mkoa akiongea na wanahabari
 Bi Rukia Kassim mfanyakazi wa Hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Kagera
  Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wakiendelea kufatilia hotuba ya mgeni Rasmi
 Baadhi ya wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wakiendelea kufatilia hotuba ya mgeni Rasmi
 Aliyekuwa mwenyekiti wa bodi iliyomaliza muda wake Bw. Johansen Lutabingwa akitoa neno
  Sehemu ya wadau na wafanyakazi wa Hospitali ya Mkoa wakiendelea kufatilia hotuba ya mgeni Rasmi katika
 Wadau mbalimbali walioshiriki shughuli ya Uzinduzi wa Bodi ya Nne ya Hospitali sambamba na Uzinduzi  Duka la Dawa la Hospitali uliofanyika Agosti 17,2017
 Bi Hafsa Galiatano Mwenyekiti wa Halmashauri ya Biharamulo
 Bi Sarah Muhasibu msaidizi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera
Mh. Oliva D.Semuguruka  Mjumbe wa Bodi ya Nne mpya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Kagera

 Bukobawadau Aug 18,2017
Next Post Previous Post
Bukobawadau