Bukobawadau

TUNDU LISSU ASAFIRISHWA KWENDA NAIROBI KWA MATIBABU ZAIDI


 

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kupitia ukurasa wake wa facebook usiku huu ameandika ;Leo Alhamisi 7/09/2017, Mwanasheria Mkuu wetu wa chama chetu cha CHADEMA, Mhe. Tundu Antipas Lissu, wakati anarudi nyumbani kwake, akitokea Bungeni alifanyiwa shambulizi la risasi.
Gari iliyokuwa ikifuata gari yake nyuma, ghafla ilitoa bunduki na kuanza kummiminia risasi na risasi kadhaa zimemjeruhi.
Alipelekwa hospitali kwenye chumba cha upasuaji ili kuona risasi zilizomuingia tumboni na maeneo mengine mbalimbali ya mwili zimesababisha madhara kiasi gani.

Tuendelee kumuombea Mhe. Lissu wakati anaposafirishwa nje ya nchi kwa matibabu zaidi huku tukisubiri taarifa rasmi kutoka kwenye chama kuhusu hatua nyingine kuhusu masuala mbalimbali.@freemanmbowetz

TunduLissu akipakiwa kwenye ndege usiku huu tayari kwa safari ya Nairobi kwa matibabu zaidi
Next Post Previous Post
Bukobawadau