Bukobawadau

MAMIA WASHIRIKI MAZISHI YA MCH.EGBERT MWESIGWA KANYAMBO HUKO KAGOMA MULEBA

Mamia ya waumini wa madhehebu mbalimbali,maaskofu na wachungaji wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania wamejitokeza kwa wingi kushiriki mazishi ya Marehemu Mchungaji Egebart Kanyambo yaliyofanyika nyumbani kwake Kijijini Kagoma Muleba,Siku ya Jana Oct 23,3017 shughuli iliyoongozwa na Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Dkt. Abednego Keshomshahara
 Baadhi ya waombolezaji wakiendelea kushiriki Marehemu Mchungaji Egbert Kanyambo yaliyofanyika nyumbani kwake Kijijini Kagoma Muleba,Siku ya Jana Oct 23,3017
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi-Bukoba Abedinego Keshomshahara akiongozi Ibada ya Mazishi ya Mchungaji Egbert Kanyambo.
 Mchungazi Egbert Mwesigwa Kanyambo pichani enzi za Uhai wake Mchungaji Egbert Mwesigwa Kanyambo alizaliwa tarehe 14/10/1961 katika kijiji cha Kagoma,kata Kagoma usharika wa Kagoma akiwa ni mtoto wa tano (5) kati ya watoto tisa (9) wa familia ya Mzee Obadia na Bibi Estelia Kanyambo.
Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Dkt. Abednego Keshomshahara akiongoza Ibada ya maziko
Pichani wanafamilia machozi na vilio vikiwatoka wakati jeneza lenye mwili wa Mch. Egbert Kanyambo linatolewa ndani.
 Wachungaji wakiwa wamebeba jeneza lenye mwili wa mpendwa wetu Mchungaji Egbert Kanyambo
Umati wa waombolezaji wakiwa tayari kushiriki Ibada ya mazishi Mchungaji Egebert Kanyambo aliyebarikiwa kuwa Mchungaji wa DKMG mnamo tarehe 16/12/1090 na kupata kutoa kutoa huduma ya Uchungaji wa Usharika Kanyinya miaka 1991-1921 na kuwa mchungaji na mwalimu wa Elimu ya Kikristo mashuleni chini ya Ofisi ya Idara ya Elimu ,DKMG
Pichani ni Mama Basheleka mzazi wa Mjane wa Mchungaji Egebert Kanyambo.
Katika picha ni muendelezo wa matukio yaliyojiri katika Ibada ya Maziko ya Mchungaji Egebert Kanyambo.
Shemasi Pesha pichani kushoto akibadilishana mawazo na mwenzako
Sehemu ya wachungaji wa kilutheri wakiendelea kushiriki shughuli ya kumuaga mwenzao
Sehemu ya wanafamilia ya Mch.Egbert Kanyambo wakiendelea kushiriki
Zoezi ya kutoa heshima za mwisho kumuaga mpendwa wetu mchungaji Egbert Kanyambo katika picha.
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho
Muendelezo wa matukio ya picha Ibada ya maziko ya mchungaji Egbert Kanyambo ikuendelea
Watoto wa marehemu wakiongozana na mama yao kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa mzazi wao Mchungaji Egbert Mwesiga Kanyambo

Utaratibu wa kutoa heshimaza mwisho ukiendelea kwa watu wote
Dada Libe pichani akiwa na huzuni mkubwa wakati wa kutoka heshima zake za mwisho kumuuaga mpendwa shemeji yake Mchungaji Egbert Mwesiga Kanyambo
Bi Febronia Abela Kanyambo (Mjane) akitoa neno na shukrani kwa wote walioweza kushiriki kwa namna moja ama nyingine katika kipindi chote cha kumuuguza mme wake mpendwa
Mama mjane anabahinisha kuwa  marehemu  alikuwa akisumbuliwa na Ugonjwa wa Saratani tangu mwaka 2014 ambapo alikuwa akipata matibabu katika Hospitali za ELCT Bukoba Town Health Center (BTHC),Ndolage,Bugando ,Ocean road,Muhimbili na Amana.
Bi Febronia Abela Kanyambo amesema; Wataalam wameshughulika sana kunusuli maisha ya mme wake mpendwa lakini mapenzi ya mungu yametimia na kukutwa na mauti tarehe 17/10/2017 akiwa katika hospitali ya Amani iliyopo Jijini Dar es Salaa.
Huzuni na Simanzi vikitawa kwa watu wote
Salaam za rambirambi

Mama mjane akitoashukrani kwa mwajiri wake mara baada ya kupokea rambirambi
Salaam za rambirambi kutoka kwa Mh.Charles Mwijage Muleba Kasikazini (CCM) Charles Mwijage
Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi-Bukoba Abedinego  mara baada ya kukabidhi rambirambi za Kanisa
Bwana Jonas Lweza akisoma wasifu wa Mchungaji Egbary
Msemaji wa familia akitoa neno la shukrani
BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045?0754 505043
Mdau Subra (KPC)Kabyemela akiwa amejumuika na watu wengine kushiriki mazishi hayo
Kaka Menshack Kanyambo ambaye ni mdogo wa marehemu akitoa shukrani kwa wote walioshiriki kusaidia kwa namna moja ama nyingine katika juhudu za kuokoa maisha ya Kaka yeke.
Hii ni baada yashukrani za pekee kutolewa kwake Libe na mme wake kufuatia jitihada zao na walivyojitoa kuhakika marehemu Mchungaji anapata huduma safi na tiba bora
Mdau pichana akiwa amesima wakati wa shukrani zake za dhati kutoka kwa familia ya Marehemu Mchungaji Egbert Mwesiga
Mama Muhazi pichani

Ibada ya mazishi wakati inaendelea
Muendelezo wa matukio ya picha Ibada ya maziko ya mchungaji Egbert Kanyambo
Wadai wakibadilishana mawazo mara baada ya shughuli ya maziko
 Taswira eneo la tukio wakati Ibada ya maziko inaendelea.
Kuelekea eneo la kaburi hakika Mungu aipokee roho ya mchungaji Egbert Kanyambo
Jeneza likiwa tayari kuingizwa kaburi
Waombolezaji kutoka maeneo  mbalimbali wakiendelea kushiriki maziko hayo

Utaratibu wa kuweka udongo kwenye kaburi ukiendelea

Wachungaji wakishiriki zoezi la kuweka udongo kwenye kaburi
Ndugu wa marehemu wakiweka Udongo kwenye kaburi
Watoto wa marehemu wakiongozana na mama yao kuweka udongo kwenye kaburi



  Askofu Dkt. Abednego Keshomshahara akisimika msalaba kwenye kaburi
Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Dkt. Abednego Keshomshahara akiwa tayari kuweka shada la maua
Zoezi la kuweka shada la maua likiwa linaendelea
Mama Mjane Bi Febronia Abela akiweka shada la maua
Mjane na watoto watatu wa kuzaliwa na Mchungaji Egbert Kanyambo wakiwa shada la maua
 Pembezoni wakati shughuli ya maziko inaendelea pichani Bi Parvin akibadilishana mawazo na Mwaliu Beatrice



Mr &Mrs Matungwa wakiweka shada la maua
Utaratibu wa kuweka mashada ukiendelea kwa kuzingatia makundi ya watu mbalimbali

Mama Victar akiweka shada maua
 Mama Basheleka ambaye ndiye mama mkwe wa Mchungaji Egebart Mwesiga Kanyambo akiwa tayari kuweka shada la maua
Eneo la kaburini wanafamilia wakishiriki kuweka mishumaa
Ndugu,jamaa na marafiki wa familia wakiendelea na utaratibu wa kuweka maua kwenye kaburi
 Baadhi ya wadau wakiwasili kijijini Kagoma kwa ajili ya kushiriki shughuli ya Mazishi ya Mchungaji Egbert Mwesigwa Kanyambo

 Eneo la maegesho
Mungu aipokee roho ya mchungaji ailaze mahala pema prponi
Muonekano wa nyumba ya Milele ya Mch.Egbert Kanyambo
Ni simanzi kubwa kwa watoto wa marehemu
Bwana Emiry Baruti akitoa mono wa pole kwa wafiwa
Waombolezaji wakiendelea kutoa mkono wa pole kwa wafiwa

Muendelezo wa matukio ya picha Ibada ya maziko ya mchungaji Egbert Kanyambo
 Majirani kutoka Vijiji jirani
Mr Nice pichani akiwa katika harakati za kuwafariji wafiwa
Bwana Salim Sadru akitoa mkono wa pole kuwafariji wafiwa.
Bi Party Visram akiwafariji watoto wa marehemu
Muendelezo wa matukio ya picha Ibada ya maziko ya mchungaji Egbert Kanyambo
Taswira mara baada ya shughuli ya maziko hayo kukamilika
BUKOBAWADAU MEDIA tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote dunia waweza kuwasiliana nasi kupitia namba +255 784 505045?0754 505043
Mwisho BUKOBAWADAU Tunatoa pole kwa familia,ndugu jamaa na marafiki Mungu awepe Subra!
Next Post Previous Post
Bukobawadau