Bukobawadau

RAIS MAGUFULI NA MH.RAIS MUSEVENI WAZINDUA KITUO CHA PAMOJA CHA HUDUMA ZA MPAKANI

 Rais Dkt John Magufuli amewataka maafisa wa vituo vya huduma za pamoja za forodha kujiepusha na vitendo vya rushwa na kufanya kazi kwa bidii ili kupunguza urasimu ambao umekuwa kikwazo kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria kutoka nchi moja kwenda nyingine.
Rais Magufuli ameyasema hayo alipokuwa akizindua kituo cha huduma za pamoja za forodha cha Mutukula kilichopo wilayani Missenyi mkoani Kagera pamoja na Rais Yoweri Museveni wa Uganda ambaye ametaka maafisa wa forodha kutotumia mwanya wa mipaka kuvuruga mahusiano ya jamii baina ya nchi hizo.
Rais Museveni amepongeza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na kutaka mipaka isiharibu mahusiano ya kijamii na ya kihistoria baina ya wananchi wa pande mbili hizo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mwenyeji wake Rais wa Uganda Yoweri Museveni wakati wa nyimbo za mataifa ya Tanzania na Uganda zikipigwa katika eneo la Uganda.
  Rais Dkt John Magufuli akikagua gwaride rasmi mara tu baada ya kupokelewa na mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kukagua gwaride Rasmi
SALAMU ZA KAMISHNA MKUU WA MAMLAKA YA MAPATO TANZANIA BW. CHARLES KICHERE KATIKA UZINDUZI WA KITUO CHA HUDUMA KWA PAMOJA (OSBP) MUTUKULA
------------------------------------------------------------------------------
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Uganda Yoweri Kaguta Museveni na Mama Janeth Museveni
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli na Mama Janeth Magufuli
Waheshimiwa Mawaziri wa Serikali ya Uganda na Tanzania mliopo hapa
Mheshimiwa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Dkt. Liberat Mfumukeko
Waheshimiwa Makatibu Wakuu wa Serikali ya Uganda na Tanzania mliopo hapa
Afisa Mtendaji Mkuu wa TradeMark East Africa Bw. Frank Matsaert
Mkurugenzi Mkazi wa TradeMark Tanzania Bw. John Ulanga
Mwakilishi wa Shirika la Misaada la UKaid
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Uganda Mama Doris Akol
Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja General Mstaafu Salim Kijuu
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Misenyi
Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Kyotera-Uganda
Viongozi mbalimbali wa serikali na taasisi za serikali na binafsi kutoka Uganda na Tanzania
Ndugu wafanyabiashara na wadau mliopo hapa
Waandishi wa habari
Ndugu Wananchi
Mabibi na Mabwana
Habari za mchana,
Waheshimiwa Marais,
Awali ya yote napenda kusema kwamba tumefarijika sana kwa ujio wenu katika kituo hiki cha huduma kwa pamoja mpakani Mutukula Tanzania. Karibuni sana
Kwa namna ya kipekee ningependa kuwashukuru waheshimiwa Marais wa Uganda na Tanzania kwa ujio wenu katika kufanikisha tukio hili la uzinduzi rasmi wa kituo chetu cha huduma kwa pamoja mpakani hapa Mutukula. Kituo hiki ni kielelezo dhahiri cha dhana nzima ya kuimarisha Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa vitendo kwa kuongeza ushirikiano na kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na abiria baina ya nchi zetu.

Waheshimiwa Marais,
Naomba nichukue fursa hii kutoa maelezo mafupi kuhusu kituo hiki.
Ujenzi wa kituo hiki ulianza rasmi mnamo tarehe 13.07.2011 na kukamilika tarehe 12.07.2015 na kuanza kutumika rasmi mwezi Agosti 2015. Mradi huu umetekelezwa na mkandarasi Lukolo Co. Ltd na mhandisi mshauri SAI Consulting Engineers kwa gharama ya kiasi cha Shilingi za Kitanzania 7,125,832,856.51 ambazo zilitokana na ufadhili wa UKaid kupitia Trade Mark East Africa (TMEA).
Waheshimiwa Marais,
Ujenzi wa kituo hiki ulihusisha vitu vifuatavyo
• Jengo kuu lenye ofisi mbalimbali kwa ajili ya kutolea huduma za forodha, uhamiaji na taasisi zingine za serikali za Uganda na Tanzania.
• Maegesho ya magari kwa ajili ya ukaguzi wa mizigo, magari ya abiria na magari binafsi.
• Vifaa vya TEHAMA,
• Samani
• Vifaa vya ukaguzi kama vile scanner na
• Huduma za maji, umeme na simu
Waheshimiwa Marais,
Uwepo wa kituo hiki umeleta faida kadhaa ambazo tayari zimeonekana, naomba nizitaje baadhi ya faida hizo kama ifuatavyo
• Kurahisisha usimamizi wa pamoja kwa taasisi zote zinazotoa huduma mpakani kwa nchi zote mbili.
• Kupunguza muda wa utoaji wa huduma kwa kuwa mizigo na abiria wanaotoka nchini Uganda husimama mara moja tu kwa ajili ya kukaguliwa na taasisi zote za serikali zilizopo katika eneo hili la upande wa Tanzania tofauti na awali ambapo walipaswa kusimama upande wa Uganda kwa ukaguzi na kisha kuja upande wa Tanzania kukaguliwa tena kabla ya kuruhusiwa
• Kurahisisha ubadilishanaji wa taarifa za ukwepaji kodi na uhalifu kwa haraka baina ya taasisi za mpakani za nchi zote mbili kwa kuwa wanafanyakazi mahali pamoja.
• Kituo kimehamasisha ufanyaji wa biashara kwa kuweka huduma muhimu kama vile huduma za kibenki kwa ajili ya malipo mbalimbali.
• Kituo kimeboresha mazingira ya kufanyia kazi kwa watumishi wa mpakani ukilinganisha na kituo kidogo na duni hapo awali.
• Kituo kimerahisisha udhibiti wa kiusalama kwa kutenga eneo maalumu la ukaguzi wa mizigo na mabasi ya abiria.
Waheshimiwa Marais,
Katika kuimarisha huduma za kituo hiki tupo mbioni kuanza kutoa huduma saa 24 kwa siku saba za wiki ili kuboresha huduma na kuongeza mapato.
Waheshimiwa marais
Napenda kutoa shukrani zangu kwa TradeMark East Africa ambao wamekubali kufadhili ujenzi wa nyumba za watumishi.
Waheshimiwa Marais,
Napenda niwashukuru tena kwa ujio wenu kuja kutuzindulia rasmi kituo chetu na tunaahidi kukisimamia kwa manufaa ya nchi zetu na wananchi wetu.
Asanteni kwa kunisikiliza.
  "Wataalam wa Tanzania na Uganda mkae pamoja mjadiliane ili mradi huu umalizike mapema"- Rais amesema Rais Magufuli
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu wakati akimkaribisha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kuwahutubia wananchi waliohudhuria shughuli hiyo

Mhe.Mama Janeth Museveni akiwapungia watu mkono wakati wa utambulisho
 Taswira mbalimbali eneo la tukio

 Mamia ya wakazi waMutukula na maeneo ya jirani wakisikiliza kwa makini hotuba ya Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli





 Mhe.Rais Museveni amepongeza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili na kutaka mipaka isiharibu mahusiano ya kijamii na ya kihistoria baina ya wananchi wa pande mbili hizo.

 Kiundi cha Imuka kiliweza kupata fursa ya kutumbuiza katika shughuli hiyo ya Uzinduzi wa kituo cha pamoja cha huduma za mpakani
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda, Mh. Yoweri Kaguta Museveni wakisaliana na viongozi mbalimbali

 Wakisalimiana na wananchi na Viongozi wa Chama
 Mhe. Rais Museveni aliyeongozana na Mkewe Mhe.Mama Janeth Museveni pichani akisalimiana na Mhe. Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dkt Kamala
 Sehemu ya umati ukifatilia yanayojiri

#bukokawadauNov9.
Next Post Previous Post
Bukobawadau