Bukobawadau

VIDEO:ZIARA YA GHAFLA YA BALOZI DR.KAMALA KATIKA KITUO CHA AFYA CHA KABYAILE - ISHOZI

 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr.Kamala akifanya mawasiliano  mara baada ya kufika ghafla katika kituo cha Afya cha Kanyaile na kushuhudia hakuna mtu wa kutoa huduma huku ikisemekana waudumu tayari wameenda kupumzika na wengine hawapo eneo la kazi.
Pamoja na mambo mengine Balozi Dr. Kamala amebaini kituo hicho kinakabiliana na changamoto ya Upungufu wa Vitendea kazi na kutokuwepo na Umeme kwa kipindi zaidi ya mwezi mmoja hivyo hamemtaka mkurugenzi wa halmashauri ya Wilaya Missenyi kuhakikisha anashughulikia swala hilo mara moja.
 Muonekano wa Mazingira na Majengo ya Kituo cha Afya Kabyaile Ishozi Wilayani Missenyi.
 Balozi Dr. Kamala pamoja na Mwenyekiti wa Kijiji Kabyaile wakipatiwa maelezo kutoka kwa mtaalam wa Maabara wa kituo cha Afya cha Kabyaile Emanuel Abuoro.aakizungumza na Viongozi wa Kijiji pamoja na mmoja
Mfereji wa maji yatokayo katika kituo hicho cha Afya ikielekea kwenye maeneo ya wakazi ya watu
 Barabara kuelekea kituo cha Afya Kabyaile ikiendelea kuharibika Vibaya kutokana na kutokuwa na mitaro iliyojengwa kwa ufanisi 
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akiendelea kukagua eneo la barabara lilivyoharibika
 TAZAMA VIDEO HAPA CHINI ALICHOKISEMA BALOZI DR.KAMALA KWENYE ZIARA YA KUSHTUKIZA KATIKA KITIO CHA AFYA KABYAILE DEC 9,2017
BUKOBAWADAU DEC 10,2017
Next Post Previous Post
Bukobawadau