Bukobawadau

KATIKA IFTAR ILIYOANDALIWA NA NDG. JUSTICE MASHEKHE WASISITIZA UMOJA NA MSHIKAMANO

 Ndugu Justuce Rugaibula amefuturisha wadau mbalimbali wa Mji wa Bukoba,marafiki wa familia waliojumuika na watoto wa kituo cha NusuruYatima katika makazi yake yaliyopo maeneo ya Ibura Manispaa Bukoba.#Ramadhan2018
 Futari hii ni maalum kwa ajili ya watoto wanaolelewa katika kituo cha Nusuru Yatima kilichopo Kashai ambapo 'Ma Grace' na mwanae Justice wamekuwa walezi wa kituo hicho kwa miongo kadhaa sasa.
 Wadau mbalimbali wakipata huduma safi ya futari
 Ndugu Abdulrahim Kabyemela na Bwana Kandanda Bwanika wakiwa makini kuhakikisha watoto waliopewa kipaumbele katika iftar wanapata kile kinachostahili
 'Zamani kulikuwa na utamaduni wa watu kufuturu nje ya nyumba zao ili wapita njia au majirani wakikuta wanafuturu nao wanajumuika, "Siku hizi tumeanza kufuturia ndani kila mtu na familia yake, basi siku moja moja kama hivi inatokea tunaamua kuukumbuka utamaduni wetu na kualikana kufuturu pamoja"Shukrani zimwendee mwandaaji wa hafla ya futari ya leo Ndugu Justice Rugaibula
 Hafla ya Iftari ikiendelea nyumbani kwa Justice Rugaibula #ramadhan2018
Waalikwa upande wa kinamama wakiendelea kupata fuatari
 Muendelezo wa matukio ya picha.
 Mgeni rasmi katikashughuli hii ni Sheikh wa Wilaya ya Bukoba Mjini Sheikh Kakwekwe.
 Muendelezo wa matukio ya picha 
 Waalikwa mbalimbali wakiendelea kupata futari
 Ikumbukwe mwaka Jana 'Ma Grace' ambaye ni Mama mzazi wa Justice alitembelea kituo hicho kwa lengo la kutoa mwaliko wa kusherekea sikukuu ya Idd na watoto yatima wa kituoni hapo,ndipo alipoguswa zaidi na hali ya mazingira na ikamladhimu kutoa msaada wa vitu mbalimbali ata kabla ya siku hiyo ,ambapo aliweza kukabidhi magodoro, nguo za watoto na mashuka na kuahidi kumsomesha binti mmoja wa kituoni hapo aliyechaguliwa kujiunga Kidato cha 5.huu ni mwendelezo wa kuendelea kuwajari watoto wanaoishi kwenye mazingira magumu
 Bwana Nkwama akitolea jambo ufafanuzi kwa rafiki yake Ndugu Afidhu Nkurukumbi Karugira.
 Sheikh Kakweke sheikh wa Wilaya ya Bukoba Mjini pichani kushoto mara baada ya futari hiyo iliyohudhuriwa na wadau mbaluimbali wa Mji wa Bukoba.
 Miongoni mwa waalikwa ni pamoja na Mzee Kabaka na Mr Taimuri pichani kushoto
 Mr. Kandanda Bwanika na Bi Grace pichani.
 Wadau wakiendelea kubadilishana mawazo.
 Katikati ni Alhaji Hashim Kamugunda mwenyekiti Mkoa Kagera na makamu mwenyekiti  Taifa waislamu madhehebu ya imam Shafi (R.A) akiwa ameungana na wadau wengine katika iftar iliyoandaliwa na Ndugu Justice Rugaibula
 Bwana Joha Rugenge akiwa ametulia mara baada ya kupata futari
Watoto hao wakielekea ndani kwa ajili ya kushiriki Dua maalum.
 Anaonekana Bwana Bashiru Kabyemela mwenyekiti wa kituo cha watoto wa Nusuru Yatima kilichopo kashai
 Ustaadhi akiongeza Dua mara baada ya futari
Ikumbukwe mwaka Jana 'Ma Grace' ambaye ni Mama mzazi wa Justice alitembelea kituo hicho kwa lengo la kutoa mwaliko wa kusherekea sikukuu ya Idd na watoto yatima wa kituoni hapo,ndipo alipoguswa zaidi na hali ya mazingira na ikamladhimu kutoa msaada wa vitu mbalimbali ata kabla ya siku hiyo ,ambapo aliweza kukabidhi magodoro, nguo za watoto na mashuka na kuahidi kumsomesha binti mmoja wa kituoni hapo aliyechaguliwa kujiunga Kidato cha 5.
 Dua ya kuiombea familia ya Bi Grace na Mwanae Justice ikiongozwa na wanafunzi wa kituo cha Nusuru Yatima,Inshallah mwenyezi mungu awazidishie heri
 Waumin wa Kiislamu wakiswali swala ya Magharibu muda mchache kabla ya futuru
#Ramadhan2018
#Bukobawadu tunatoa Wito kwa watu wenye uwezo wa kifedha kujenga tabia ya kuwasaidia watu wenye uhitaji ili kuwapunguzia ukali wa maisha.
God bless you Justice Rugaibula and your family 'Omkama Abangole'!! #Ramadhan2018

Next Post Previous Post
Bukobawadau