Bukobawadau

UMATI WAMZIKA MLANGIRA PAULIN RWEZAURA

Matukio ya picha yaliyojiri katika shughuli ya mazishi ya Omlangira Paulin Rwezaura yaliyofanyika Nyumbani kwake Kijijini #Kizigo #Kamachumu Juma lililopita na kuhudhuriwa na umati wa waombolezaji
 Pichani ni watoto watano wa kuzaliwa na mpendwa wetu Omlangira Paulin Rwezaura na Mama yao Bi Yustina wa pili kutoka kushoto pichani.
 Ibada ya mazishi hayo ikiongozwa na Fr. Faustin Baba paroko wa parokia ya Rutabo Kamachumu
Muonekano wa Jeneza lenye mwili wa Mzee wetu Omlangira Paulin Rwezaura
 Mr Catres akibadilishana Mawazo na Mama Kiroyera.
Marehemu Paulin Rwezaura pichani enzi za uhai wake.Marehemu Mzee Paulin Rwezaura na mtoto wa Omlangira Paskale Rutaihwa na Bi Angelina Kokugonza ambao ni marehemu, alizaliwa katika Kijiji cha Kizigo Bushagara-Kamachumu mwaka 1943 na ni mtoto wa kwanza na kifunga mimba katika uzao wa wazazi wake
 Maisha ya marehemu Mzee Paulin Rwezaura,alifunga ndoa takatifu tarehe 28/1/1978 na mke wake Bi Yustina,marehemu alisoma shule ya Rutabo zamani ikiitwa Rutabo Primary School  darasa la kwanza mpaka la nne na kuendelea na middle School shuleni hapo darasa la tano na la nane alipo maliza masomo yake na kufauru vizuri masomo yake zamani yakijulikana kama ''Standard Eight Teritorial Examination''
 Wawakilishi wa MSD kutoka Jijini Dar es Salaam wakiwasili msibani hapo kwa ajili ya kushiriki mazishi ya Baba Mzee wa mfanyakazi mwenzao Mzee Paulin Rwezaura
 Waombolezaji wakiendelea kuwafariji wafiwa.
 Wasifu wa marehemu Mzee Paulin Rwezaura unaonyesha baada ya masomo yake alijiunga na Jeshi la Polisi na aliweza kujiendeleza zaidi kwa kusoma sheria na kupelekea kupanda cheo na kuwa ''Inspector'' na kuamishiwa Idara ya uhamiaji.
 Waombolezaji wakiendelea kuwafiriji wafiwa


 Matukio ya taratibu za kimila kutoka kwa wajukuu wa mpendwa wetu Mzee Paulin Rwezaura
 Mjukuu wa Marehemu Mzee Paulin Rwezaura.
 Bwana Gama Mkurugenzi wa Kampuni ya Vinywaji ya 'Mali Juice'
 Mzee Mchuruza pichani kulia akisalimiana na mmoja wa waombolezaji
 Muendelezo wa matukio ya picha msibani hapo

 Padre Erick Shumbusho wa parokia ya Kishongo akisaidiana na Paroko wa Rutabo kuongoza Ibada ya mazishi ya mpendwa mzee wetu Omlangira Paulin Rwezaura

 Taswira wakati Ibada ya mazishi ikiendelea
 Sehemu ya wanakwaya wakiendelea kushiriki Ibada ya mazishi hayo yaliyofanyika Juma lililopita nyumbani kwa marehemu mzee Paulin Kijijini Kamachumu

 Bi Gode pichani mmoja wa wanafamilia


 Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiendelea
 Kwa majonzi makubwa anaonekana mjane wa Marehemu wakati wa kutoa heshima za mwisho. 
 Zoezi la kutoa heshima za mwisho kwa mpendwa wetu likiendelea
 Machozi yahuzini yakiwatoka wanafamilia wote.
 Waliosimama ni 'waka mwana' wanao olewa katika familia hii ya marehemu mzee Paulim Rwezaura.
 Msemaji wa familia akitoa neno la shukrani

Eneo la kaburi wakati shughuli ya mazishi yakiendelea
 Watoto wa kiume wa marehemu mzee Paulin Rwezaura wakiweka shada la maua
  Mama Mjane wa marehemu Mzee Paulin Rwezaura Bi Yustina wakati akiweka shada la maua.
SEHEMU YA MATUKIO YA AWALI KABLA YA IBADA YA MAZISHI
 Katika picha ya pamoja kwa ajili ya kumbukumbu
 Mkono wa kuwafariji wafiwa
 Mama mjane na mwanae wakiwa na huzuni mkubwa.


 Matukio ya hapa na pale kabla ya shughuli ya Ibada
MWISHO #Bukobawadau tunatoa pole kwa wafiwa wote! BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE!!!!
Next Post Previous Post
Bukobawadau