Bukobawadau

HAJJAT ZAHARA DATTANI APOKEA ZAWADI ZA PONGEZI KUTOKA KWA NDUGU NA MARAFIKI..!

Hajjat Zahara Dattani pichani akiomba Dua kwa Allah muda mchache kabla ya kuanza kwa hafla fupi ya kupokea zawadi kutoka kwa ndugu , jamaa ,marafiki ,majirani na vikundi mbalimbali ikiwa ni katika kumpongeza kwa kukamilisha Ibada tukufu ya hijja  na kurejea salama  nyumbani kwao Kijijini Katoro Bukoba.
Mara baada ya kuwasili kutoka Makkah katika ibada ya Hijja,Hajjat Zahara Dattani alipokelewa na umati wa watu na msafara wa mapokezi ulielekea nyumbani kwao Kijijini #Katoro nakufatiwa na Dua maalum,yafuatayo ni matukio ya picha yaliyojiri siku ya pili katika hafla ya kukabidhiwa zawadi kutoka kwa watu mbalimbali
Tazama mwanzo mwisho matukio ya picha yaliyojiri katika hafla ya kukabidhiwa Zawadi #HajjatZaharaDattani.
Sehemu ya wageni wakifuatilia kinachojiri
Hajjat Zahara katika  picha ya pamoja na Mama Abdulkadiri Kajumlo. 
Hajjat Zahara na Hajjat Hindu katika picha ya pamoja
 Katika picha ya pamoja kutoka kushoto ni Bi Najath Abdallah,Hajjat Zahara Abdallah (Mrs Dattani),Bi Nura Abdallah,Hajjat Hindu,Bwana Jafari na Hajjat Johari
 Ndugu wa familia pichani kutoka kushoto ni Bi Najath Abdallah,Hajjat Zahara Abdallah (Mrs Dattani),Bi Nura Abdallah,Hajjat Hindu,Bwana Jafari na Hajjat Johari
 Bi Najath,Hajjat Zahara na Bi Nura katika picha maalum kwa ajili ya kumbukumbu
Dua mara baada ya kupokea zawadi kutoka kwa wajukuu wa familia hiyo
Wanafamilia katika picha maalum kwa ajili ya kumbukumbu
Hajjat Zahara akiangalia zawadi ya mbuzi na mmoja wa marafiki wa familia kama pongezi baada ya kukamilisha nguzo ya tano ya Kiislam huko makka nchini Saudi Arabia
Furaha na shangwe vikiendelea kutawala

 Ndugu wa familia wakifurahia jambo
Muendelezo wa matukio ya picha yaliyojiri katika hafla ya kukabidhiwa Zawadi #HajjatZaharaDattani.
 Wadau wakipata Dua kutoka kwa hujaji mwingine mkazi wa Katoro pichani katikati
 Hajjat Zahara Dattani (Mama Sonia) pichani
Zawadi mbalimbali zikiendelea katika hafla fupi yakumpongeza baada ya kurejea salama kutoka katika ardhi tukufu ya Makka.
 Ng'ombe wa shughuli akiwa tayari kuchinjwa.
 Maandalizi ya msosi siku ya pili ya hafla ya pongezi na kupokea zawadi kwa Hajjat Zahara Dattani
Mbuzi wakiwa tayari kuchinjwa kwa ajili ya shughuli ya Dua iliyofanyika siku iliyofuata, majuzi Ijumaa ya tarehe 20/9/2018
 Bwana Seif pichani akifuatilia kinachoendelea


 Shughuli ni watu ,kinachoendelea ni wanamama kuchambua mchele


 Bi Najath Abdalla mdogo wake Hajjat Zahara Dattani akiwa katika hekaheka za hapa na pale.
 Hajjat Hindu ambaye ni Dada yake Hajjat Zahara akifurahia jambo
 Wageni wakiendelea kuwasili kwa ajili ya kumpongeza Hajjat Zahara
Wageni wakiendelea kuwasili kwa ajili ya kukabidhi zawadi zao.


Muendelezo wa matukio ya picha, ndugu na marafiki wa familia ya hajjat Zahara Dattani wakiendelea kuwasili nyumbani kwake na kutoa zawadi zao za pongezi
Hajjat Zahara akiendelea kusalimiana na wageni waliofika kwa ajili ya kumpongeza.
 Pongezi za hapa na pale  sambamba na zawadi zikiendelea kumiminika kwa Hajjat Zahara
Kijana wa bodaboda akiwasili mahala hapo.
 Hongera sana Hajjat Zahara kwa kukamilisha ibada tukufu ya Hijja!!
 Katika picha ya pamoja na Mama Abdulkadiri Kajumlo 
 Muendelezo wa matukio ya picha
 Bwana Omary Juma pichani kushoto mkwe wa familia hii akifanya mawasiliano
 Mzee Issa Bukana pichani katikati akikabidhi zawadi ya mbuzi
Mzee Issa Bukana (kulia) katika picha ya pamoja na Hajjat Zahara Dattani mara baada ya kukabidhi zawadi zake


 Kutokana na mifumo ya hali ya hewa, mvua kuelekea msimu wa vuli tayari zimeanza mkoa wa Kagera ambapo watu wameanza kupanda mazao kama unavyojionea pichani
 Picha kutoka Kijijini Katoro-Bukoba mvua kuelekea msimu wa vuli tayari zimeanza na watu wameanza kupanda mazao yao.
Taswira s eneo la tukio ilipofanyika shughuli ya Dua maalum ya kumpongeza Hajjat Zahara Dattani,shughuli iliyofanyika majuzi alhamisi tarehe 20/9/2018.

Next Post Previous Post
Bukobawadau