Bukobawadau

HALFA YA FUNGA MWAKA YA 'RUZINGA DAY' YAFANA - MGENI RASMI BALOZI DR KAMALA...!

Hafla ya funga mwaka ya Ruzinga Day yafana sana,Mgeni Rasmi katika hafla ya funga ya mwaka ya wadau wa maendeleo wa kata ya hiyo,Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akizungumza na Wajumbe wa kamati tendaji Ruzinga Day pamoja na Viongozi wa kata hiyo mara baada ya kukagua Chanzo cha mradi wa Maji.
 Kwa kipindi cha  Miaka kumi na tatu(13) Kata ya Ruzinga imekua ikiandaa tamasha kubwa la 'Ruzinga Day likiambatana na sherehe za kuaga nakukaribisha mwaka mpya,Tamasha lenye lengo la kuwakutanisha kwa pamoja wananchi wote wa Kata Ruzinga,marafiki na wadau wanaishi ndani na nje ya kata hiyo kwa nia ya kuhamasisha  na kuchangia  miradi mbalimbali ya maendeleo katika Elimu,Afya na huduma za Jamii
 Mwenyekiti wa RD  Bi Elizabeth Rugenga katika picha na Mh.Diwanai wa kata ya Ruzinga 
 Jumla ya Vitanda 22 vieweza kununuliwa kwa nguvu ya Wajumbe wa Kamati tendaji ya Ruzanga Day na wananchi wa kata ya Ruzinga
 Katika kuunga mkono mkakati wa Serikali pamoja na Juhudi za Mbunge wao Balozi Dr. Kamala za kuboresha Elimu,Wakazi wa kata ya Ruzinga wamekuwa wakichangia maendeleo ya kata hususani katika nyanja ya Elimu kupitia kauli mbiu yao inayosema;'Punguza Michango ya Harusi na starehe changia maendeleo ya kata Ruzinga' pichani anaonekana Mwenyekiti mstaafu wa Ruzinga Day Ndugu Aspon Mwijage akikagua mazingira ya Bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Ruzinga
Wajumbe wa kamati tendaji ya'Ruzinga Day' katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala
Mbele ya Jengo Jipya la  Bweni la wasichana katika shule ya Sekondari Ruzinga pichani katikati ni Mwenyekiti wa RD  Bi Elizabeth Rugenga.
Baadhi yawananchi wakichota maji katika chanzo cha maji cha 'Akaina' kilichopo ndani ya kata ya Ruzinga
 Baadhi ya wanafunzi wa darasa la saba waliopata alama  A na B katika shule za kata ya Ruzinga ameeza kukabidhiwa zawadi ya pesa taslimu Tsh 50,000 wenye alama A na shilingo 30,000 kwa wenye alama B ikiwa ni mkakati wa RD wa kuongeza ufaulu mashuleni
Mmoja wa wazazi akipokea zawadi ya pesa taslimu kwa niaba ya mwanae.
Balozi Dr. Diodorus Buberwa akimkabidhi tuzo mwalimu mkuu wa shule ya msingi Ruzinga
Mwenyekiti mstaafu wa Ruzinga Day Ndugu Aspon Mwijage mara baada ya kukabidhiwa tuzo ya shukrani kwa kutambua mchango wake katika maendeleo ya wanaruzinga.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akikabidhia tuzo ya heshima na kamati tendaji ya Ruzinga Day.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akitunukiwa tuzo ya heshima kwa kushiriki ,kuhamasisha na kuchangia kwa dhati maendeleo ya Wanaruzinga.
Mwenyekiti wa RD  Bi Elizabeth Rugenga fimbo mkononi mara baada ya kukabidhiwa fimbo na Mwenyekiti mstaafu wa Ruzinga Day Ndugu Aspon Mwijage,fimbo hiyo ni  ishara na heshima ya uongozi kwa desturi jamii zetu.
Meza kuu wakibadilishana mawazo katika hafla ya Ruzinga Day inayofanyika kila mwaka ifikapo tarehe 31 disemba, pichani kushoto ni Dr Frank Ludigo.
Ndugu Kato Kamala mdau wa maendeleo ya Ruzinga akichangia kupitia mnada wa mazao.
Tamasha la Ruzinga Day ni pamoja na ligi ya mpira wa miguu iliyoandaliwa na kamati tendaji ya RD  na timu ya Bwanja Fc iliibuka mshindi na kukabidhiwa zawadi ya Ng'ombe na kila mwaka utaratibu wa zawadi ya ng'ombe mmoja utoka kwa Mbunge Balozi Dr.Kamala
 Ni wasaa wa burudani ya mpira wa miguu
 Wadau wakifuatilia soka tamasha la Ruzinga Day
 Wadau wakifuatilia soka tamasha la Ruzinga Day
 Timu  zote mbili zikiwa tayari kusalimiana na Mgeni Rasmi
 Mgeni Rasmi Mbunge Mbunge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akisalimiana na muamuzi wa mchezo wa fainali za rRuzinga Day.
 Mgeni Rasmi Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akikagua timu mbili zilizoshiriki fainali ya Ruzinga Day
 Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr. Diodorus Buberwa Kamala akifurahia jambo
 Mtangazaji Shaidu Chagulani akiwajibika

 Taswira  mbalimbali uwanjani
 Mshindi amepatikani kwa mikwaju ya penati.
 Wadau mbele ya Camera yetu

 Shangwe za mashabiki wa Bwanja Fc mara baada ya timu yao kuibuka na ushindi
 Usiku wa tamasha la Ruzinga Day mambo yakiendelea kuchukua kasi
 Muendelezo wa matukio ya picha
 Taswira mbalimbali eneo la tukio
 Zoezi linaloendelea ni Michango ya maendeleo ya Ruzinga
Utaratibu wa kuchangia maendeleo ya Ruzinga ukiendelea, pichani kushoto ni Adv. Kamala na Mr Kato Kamala
Kakau Band wakitumbuiza jukwaani.

Next Post Previous Post
Bukobawadau