Bukobawadau

MUSHEMBA TRINITY SCHOOL – Nyota inayong’ara Tanzania.

Mushemba Trinity school ni shule ya kutwa na bweni inayomilikiwa na Mushemba Foundation iliyoanzishwa  takribani miaka 8 na mwanzilishi wake Bw. Josephat Mushemba  ambaye  pia ndiye mkurugenzi  mkuu wa  shule hii.
 Bw. Josephat Mushemba pichani Mkurugenzi wa Shule ya Mushemba Trinity iliyopo Manispaa ya Bukoba akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo katika hafla ya kuwapongeza wanafunzi wa darasa la nne wa shule hiyo waliofaulu vizuri kwa mwaka 2018 wengi wao wakiwa na daraja ”A” na kuipa shule hiyo nafasi ya pili kiwilaya.
 Mwaka  juzi baada ya matokeo ya mtihani wa  kitaifa  ya  darasa la nne kutoka , nilipata nafasi ya kutembelea  shule na kuandika  makala  inayosema    Mushemba   Trinity” tunda linalochipuka  na hapo ilikuwa   imechukua  nafasi  ya 3/13 kiwilaya na 5/350 kimkoa na 13/5875 kitaifa, hapo ilikuwa mwaka 2016.
Baadae  mwaka 2017 , nilikuwa katika kazi zangu , nikasikia  kuwa  shule  imefanya vizuri kwa mara ya pili na kuwa  ya 1/11 kiwilaya , 5/255 kimkoa na 13/5123, Na kwa  ushindi huu shule ilikuwa ikishindana na shule nyingine  ambazo ziko katika kundi la watoto wasiozidi 40 darasani, ambapo kiukweli shule  za idadi hii sio nyingi mno.

Mwaka 2018 shule hii ilikuwa kwenye kundi la shule ambazo zina watoto  zaidi ya 40 darasani  ambapo shule zenye idadi hii ni nyingi, hapo tena hamu yangu ilikuwa  kubwa zaidi kujua matokeo yatakuwaje.
Punde matokeo yalipotoka  ya mwaka 2018,nilikimbilia kwenye mtandao kuangalia matokeo   ambapo  kwa mara ya tatu shule ya Mushemba Trinity  
iliendelea kung’ara zaidi. Shule imekuwa ya 2/33 kiwilaya,  ya 15/791 kimkoa na  69/13182  kitaifa  ambapo shule  iliingia katika kundi la shule  bora kitaifa, kwa maana ya Tanzania nzima.
Tarehe 10/01/2019 , Mkurugenzi  wa shule Bw. Josephat  Mushemba , alifanya sherehe ya kuwapongeza  wanafunzi  ambao wengi wao walishinda kwa  daraja ”A” nami nilipata nafasi ya kuhudhuria sherehe hiyo.
Shule imejificha kidogo prmbeni mwa barabara kuu kuelekea Maruku na imezungukwa na mazingira  yaliyopambwa  na kupandwa maua. 
Moja kati ya Jengo la Bweni la shule hiyo.
Shule ina majengo yenye viwango na mabweni ya wanafunzi  ya  kulala yako katika viwango vya hali ya juu. Shule  ina mabweni ya kike na kiume   watoto huwa wanakutana  pamoja jioni 
kwenye ”Study room” ambapo pia  sehemu hii imejengwa kwa ustadi . Kwakweli nimeona mabweni mengi lakini mabweni ya shule  ya Mushemba ni mojawapo ya mabweni yenye   viwango, kuna usafi wa hali ya juu ,shule hii hata ukimuacha mtoto  ili alale ,unakuwa na amani moyoni  kwamba mtoto umemuacha sehemu salama.. Watoto wana walezi wenye upendo  na wanaonekana wako makini   sana na kazi  yao.
MADARASA. 
Nilipata muda pia wa kutemebelea madarasa  yao ambayo kwa kweli ni mazuri kama mnavyoona hapo kwenye picha lakini cha msingi , ufundishaji  mahiri wa walimu  ambao wote wanaonekana  kuwapenda watoto , hii ni shule inayokazia 
walimu kuwa na wito, upendo kwa watoto  na kutokimbilia adhabu zinazowaathiri watoto kisaikolojia.
Baada ya hapo nilihudhuria sherehe  ya kuwapongeza watoto walioshinda,Kulikuwepo na nyimbo, watoto waliimba na kuonyesha vipawa vyao , maigizo  na chakula kizuri.
Baba  Askofu  Dk. Samson  Mushemba ambaye  ni mlezi wa shule hii, naye alihudhuria sherehe hii na aliwaasa watoto kusoma kwa bidii na kutanguliza  heshima na adabu kwa walimu wao.
Itakumbukwa kwamba , pamoja na shule  kufanya vizuri, shule hii inasaidia na kusomesha watoto   wanaotoka kwenye mazingira magumu , wengi wao wakiwa wamefiwa na wazazi  mmoja au wote wawili na wanafunzi wengine ni wale  wenye uwezo wa kulipa ada wenyewe. Asilimia 50 ya watoto  wanaosoma katika shule hii , ni wale wanaolipiwa ada na asilimia 50 ni wale wenye uwezo wa kulipa ada wenyewe.
 Maono ya shule hii , pamoja na kwamba  imeendelea kufanya vizuri, kiwilaya , kimkoa na kitaifa, ni kuendelea kuwasaidia watoto wanaotoka katika mazingira magumu   kwa njia hii pia   ni kuendelea katika kusaidia juhudi za  serikali ya mheshimiwa  Dr. John   Pombe  Magufuli katika  kuwawasidia wanyonge kuwapa elimu bora.
Nikiwa naelekea nyumbani  nilienda  natafakari  , hakika tunahitaji shule za namna hii nyingi zenye ubora lakini pamoja na ubora wa hali ya juu  bado shule ina nafasi  kwa watoto wanaotoka kwenye mazingira  magumu!  Kweli  kuna umuhimu wa shule nyingine kwenda kujifunza jambo hili katika shule ya Mushemba!   Kweli shule hii ni bora .
Baba askofu mstaafu Dr.Samson Mushemba akitoa neno katika hafla ya kuwapongeza Wanafunzi wa darassa la nne shule ya Mushemba Trinity school
Kwa maelezo zaidi  kuhusu shule hii na uwezekanao  wa kupata  nafasi ya mtoto wako.
piga simu  namba  0754 9060183 au 0788 819 725
Email. mushemba.found @gmail.com
 Muonekano wa mazingira na Majengo ya Shule hiyo
 Muonekano wa mazingira na Majengo ya Shule hiyo
Ndani ya Bweni ya Wasichana wa Mushemba Trinity school 
 Utaratibu wa kukabidhi zawadi kwa Wafanyakazi wa shule hiyo ukiendelea
 Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo,Mwl Johansen Jonadhan akipokea mkono wa pongezi na  zawadi kutoka kwa Mkurugenzi wa  Shule ya Mushemba Trinity Bw. Josephat  Mushemba kufuatia kazi nzuri wanayoifanya.
 Mkurugenzi wa  Shule ya Mushemba Trinity Bw.Josephat Mushemba akikabidhi zawadi kwa kwa Mwalimu Gilbert.
 Muendelezo wa mtukio ya picha wakati Mkurugenzi wa  Shule ya Mushemba Trinity Bw. Josephat  Mushemba akiwakabidhi zawadi Walimu wote wa Shule hiyo na wafanyakazi wote  wa Idara mbalimbali shuleni hapo kufuatia kazi kubwa na nzuri wanayoendelea kuifanya.
NOTE:Kwa maelezo zaidi  kuhusu shule hii na uwezekanao  wa kupata  nafasi ya mtoto wako.Wasiliana nao kupitia simu  namba  0754 9060183 au 0788 819 725
Email. mushemba.found @gmail.com

Next Post Previous Post
Bukobawadau