Bukobawadau

MBUNGE BALOZI DR KAMALA AMWEZESHA NA KUMPONGEZA BI SICOLASTIKA BAHATI MWENYE ULEMAVU WA NGOZI

 Mbunge wa Jingo la Nkenge Balozi Dr.Diodorus Buberwa Kamala apokea kilio na kumwezesha Mama mwenye Ulemavu wa Ngozi (Albino) pichani kushoto Bi Sicolastika Bahati Mkazi wa  Kijiji Nyakuanga Kata Minziro Wilayani Missenyi,Bi Sicolastika mwenye watoto watatu aliweza kulima shamba lake lenye ukubwa wa heka 3 na kwa na kwa sasa anakabiliwa na changamoto ya kupalilia shamba hilo na hii ni kutokana na kutotakiwa kukaa juani  muda mrefu hivyo amemwomba Mbunge amwezeshe ili aweze kumudu hatua ya kupalilia.
Balozi Dr. Kamala ameguswa na Mama huyo anayejituma na kumsaidia kiasi cha shilingi laki Moja (100,000) na kumtaka Diwani wa kata ya Minziro amuingize katika makundi maalumu ya watu wenye Ulemavu ili aweze kunufaika.
 Balozi Dr.Diodorus Buberwa Kamala katika picha ya pamoja na Bi Sicolastika Bahati 
Baadhi ya Wakazi wa Kata Minziro wakimsikiliza Mbunge wao Balozi Dr. Kamala
 Pia Mbunge wa Jimbo la Nkenge Balozi Dr.Diodorus Buberwa Kamala ametoa pongezi kwa Viongozi wa Kata Minziro namna wanavyo jitahidhi kutatua migogoro ya ardhi wao wenyewe
Baadhi yaViongoji wa Kata ya Minziro pichani wakipongezwa na Mbunge wao Balozi Dr. Kamala
 Mzee Mutasi Diwani ya Kata Minziro akiongea mbele ya wananchi walioweza kuhudhuria mkutano wa Mbunge Balozi Dr. Kamala
 Hoja mbalimbali zikiendelea kutolewa na wananchi
 Mkutano ukiwa unaendelea katika Viwanja vya Chama cha Ushirika 'Minziro Cooperative Society'
 Wananchi wakitoa hoja zao kwa Mbunge Balozi Dr.Diodorus Buberwa Kamala
Wananchi wakiendelea kumsikiliza Mbunge wao Balozi Dr.Diodorus Buberwa Kamala anaye endelea na ziara zake Jimboni kila kata na baadhi ya Vijiji.
Next Post Previous Post
Bukobawadau