Bukobawadau

BALOZI KAMALA KUANDAA MKUTANO MKUBWA UJULIKANAO KAMA 'MISSENYI INVESTMENT FORUM'

TAZAMA katika Video hapo juu Mkutano wa Mbunge wa Jimbo Nkenge Balozi Diodorus Buberwa Kamala alipokutana  na wananchi wa Kata ya Kasambya Bunazi Wilayani Missenyi na kusikiliza kero mbalimbali za wananchi hao,Katika mkutano huo Mbunge Balozi Dr. Kamala ameweza kutolea ufafanzi sheria mpya zilizopitishwa na Bunge kama muswada wa sheria ambao pamoja na mambo mengine unaondoa kodi ya zuio la asilimia tano inayotozwa kwenye bei ya kuuzia madini kwa wachimbaji wadogo na kurekebisha Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) kwa kutoa msamaha kwenye madini ya metali na vito yatakayouzwa katika masoko ya ndani ya nchi
Balozi Diodorus Buberwa Kamala amezitaja sheria zilizofanyiwa marekebisho ni Sheria ya Madini, ya Ushuru wa Bidhaa, Kodi ya Mapato, Mamlaka ya Serikali za Mitaa ya utozaji kodi ya majengo,na ya VAT.Amesema;Marekebisho hayo pia yanakusudia kuanzisha vituo vya ununuzi wa madini katika maeneo ambako masoko ya madini hayakuwepo, na kuweka utaratibu wa uingizaji madini nchini.
Pia katika Mkutano huo Mbunge Balozi Dr.Kamala ameongelea maandalizi ya Mkutano Mkubwa ujulikanao kama 'Missenyi Investment Forum' unaoandaliwa na Ofisi yake kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya pamoja na Halmashauri,Lengo kuu la mkutano huo ni kukuza na kubahinisha fursa za biashara katika sekta mbalimbali Wilayani Missenyi.
 Ndugu Kutone mdau wa maendeleo Missenyi akitoa hoja yake kwa Mbunge wa Jimbo la Nkenge


 Bwana Shahidu Chagulani pichani
 Mh.Twaha Diwani wa Kata Kasambya na Mh. Lidia Diwani viti maalum wakimsikiliza kwa makini katibu wa Mbunge wa Jimbo la Nkenge Ndugu Peter Mwafiwa.
 Katibu wa Mbunge wa Jimbo la Nkenge kwa tarafa ya Missenyi Ndugu Peter Mwafiwa 'Shegede' pichani akitolea jambo ufafanuzi katika mkutano huo uliofanyika Viwanja vya shule ya Msingi Kasambya.

 Baadhi ya wananchi wakifuatilia kinachojiri
Muendelezo wa matukio ya picha
Next Post Previous Post
Bukobawadau