Bukobawadau

KHERI NA BARAKA TELE OMULANGILA NESTOR MUZANILA KWA KUTIMIZA UMRI WA MIAKA 70 !!

 Omulangila  Nestory Norbert Muzanila (katikati ) katika picha ya pamoja na Mapadre walioongoza Misa takatifu ya kumshukuru Mungu katika kuadhimisha kumbukumbu ya miaka 70 ya kuzaliwa kwake iliyofanyika Nyumbani Kwake Ibalaizibu-Bukoba nakufuatiwa na hafla fupi ya kumpongeza.
Wanafamilia na Mapadre katika picha ya pamoja na Mama mzazi wa Omulangila Nestor ,Isabela Norbert Muzanila (Ma Kokurola) mwenye umri wa Miaka 94 

 #Bukobawadau tunapenda kuchukua nafasi hii kukutakia heri ya kuzaliwa,Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu ya furaha na yenye baraka
 Zawadi kwa Baba ikikabidhiwa na mwanae Rita Muzanila
 Katika picha ya pamoza Omulangira Nestory Muzanila ,mabinti zake na mmoja wa Wajukuu mara baada ya kumkabidhi zawadi yenye nembo na Ujumbe mzuri wa Shukrani
Historia fupi ya Omulangila Nestor Muzanila iliyosomwa na Mwanae Rita Muzanila pichani
Omulangila Mzee Nestor Muzanila alizaliwa tarehe 30/6/1949 hapa katika kijiji hiki cha Ibaraizibu Bukoba. Alisoma shule ya msingi ya Itahwa kwanzia darasa la kwanza hadi la nne mwaka 1957-1960. Baada ya hapo aliendelea na middle school katika shule ya Kiteyagwa mwaka 1961-1965. Kisha alijiunga na shule ya secondary ya Grewal Bukoba kwanzia mwaka 1966-1969. Baada ya hapo alianza kazi na kujiunga na chuo cha taifa cha ustawi wa Jamii na kupata diploma ya ustawi wa jamii mwaka 1976.
Omulangila Nestor Muzanila alihamua kuchagua taaluma ya ustawi wa jamii (social work) kutokana na malezi aliyokuwa amepewa na wazazi wake. Alizaliwa kwenye ukoo wa kitemi na Baba yake alikuwa mwalimu. Alishuhudia watu wengi katika jamii wakija kuomba misaada mbali mbali na ushauri kutoka kwa wazazi wake. Na Baba yake alimshirikisha. Hivyo basi, Mzee Nestor alijifunza na kupata moyo wa kusaidia watu pia. Alipokuwa shule alijiunga na Chama cha mascout ambako alijifunza mambo mbalimbali ya kuhudumia watu na jamii. Kadhalika alishiriki katika vyama mbali mbali vya kitume vya kikristo kama YCS na alichaguliwa kuwa Rais wa chama hicho katika jimbo la Bukoba. Chama hiki kiliunganisha wanafunzi katika shule mbali mbali za sekondari, na sayansikimu na shule za manesi. Kutokana na uzoefu wake, alichaguliwa kuwa kiranja mkuu alipokuwa sekondari.
 Akiwa mtumishi katika idara ya ustawi wa jamii, aliteuliwa kushika nyazifa mbali mbali. Kwa mfano, aliwahi kuteuliwa mara mbili kwa nyakati tofauti kuwa katibu mtendaji wa Baraza la taifa la huduma za ustawi wa jamii. Baraza ambalo lilikuwa na mashirika 44, chini yake yakiwemo idara/wizara za serikali na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali. Baraza ilo lilimpatia fursa ya kuhudhuria na au kushiriki katika makongamano na seminars katika nchi mbali mbali zikiwemo Kenya, Ghana, Nigeria, Zambia, Zimbabwe, na Ethiopia. Pia aliwahi kuteuliwa kuwa Afisa ustawi wa jamii wa mkoa katika mikoa ya Dodoma, Tanga, Arusha, Kilimanjaro, Iringa na Mara.

Kwa kutambua umuhimu wa kujiendeleza kielimu, Baba yetu /mzee wetu Omulangila Nestor Muzanila kujiunga na chuo kikuu cha Washington mwaka 1994 kilichopo katika jiji la St. Louis, jimbo la Missouri nchi Marekani. Na kwa kutambua Elimu na uzoefu wake wa kazi wa Muda mrefu, chuo hicho kilikubali maombi yake na kumpatia scholarship ya Mother Theresa wa Calcuta kwanzia mwaka 1996. Mwaka 1998, alipata Masters Degree ya Social Work. Baada ya masomo, alijiunga na shirika la hope well center ili kupata uzoefu zaidi wa kazi katika mazingira ya Marekani. Na baada ya hapo aliombwa na shirika ilo kuendelea kuwafanyia kazi. Hivyo, aliiomba serikali ya Tanzania kustaafu na kwa kuwa alikuwa amefikia umri wa kustaafu kwa Hiari, alikubaliwa. Aliendelea kufanya kazi Marekani mpaka alipofikia umri wa kustaafu kwa Sheria za kule.

 Omulangila Nestor Muzanila akimlisha kipande cha Keki Mama yake Mzazi  Isabela Norbert Muzanila (Ma Kokurola) mwenye umri wa Miaka 94.
Baada ya kustaafu huko Marekani, alihamua kurudi nyumbani. Na sasa anaishi hapa kijijini Ibaraizibu Bukoba akijishughulisha na shughuli za kilimo na ufugaji.
#Bukobawadau tunapenda kuchukua nafasi hii kukutakia heri ya kuzaliwa,Mwenyezi Mungu akupe maisha marefu ya furaha na yenye baraka


Pichani ni Mr & Mrs Gody Katemana

Muendelezo wa matukio ya picha wakati sherehe ikiendelea.



Kikunddi cha Kashai One kikishusha burudani 

Next Post Previous Post
Bukobawadau