Bukobawadau

NDG JOANFAITH KATARAIA AZINDUA KONGAMANO LA ARUSHA JIJI YA KIJANI

Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana Taifa ndg Joanfaith Kataraia leo amezindua Kongamano la Arusha jiji ya kijani lililofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC jijini humo
Akizungumza wakati wa Ufunguzi huo amewataka Vijana hao kuitumia kampeni hiyo vizuri kwa kuendelea kujengeana maarifa mbalimbali kwa kila mmoja kuitambua nafasi yake katika Chama na Jamii kwa Ujumla.
Amesema “Katika Kampeni hii tunapaswa kufahamu vijana ndio wenye dhamana ya kuendelea kusukuma gurudumu la maendeleo ya Taifa letu kwa Nguvu na Umoja hivyo ni muhimu kwa kila mtu kwa nafasi yake kuendelea kujiongezea maarifa kwa kadri ya uwezo wake ili kuwa Viongozi bora wenye mawazo na maarifa ya kuisaidia jamii inayo tuzunguka”
Pia Ndg Joanfaith ameendelea kuwasisitiza Vijana hao kuendelea kuwa na msimamo thabiti kwa imani ya Chama Cha Mapinduzi hasa katika kipindi hiki cha kuelekea katika Chaguzi mbalimbali za kiserikali kutumika kwa maslahi ya chama na si mtu binafsi.
Aidha amewataka Vijana hao kuendelea kuyasemea mazuri yote yanayo tekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli.
katika kongamano hilo amezindua Daftari maalum kwa ajili ya Uandikishwaji wa Wanachama pamoja na kuwapatia kanuni 500 na kadi za Umoja wa Vijana 500.
Next Post Previous Post
Bukobawadau