TAASISI YA TA'AWUNUL ISLAAM YAZINDULIWA RASMI KATORO-BUKOBA KATIKA BALAZA LA EID!
Hajjat Zahara Dattani Mwenyekiti wa taasisi ya Kiislam ya TA'AWUNUL ISLAAM akitangaza Viongozi waandamizi wa taasisi hiyo ambapo Makamu mwenyekiti ni Abdurazak Dattani katibu ni Sheikh Farid Issa Bakana, muweka hazina ni Bwana Hassan Datani na wajumbe wa taasisi ni pamoja na Al hajj Sheikh Hassim Kamugunda ,Sheikh Abutwahil Kassim na Bi Sonia Datan pamoja na mambo mengine Hajjat Zahara ametumia fursa hiyo kutoa shukrani kwa watu wote wanaotoa ushirikiano kwa namna moja ama nyingine na kwa umuhimu shukrani za kipekee zimwendee Mama Abdul ambaye ni Mama yake mdogo.
Ustaadh Maulana Farid alipopata fursa ya kutaja Uongozi wa Msikiti uliojengwa kwa Udhamini wa Mwenyekiti wa taasisi Hajjat Zahara Dattani ,Mwenyekiti wa Msikiti huo uliopo hapo Itoma Katoro ni Hajji Idrisa Katabazi, Katibu ni Bi Fatma Izam,Mlezi - Hajjat Joha Byabato Wajumbe ni Imam Karim Kataratasi,Mikidadi Mustafa na Bi Rukia Abdallah
Taswira kutoka Viwanja vya Masjid Taawunul Islaam Itoma-Bukoba lilipofanyika Balaza la Eid Fitri kwa mwaka 2019.
Umaati mkubwa wa Waumini wakiwa wamehudhuria Balaza la Eid El Fitri lililofanyika siku ya Idd pili alhamisi ya tarehe 6/6/2019
Baadhi ya Waislamu wa Katoro waliohojiwa nasi wameilezea taasisi hii kama mkombozi anayepaswa kuendelezwa na Waislamu na kutoa wito kwa Waislamu wenye uwezo pamoja na mashirika ya misaada ya Kiislamu kuisaidia taasisi hii ili iweze kutekeleza mipango yake kikamilifu
Al hajji Hashim Kamugunda Mjumbe wa bodi ya taasisi TA'AWUNUL ISLAAM
Katika picha ya pamoja na mwakilishi wa Jambo Bukoba
Hajji Hassim Kamugunda, Taimur,Fadhil Ibrahim na Mkurugenzi wa chuo cha DAN Computer Ndg Abdul Said.
"Matatizo makubwa yanayowakabili Waislamu wengi hivi sasa ni kupata elimu na nyenzo za kuwaendeleza kimaisha hivyo kwamba taasisi mpya iliyozinduliwa leo imechukua majukumu ya kukabiliana na matatizo hayo.."
Mr & Mrs Dattani katika picha ya pamoja na kijana mwenye ulemavu wa macho waliyeweza kumpatia msaada wa matibabu
Sheikh wa Wilaya ya Bukoba Vijijini
Sheikh wa Wilaya ya Missenyi
Picha maalum kwa ajili ya kumbukumbu.
Hajjat Zahara akisisitizia jambo.
Sheikh wa Wilaya ya Missenyi Sheikh Chagulani na Sheikh wa Wilaya ya Bukoba wakibadilishana mawazo na Hajjat Zahara pichani kulia.
Nasaha kutoka kwa Mgeni Rasmi Hamim Mahamud Mwenezi CCM Mkoa
Mgeni Rasmi Hamim Mahamud
Bi Husna akicheck na Camera yetu
Mjumbe kutoka Kanyigo akitoa Salaam
Mjumbe wa taasisi rafiki kutoka kanyigo akiwa tayari kuwasalimia waumini
Taswira mbalimbali wakati shughuli ikiendelea
Taswira mbalimbali wakati maulid ya balaza la Eid el fitr likiwa linaendelea
Bwana Abdulrazak Datan akikabidhiwa rasimu ya taasisi na Mgeni Rasmi Mwenezi wa CCM Mkoa kagera Hamimu Mahamod
Picha mbalimbali zoezi la Uzinduzi wa taasisi ya TA'AWUNUL ISLAAM likiendelea
Mkurugenzi wa Dan Computer akitoa taarifa kwa Waumini waliohudhuria balaza hilo
Wanafunzi wa Katoro Islamic wakiimba Wimbo maalum/Utenzi wa kumpongeza na kumshukuru Hajjat Zahara Dattani kwa anavyojitoa kwa kuimiza na kuchangia harakati za maendeleo kwa jamii yake
Pale Kaswida inaponoga...!!
Wanafamilia katika picha kwa ajili ya kumbukumbu
Picha kwa ajili ya kumbukumbu
Katika kutunza heshima ya kipenzi chetu Mtume Muhammad (s.a.w) heshima ya muumini ipo katika kusimamisha kusoma na kukesha kwa ajili yake
Wimbo maalum wa kumtukuza Mtume wetu uliopata kutamba sana mnami 80s-90s (hakuna shaka kisimamo chetu kikubaliwe...!!
Huduma ya Chakula ilienda sawa bin Sawia wakati wote maulid ikiendelea
Burudani ya Dufu Al Dufufu ikichukua kasi
Muendelezo wa matukio ya picha.
Mama Abdul pichani, mama mdogo wa Hajjat Zahara Dattani
Baadhi ya Waislamu wa Katoro waliohojiwa na #bukobawadau wameilezea taasisi hii kama mkombozi anayepaswa kuendelezwa na Waislamu na kutoa wito kwa Waislamu wenye uwezo pamoja na mashirika ya misaada ya Kiislamu kuisaidia taasisi hii ili iweze kutekeleza mipango yake kikamilifu