Bukobawadau

KAGERA MMEVUNJA REKODI KWA MKAKATI WA KUTANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI MMEJIPANGA VIZURI MTAFANIKIWA – WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA

• Azindua Rasmi Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera
Nimehudhuria makongamano ya uwekezaji katika mikoa sita lakini kwa mkoa wa Kagera kweli mmejipanga kuhamasisha uwekezaji maandalizi yenu si ya michezo mnaye mkuu wa mkoa mbunifu na mfatiliaji, nimepita kwenye mabanda nimejionea bidhaa mbalimbali zinazosindikwa hapa Kagera kweli Kagera kwa mkakati huu mtafanikiwa.
Maneno hayo yalisemwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kagera Agosti 14, 2019 katika viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba alipokuwa mgeni rasmi na kuzindua rasmi Wiki ya Uwekezaji Kagera.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi wa Mkoa wa Kagera alisema kama mkakati wa Wiki ya Uwekezaji Kagera utatumika vizuri utaupandiusha uwezo wa kiuchumi wa mwananchi mmoja mmoja, uwezo wa mkoa pia na Taifa kwa ujumla.
“Kama tutachangamkia fursa ya uwekezaji Kagera tutaweza kuinua zaidi pato la sasa la mwananchi ambapo kwasasa ni shilingi 1,370,000/= kwa mwaka na pato la mkoa la sasa la shilingi bilioni 4.98 aidha, mkoa wa Kagera utachangia zaidi pato la taifa badala ya asilimia 3.9 unavyochangia sas.” Alifafanua Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi pamoja na wageni mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara kutoka nchi za Burundi na Rwanda alisema kuwa kuna sababu za kuwekeza katika mkoa wa Kagera kwa sasa na alizitaja sababu hizo kama ifuatavyo:
Kwanza Mkoa wa Kagera una amani na utulivu na usalama wa kutosha ambapo alisema kuwa mwekezaji yeyeyote anapenda sana kuwekeza sehemu na mahala penye utulivu.
Pili ni fursa za masoko katika mkoa wa Kagera ambapo alisema kuwa mkoa unapakana na nchi nne za Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda lakini pia upo karibu na nchi za Kongo (DRC) na Sudani ya Kusini na kwa ujumla nchi hizo kuna soko la watu zaidi ya milioni 190.
Sababu ya tatu mkoa wa Kagera una hali nzuri ya hewa, ukiwa na rutuba ya kutosha kuotesha na kustawisha mazao yote, ukipata mvua nyingi mara mbili kwa mwaka kuanzia kwa kiwango cha milimita 600 hadi 2000 kwa mwaka. Kutokana na hali hiyo mkoa wa Kagera unaongoza kwa uzalishaji wa kahawa yenye ubora na pendwa sana duniani ya robusta na arabika.
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliwasistiza wafanyabiashara kuja kuwekeza Kagera kwani viwanda vya kuchakata kahawa bado ni vichache sana lakini pia aliwakumbusha wananchi kuanza kuwekeza katika viwanda vidogo na vya kati kusindika mazao mbalimbali na kutolea mfano wa mjasiliamali wa anayetengeneza sabuni kwa mafuta ya mawese kutoka Wilayani Biharamulo anayezalisha boksi 2000 kwa mwaka.
Waziri mkuu Mhe. Kassim Majaliwa aliwasisitiza wafanyabiashara kutoka nchi jirani kuja Kagera kuwekeza katika kilimo cha zao la Vanilla ambalo linalipa sana na maka jana 2018 kilo moja ilikuwa inauzwa kwa shilingi 150,000/=.
Aidha, alisema kuwa Mkoa wa Kagera ni mkoa wenye neema kwani kuna fursa za kuwekeza katika uvuvi, maeneo ya kufugia katika ranchi za taifa ambako kuna zaidi ya hekta 120,000 za kufugia , vile vile alitoa wito kwa Wanankagera pamoja na Watanzania kuchangamkia fursa ya utalii hasa kujenga Mahoteli na kuanzisha makampuni ya utalii ili kuchangamkia fursa ya mbuga za Hifadhi za Taifa za Brigi Chato, Ibanda, na Rumanyika.

Aidha, alisema kuwa Mkoa wa Kagera ni mkoa wenye neema kwani kuna fursa za kuwekeza katika uvuvi, maeneo ya kufugia katika ranchi za taifa ambako kuna zaidi ya hekta 120,000 za kufugia , vile vile alitoa wito kwa Wanankagera pamoja na Watanzania kuchangamkia fursa ya utalii hasa kujenga Mahoteli na kuanzisha makampuni ya utalii ili kuchangamkia fursa ya mbuga za Hifadhi za Taifa za Brigi Chato, Ibanda, na Rumanyika.
Naye Mkuu wa Mkoa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gaguti wakati akitoa neno kabla ya Waziri Mkuu kuwahutubia wananchi alisema kuwa Kagera inawakalisha ukanda wa Kasikazini Magharibi kwa fursa ulizonazo na kuwa kitovu cha biashara kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Pia alimweleza Waziri Mkuu kuwa mara baada ya kukutana na Mabalozi wa nchi tano mkoa umejipangia kwenda katika nchi hizo kuhakikisha fursa zilizowasilishwa na Mabalozi hao zinafanyiwa kazi ili kuufungua uchumi wa ukanda wa Kasikazini Magharibi.
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akikamilisha hotuba yake aliwataka Wakuu wa mikoa wengine kuiga katika mkoa wa Kagera namna ya kutangaza fursa za uwekezaji na kuwahamasisha wawekezaji kuja Kagera kuwekeza kwani panafikika kwa njia zote za anga, barabara, na majini.
Mara baada ya hotuba yake Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alizindua rasmi Wiki ya Uwekezaji Kagera , pili alizindua Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Kagera na alizindua rasmi Kongamano la kujadili na kudadavua fursa za uwekezaji Kagera ambalo litaanza rasmi Agosti 15, 2019 wakati wote huo maonesho ya bidhaa mbalimbali yakiendelea katika viwanja vya Gymkhana Manispaa ya Bukoba.
 Ndani ya banda la Kiwanda cha Kagera Sukari
Mh.Bernadeta K. Mushashu akitolea jambo ufafanuzi kwa Waziri Mkuu ,Mh.Kassim Majaliwa.
Muonekano wa Nje banda la Kagera Sukari
Burudani kutoka kwa Msanii Saida Karoli
 Taswira mbalimbali Viwanja vya Ghymkhana wakati mkutano unaendelea
 Taswira mbalimbali Viwanja vya Ghymkhana wakati mkutano unaendelea
 Mweyekiti wa CCM (W), Bukoba Ndg. Joas Muganyizi Zachwa mara baada ya kusalimiana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa
Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimia na  Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Kagera, Hamimu Mahamud
 Waziri Mkuu Kassim M. Majaliwa akisalimiana na Ndugu Wilbroad Mutabuzi (Mnec) Mkoa Kagera
 Mjumbe wa Kamati ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana Taifa Ndg Joanfaith Kataraia akisalimiana na Mheshimiwa Kassim M. Majaliwa (MB.), Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
  Mheshimiwa Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim M. Majaliwa akiteta jambo na Ndugu Seif Mkude Mewenyekiti wa wafanyabiashara Mkoa Kagera
 Ndani la banda la kiwanja cha Tanica
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Nkenge  Balozi Doudorus Kamara
 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akisalimiana na Mbunge wa Jimbo la Nkenge  Balozi Doudorus Kamara
 Muendelezo wa Matukio ya picha kutoka viwanja vya Ghymkhana Mjini Bukoba
 Amimza Cafe wazalishaji wa kahawa bora kabisa
Ndugu Thomas Charles akiwa Uwanjani hapo
 Kagera ni  Mkoa wenye fursa kubwa ya uwekezaji kwenye viwanda vya kukoboa na kusindika kahawa


Muonekano wa banda la Halmashauri ya Wilaya Muleba
Credit :Na: Sylvester Raphael 
Next Post Previous Post
Bukobawadau