Bukobawadau

Mjumbe Wa Kamati ya ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM Taifa Ndg Joanfaith kataraia alizindua Rasmi Kampeni ya Kijani Katika Wilaya Ya Mafia Mkoani Pwani

Mjumbe Wa Kamati ya ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM Taifa *Ndg Joanfaith kataraia* tarehe 28 Septemba 2019 alizindua Rasmi Kampeni ya Kijani Katika Wilaya Ya Mafia Mkoani Pwani .
Awali akizungumza na Mamia ya wana CCM waliohudhuria uzinduzi huo Ndg Joanfaith amewaasa kuendelea kuunga Mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano Inayoongozwa na Mwenyekiti Wa CCM Taifa Dkt John Pombe Magufuli kwa kuendelea kudumisha Umoja na Ushirikiano katika Shughuli mbalimbali za kuijenga Jamii.
Pia Ndg Joanfaith amewataka Vijana hao kuendelea kuwa mabalozi wazuri wa Chama Na Serikali kwa Kuyasemea Mambo yoye yanayotekelezwa na Serikali pamoja na kuwa Maadui na wapenda Rushwa,wakandamizaji,wakwepa kodi pamoja na wabaguzi wapinge kabisa mambo yote yanayorudisha maendeleo ya mafia nyuma.
Aidha ametumia fursa hiyo kuwakumbusha Wananchi wote juu ya Uandikisha wa Daftari la Wapiga kura na Kuwataka Vijana wote kuendelea kuhamasishana kwa kupeana elimu ili itakapofika wakati wa Uchaguzi kila mmoja apate nafasi ya Kuchagua kiongozi bora na Viongozi bora wote wanatoka CCM.
Wananchi wakimsikiliza Ndg Joanfaith kataraia*Mjumbe Wa Kamati ya ya Utekelezaji ya Umoja wa Vijana wa CCM Taifa
“Viongozi tunalo jukumu la kuhamasisha Vijana kujiandikisha katika daftari la Mpiga kura kwa Mujibu wa Kalenda ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) tupite nyumba kwa nyumba,kijiwe kwa Kijiwe,Kisiwa kwa Kisiwa ili tuhakikishe tunapata Viongozi bora Wanaotokana na Chama Cha Mapinduzi “Alisema Ndg Joanfaith.
#TukutaneKazini
Next Post Previous Post
Bukobawadau