Bukobawadau

UVCCM MKOA KAGERA WATOA MSAADA WA KIJAMII KWA WANAFUNZI WENYE MAHITAJI MAALUMU WA SHULE YA MSINGI KAIGARA WILAYANI MULEBA.

Umoja wa Vijana wa CCM Mkoa wa Kagera* leo Jumatatu Novemba 25,2019 Umetoa Mchango wa kijamii kwa kutoa Msaada wa Magodoro, Sabuni,taulo za kike, Kalamu na Karatasi za Mitihani kwa Shule ya Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum ya Kaigara iliyopo Wilayani Muleba.
Viongozi wa Uvccm Mkoa wa kagera wametumia nafasi hiyo kuongea na Walimu na kuwafariji watoto hao wenye mahitaji maalumu kama anavyoonekana Mtoto Furaha pichani akiteta na Viongozi hao.
 Uongozi wa Uvccm mkoa wa kagera Uliongozwa na mwenyekiti wake Ndugu Happiness Runyogote, Mjumbe wa kamati ya Utekelezaji Uvccm Taifa kutoka mkoa wa Kagera Ndugu Joanfaith Kataraia, Mjumbe wa baraza kuu Uvccm Taifa Fahami Matsawili, Katibu wa chipukizi na Hamasa Uvccm Mkoa Ndg Samidu kajumulo, Mwenyekiti wa Uvccm wilaya ya Muleba Mtwawafu, na katibu wa Uvccm wilaya ya Muleba.
Mjumbe Kamati ya Utekelezaji UVCCM Taifa, Joanfaith Kataraia katika picha ya pamoja na wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa shule ya Msingi Kaigara iliyopo Wilayani Muleba siku ya jana Uongozi wa Uvccm Mkoa Kagera ulipotembelea shuleni hapo na kukabidhi msaada wa vitu mbalimbali.
 Mwenyekiti wa Uvccm Mkoa Kagera Ndg. Happiness Runyogote akizungumza  na Walimu na wanafunzi wenye mahitaji maalumu wa shule ya Msingi Kaigara kuhusiana na lengo la ziara yao shuleni hapo
 "Ni jukumu la kila mmoja kuthamini mahitaji ya kielimu kwa watoto wenye ulemavu na mahitaji Maalumu";Mjumbe wa baraza kuu Uvccm Taifa Fahami Matsawili
 Bango la Shule ya Msingi Kaigara iliyopo Wilayani Muleba
Kutowaacha nyuma watoto wenye ulemavu ni kutimza mahitaji.
 Katika picha ya pamoja  viongozi wa Uvccm na baadhi ya Walimu wa shule ya Msingi Kaigara
 Mwalimu Jesse Tibaijuka  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kaigara pichani kulia, akiongozana na Viongozi hao kuelekea kwenye Mabwenu yanayotumiwa na Wanafunzi wenye uhitaji maalumu
Mwalimu Jesse Tibaijuka  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kaigara pichani katikati akiongozana na Viongozi hao kuelekea kwenye Mabwenu yanayotumiwa na Wanafunzi wenye uhitaji maalumu
 Shule hii inajumla ya wanafunzi 60 wenye mahitaji maalum, Changamoto kubwa tuliyonayo ni Mabwenu kwa ajili ya wanafunzi hao amesema; Mwalimu Jesse Tibaijuka  Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kaigara na kuishukuru Serikali kwa juhudi kubwa zinazoendelea kuchukuliwa  katika kutambua changamoto zinazowakabili wanafunzi wenye mahitaji maalumu.




Next Post Previous Post
Bukobawadau