Bukobawadau

BWANJAI COMMUNITY GROUP WAFANIKISHA SHEREHE YA BWANJAI DAY 2019'

Mgeni Rasmi Katibu Tawala wa Mkoa wa Kagera Profesa Faustin Kamuzora wa pili pichani kulia akiwasili eneo la tukio kwa ajili ya kushiriki sherehe za Bwanjai Day zilizofanyika  viwanja vya shule ya Msingi Mugana B  tarehe 27/12/2019 na kuhudhuliwa na watu wengi,Sherehe hizo zimeandaliwa na 'Bwanjai Community Group' ziliambatana  na zoezi la upimaji wa Afya kwa wananchi wote,Wanakamati  kutembelea miradi ya maendeleo,Semina kuhusu ( kilimo,ufugaji,mazingira na ujasiliamali) burudani za aina mbalimbali pamoja na harambee.
Kikundi cha Bwanjai  Community Group kilichoanzishwa mnamo tarehe 25/01/2015 kupitia mtandao wa kijamii wa Whatsaap sambamba na mtandao wa Whatsaap kikiwa na madhumuni ya kuhamasish WanaBwanjai wahishio nani na nje ya Kata ya Bwanjai iliyopo Wilayani Missenyi .Kushiriki katika shughuli za maendeleo ya kiuchumi,kiutamaduni na kijamii ili kata ya Bwanjai iweze lusonga mbele kimaendeleo katika Nyanja zote hususani Elimu,Afya na ustawi wa jamii kwa ujumla
Hadi hivi sasa kundi hili linajumla ya washiriki(participants) 149 kutoka ndani ndani na nje ya Bwanjai na wengine ambao ni wazaliwa wa kata hiyo lakini wameendelea kuunga mkono harakati hizo
Idadi hii inaweza ikawa ni ndogo kulingana na Idadi ya wazaliwa wa kata ya Bwanjai hivyo hivyo WanaBwanja wote popote walipo mnaombwa kujiunga na kuwaunga mkono 'Bwanjai Community Group'
Afisa Mtendaji waKata ya Bwanjai amedhibisha kuwa Bwanjai Community Group imefanya kazi kubwa sana katika kuchangia shughuli za maendeleo ndani ya kata ya Bwanjai. na kwa mwaka 2020 Bwanjai Community Group inayo malengo ya kuendelea kuchangia maendeleo ya kata hasa upande wa Elimu.
Bwanjai Community Group wanatalajia kuanzisha kuanzisha ujenzi wa wa Bweni la Wasichana shule ya sekondari Bwanjai,Jengo la Bwana hilo linakadiliwa kutumia jumla ya shilingi 160,000,0000/= na ujenzi wa msingi utaanza mwakani,Pili Bwanjai Community Group baada ya kupokea maombi kutoka bodi ya ya shule ya Sekondari Bwanjai wameamua kwa kuanzia kununua set ya Computer (Desk top) pamoja na printer vyenye thamani ya shilingi 1,250,00/= ili kuwezesha walimu  kufanya maandalizi ya vipindi na mitihani pamoja na Tahama kwa ujumla
Tatu ,Bwanjai Community Group watatoa motisha ya sh 400,000/= kwa walimu kwa ajili cha chai ya asubuhi pindi wawapo kazini
Bwanjai Community Group wapo tayari kuchangia shughuli za maendeleo kwenye shule za msingi kama ambavyo wameishafanya kwenye kwenye baadhi ya shule.
Dr.Frank Ludigo mdau wa maendeleo wa Kata ya Bwanjai -Kiziba Wilayani Missenyi
Muendelezo wa matukio ya picha sherehe za Bwanjai Day


Muendelezo wa matukio ya picha
 ITAZAME KATIKA VIDEO

  Credit @Bukobawadau ,Video na Millarday
Next Post Previous Post
Bukobawadau