Bukobawadau

BISHOP MUSHEMBA FINAL FAREWELL TO HIS LAST JOURNEY HELD AT KANISA KUU (KKKT) BUKOBA

Bishop Mushemba Final Farewell to His Last Journey held at Kanisa Kuu (KKKT) Bukoba
Baba Askofu Fredrick Shoo,Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),Leo tarehe 15,April 2020 ameongoza Ibada ya Mazishi Baba askofu mstaafu Dr, Samson Mushemba yaliyofanyika katika Kanisa kuu la KKKT Bukoba,pichani Askofu Shoo akikabidhi rambirambi kwa wanafamilia ya Baba Askofu Mushemba
Pamoja na kuwa Askofu Mkuu wa KKKT nchini pia Dr.Samson Mushemba aliwahi kuwa Akofu wa awamu ya tatu, Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, Bukoba tangu 1984 hadi 2000,Akiongoza ibada ya mazishi, Askofu Mkuu wa KKKT, Dk. Frederick Shoo, alisema Askofu Mushemba hakufanya kazi kwa ajili ya kanisa tu bali kwa jamii nzima ya Watanzani......
 Mazishi hayo yamehudhuriwa na Viongozi Serikali na Dini mbalimbali watu mashuhuri na viongozi wa vyama.
Jeneza lenye mwili wa  Baba askofu mstaafu Dr, Samson Mushemba likiwasili viwanja la Kanisa kuu Bukoba


Msafa ukielekea ndani ya kanisa Kuu kwa ajili ya Ibada na Mazishi ya wa Askofu Dk. Samson Mushemba aliyewahi kuwa Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), umezikwa nje ya Kanisa Kuu la Bukoba Mjini, huku viongozi mbalimbali wakisema enzi za uhai wake alikuwa mfano wa kuigwa kutokana na utumishi wake kugusa maisha ya wengi.
 Dk. Mushemba ambaye alifariki dunia Aprili 9, mwaka huu, wakati akipatiwa matibabu Hospitali ya Ndolage Kamachumu, alizikwa jana katika kanisa hilo Dayosisi ya Kaskazini Magharibi, huku mazishi yake yakihudhuriwa na viongozi wa mbalimbali wa dini na wananchi kutoka maeneo mbalimbali.
Askofu Shoo wakati wa Ibada amesema;“Unaweza kuwa mtumishi, lakini ukawa si mfuasi wa Kristo katika tabia yako, matendo na mwenendo wako mzima. Mfuasi wa kweli wa Yesu anamtii bwana na mwokozi wake, anamfuata huyu Yesu kristo, alikuwa mtu mnyenyekevu, mtu mtii kwa bwana kama baba, mchungaji, askofu, mkuu wa kanisa na kiongozi akawa mtu wa maombi,” alisema Dk. Shoo.
Ma Yudesi rafiki wa familia ya Marehemu Askofu Mushemba akifuatilia Ibada..
Kutoka Jimbo la Karagwe Salaam za rambirambi zikitolewa...
Rev Modest Pesha pichani katikati akifuatilia kinachojiri Mazishi ya Askofu Samson Mushemba...
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dk Fredrick Shoo na  Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Jimbo Kuu la Bukoba, Dk Abelnego Mushahara
Katibu Mkuu wa Dayosisi Ndugu Kigembe akitoa ufafanuzi kulingana na ratiba.
 Muonekano wa Jeneza lenye mwili wa Askofu (Mstaafu) wa KKKT Dkt. Samson Mushemba wa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi #BukobaAskofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Jimbo Kuu la Bukoba, Dk Abelnego Mushahara
 Viongozi Mbalimbali wa Chama na Serikali wameweza kushiriki mazishi hayo...
 Katibu Mkuu wa Dayosisi Ndugu Kigembe
 Taarifa kutoka hospitali ya Ndolage kufuatia kifo na sababu kuhusu umauti wa Askofu Mushemba


 Taswira mbalimbali Ibada ya Mazishi ikiendelea...
 Sheikh Kakwekwe wa Bakwata
 Mhashamu Askofu Dederius Rwoma wa Jimbo Katoliki la Bukoba
 Askofu Methodius Kilaini ambaye ni Askofu msaidizi wa jimbo Katoliki Bukoba akitoa salaam za rambirambi msiba wa Baba Askofu Mstaafu Samson Mushemba
 Muendelezo wa matukio ya picha
 Muendelezo wa matukio ya picha Salaam za rambirambi zikiendelea..
Viongozi mbalimbali Maaskofu na Masheikh wakifuatilia kinachojiri
Bwana Kandanda Bwanika ni miongoni mwa waombolezaji walioshiriki Ibada ya Mazishi hayo
Neno kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti 
Neno la familia likitolewa na Mtoto wa Marehemu Mushema Josephat Mushemba, alisema baba yao alipenda kuwa na uhusiano na watu wote na hata alipostaafu alichagua kuishi kijijini, huku akiwasaidia watu mbalimbali.
“Hakuwa na ubaguzi kwa watoto, hakuwa na ubaguzi wa dini, nyumba ya baba imekuwa ni nyumba ya watu wa dini zote, tuliishi na watu wa aina mbalimbali na kabila mbalimbali.
Baba yetu alilikuwa tayari kuomba msamaha kwa watu wote hasa kwetu sisi watoto pale alipokuwa amekosea au kumkwaza yeyote, kwa mfano miaka 10 iliyopita alimpelekea ndugu yake kitenge sasa yule ndugu yake alichukia sana, na kusema (yaani ndugu husika) kwanini unaniletea kitenge akamrushia, baba hakusema chohote aliondoka na kukiacha. Baba alianza kulia akasema muende mumlete yule mama alipo nimuombe msamaha kabla sijafa
Ninachokumbuka ni kwamba Baba alimuomba Kaka yetu mkubwa ajaribu kumtafuta kumfuata yule mama kusudi amuombe msamaha, baba akasema mpelekeeni Sh 50,000 za chakula alizokuwa akidai,”ili nafsi ya Mzee ipate kulidhika  na huyo ndo Baba yetu tunavyomjua sisi wanae..
Askofu shoo akiongoza Ibada amesema;“Unaweza kuwa mtumishi, lakini ukawa si mfuasi wa Kristo katika tabia yako, matendo na mwenendo wako mzima. Mfuasi wa kweli wa Yesu anamtii bwana na mwokozi wake, anamfuata huyu Yesu kristo, alikuwa mtu mnyenyekevu, mtu mtii kwa bwana kama baba, mchungaji, askofu, mkuu wa kanisa na kiongozi akawa mtu wa maombi,”
Jeneza lenye mwili wa Baba Askofu Samson Mushemba aliyezaliwa wa Juni 30, 1935 ameacha mjane, watoto saba, wajukuu 22 na kitukuu kimoja


Taswira mbalimbali ndani ya kanisa kuu la KKKT Bukoba
 Dean mstaafu Rwankomezi na Rev.Lugemeleza wa Kanisa kuu pichani kulia wakishiri
Dean Jackson Mushendwa pichani kulia akiwa na Maaskofu wakati wa Mazishi...
Askofu Fredrick Shoo,Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT),akiweka shada la maua kwenye kaburi la Askofu Mushemba..
 Mkuu wa Mkoa wa Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gaguti akiweka shada la maua pamoja na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera mama Costancia Buhiye
Watoto wa Marehemu Askofu Mushemba wakiweka shada la maua
Askofu wa Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Benson Bagonza akiwa tayari kuweka shada la maua
Askofu wa Dayosisi ya Karagwe ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk Benson Bagonza mara baada ya kuweka shada la maua


 Viongozi wa Baraza kuu la Waislam (BAKWATA) wamewakilishwa na Sheikh Kakwekwe akiweka shada la maua pamoja  Sheikh Hashim Kamugunda Mwenyekiti wa Jumuiya ya Imamu Shafii Mkoa Kagera
 Mzee Godwin Rwezaula katibu mkuu Mstaafu akiweka Shada la maua...
 Mbunge wa Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka Mama Anna Tibaijuka akiweka shada la maua
 Pia yupo aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna mstaafu Alfred Tibaigana kama anavyo onekana pichani akiweka shada la maua kwenye kaburi la Baba Askofu Mushemba.


 Muendelezo wa matukio ya picha eneo la kaburi.
 Askofu Rwoma na Askofu Kilaini wakiwa tayari kuweka Shada la Maua
 Askofu Methodius Kilaini na Mhashamu Askofu Dederius Rwoma
 Rev.Lugemeleza na Dean Jackson Mushendwa wakikamilisha kwa kuweka bango lenye ujumbe katika kaburi la Baba Askofu Mushemba.
 Raha ya Milele umpe Ee Bwana na Mwanga wa Milele umwangazie ...Apumzike kwa aman
 Bwana Josephat Mushemba mtoto wa Marehemu Askofu Mushemba pichani kushoto,Katikati ni rafiki yake Jamal Kalumuna wakiwa na jamaa  wa karibu na familia
 Bi Jennifer Murungi na Kibira pichani..
 Viwanja vya Kanisa Kuu,Ulipozikwa Mwili wa Baba Askofu Samson Mushemba
 Katibu wa CCM Mkoa Kagera katika picha na Mzee Pius Ngeze..
 Ndugu Msheshe Meneja wa ELCT Hotel Bukoba akitoa ufafanuzi kuhusiana na masuala ya Menu kwa watu wote walioweza kushiriki Mazishi ya Askofu Samson Mushemba
 Mzee Muganyizi Zachwa pichani kulia akitete na Bi Jeniffer..
 Mzee Godwin Rwezaula mara baada ya shughuli ya Mazishi ya Baba Askofu Mushemba
 Watoa huduma ya kwanza ...
 Kijana Mwesiga akiwajibika usalama wa Nje ya kanisa..
 Asnath Askari akiwajibika eneo la usalama wa Parking...
 Hapa ni maeneo ya Kyetema -Bukoba wakati msafara ukitokea Kamachumu Nyumbani kwa Marehemu Baba Askofu Mushema
 Msafara huo ukiongozwa na Patrick Kaimukilwa pichani
 Wakati Msafara wenye Mwili wa Baba Askofu Mushemba ukitokea nyumbani kwake Kijijini Kamachumu kuelekea Kanisa kuu Bukoba ,Baba Askofu Dk. Mushemba lifariki dunia Aprili 9, mwaka huu akipatiwa matibabu Hospitali ya Ndolage Kamachumu-Muleba , Mazishi yake yamefanyika katika Viwanja vya Kanisa Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Bukoba
 Maeneo ya Rwamishenye...msafara ukielekea Mjini Kati.
Next Post Previous Post
Bukobawadau