Bukobawadau

FAMILIA INATOA SHUKRANI KWA WALIOSHIRIKI MSIBA WA BABA YETU MZEE PAUL BASHEREKA..


Familia ya Marehemu Mzee Paul Bashereka wa Kitendaguro Bukoba inayo heshima kubwa kutoa shukrani za dhati kabisa kwa ndugu, jamaa na marafiki ambao walishiriki kwa namna moja ama nyingine kufanikisha msiba, mazishi na hatimaye matanga ya Mzee/Baba yao mpendwa,Paul Bashereka (88) aliyefariki dunia usiku wa Jumapili April 5,kwenye Hospitali ya TMJ na kuzikwa Nyumbani kwake Kitendaguro Manispaa ya Mji Bukoba,Alhamis ya April 9,2020
Mama Mzazi wa familia Ma Bernaidina katika picha ya pamoja na mabinti zake pamoja na wakwe wa familia.
Kwa vile waliotuunga mkono na kutufariji wakati wa kipindi hiki kigumu cha msiba huu mkubwa ni wengi na ni vigumu kuwataja wote kwa majina, Familia, inapenda kwa heshima na taadhima nyingi kutoa shukrani za jumla ikiwaomba wote mkubali kuzipokea kwa moyo ule ule kama mlivyotuunga mkono. Mmetufariji sana, mmekesha nasi, mmeshinda nasi, nyote mmekuwa kimbilio salama kwetu wakati wa kipindi hiki kigumu;Mzee Robart Matungwa Kaka Mkubwa wa familia.

Wakisali kwa unyenyekevu mkubwa...
Mwanzo wa Ibada ya kuanua Matanga Msiba wa Mzee wetu Mzee Paul Bashereka
Kaka Medard Bashereka akisoma neno la Bwana...
Padre akitoa mahubiri wakati wa Misa ya Matanga ya Mzee wetu Mzee Paul Bashereka
Wanafamilia wakiendelea kushirika Ibada ya Matanga ya kumaliza msiba wa mpendwa wao..
Wanafamilia na Ndugu na  jamaa wa karibu na wakiendelea na Ibada ya Matanga ya Mzee wetu mpendwa...
Muendelezo wa matukio ya picha Ibada ikiendelea,,,,Matanga ya Mzee Paul Bashereka.

Wanakwaya wa Kitendaguro wakiendelea kushiriki Ibada hiyo...

Familia inasema;Mmeonesha upendo wa kweli kweli kwetu kama Familia na kwa mwanetu dada yetu ambaye angerejea kwenye uzima tena, naye bila shaka yoyote angetoa shukrani za dhati ya moyo wake

Tukio lililoambana na Ubatizo wa Mjukuu wa Mzee Robart Matungwa,Mtoto wa Walter Matungwa pichani kulia.

Hakika Sakramenti ya kwanza daima ni ubatizo...
Hongera Walter hongera kwa familia kukamiliza ubatizo ikiwa ni uzima mpya kwa mtoto wenu.
Na ni heri kuiendea nyumba ya matanga, Kuliko kuiendea nyumba ya karamu. Kwa maana huo ndio mwisho wa wanadamu wote, naye aliye hai atautia moyoni....
Wanafamilia wakiendelea na Ibada..


Mama Deo,Benna akiendelea kushiriki Misa ya Matanga ya mpendwa wetu Mzee Paul Bashereka.

Picha zote zinajitoshereza endelea kufatilia ukurasa wetu mpaka mwisho...Waumini wakipata Komonio...Kaka Lomward Bashereka akipata komonia katika Misa ya matanga msiba wa Baba yake mzazi

Mama yetu Ma Bernaidina Bashereka

Kaka Romward Bashereke,akiwa eneo la makaburi kuwaombea wapendwa wetu waliotangulia mbele ya haki

Wanafamilia na Wanaukoo wakiwa eneo la kaburi kwa ajili ya Misa fupi ya kumuombea mpendwa wao.


Ibada fupi eneo la kaburi....

Bi Benna Kurji /Mrs Deo rafiki wa familia


Ms Lesper George na Kijana Amon katika picha ya pamoja..

Wajukuu wa familia katika picha ya pamoja kwenye kaburi la Mpendwa Babu yao,pichani yupo Atu, Elina, Malaika, Walter, Samuel na Emille.

Baada ya Masuala ya Ibada Sasa tunaendelea kupata vinjwaji, Msosi na Burudani..

Murungi Badru Kichwabuta na Bi Jamila wa Jamco wakibadilishana mawazo

Mr.Manyele Mkwe wa familia hii..


Mzee Robart Matungwa akifuatilia kinachojiri...

Kaka Medard Bashereka pichani akifurahia jambo...

Picha zinazungumza, endelea kufuatriria mtiririko mzima mpaka mwisho yaliyojiri katika Misa ya matanga ya Mzee wetu Paul Bashereka...

Yote haya ni kutoka Kitendaguro nyumbani kwa familia ya 'Bashereka'

Mama Khajda pichani akifatilia kinachojiri

Maelekezo,Bwana Matunda akipokea utaratibu kutoka kwa Mzee Matungwa.

Taswira mbalimba kitovu cha Green Hill nyumbani kwa familia ya Mzee Bashereka

Mwalimu George pichani...


Kivutio kikubwa ni uwezo wa wanakwaya wa BCC ...

Wanakwaya wakiwajibika vyema kwa nyimbo na muziki mtakatifu Wakitumbuiza...

Marafiki wa wanafamilia wakiendelea kujumuika kwa pamoja.

Mr Manyere Frednand na Mke wake Liberatha Bashereka

Hata hivyo, tunapenda kutoa shukurani kwa makundi machache ya marafiki ambao mchango wao utabakia kwenye nyoyo za wazazi na familia yetu tukianza na majirani na marafiki wa karibu wa Familia.

Kuelekea Mwisho Shukrani ya familia ikitolewa na Mzee Robart Matungwa.

Mtaalam Roben Sunday pichani.

Mzee Byamungu pichani kulia...Ubora wa picha wasiliana nasi....

Muendelezo wa matukio ya picha kwa ajili ya kumbukumbu


.......Picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu

Matukio ya Picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu....

Muendelezo wa matukio ya picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu mara baada ya Shughuli ya Matanga ya Mzee wetu Baba yetu Paul Bashereka

Mtu na Wifi yake wakicheck na Camera yetu...

Bi Jeannefer Murungi Kichwabuta na Mama Totoz wakimfariji Mfiwa Dada Libe Bashereka..

'Okushura' kwa Buhaya ni matendo ya kitamaduni ikiwa ni ishara ya Upendo undugu kwa kumfariji mfiwa....

Mama Totos 'Kamama' akiongozana na Dada Liberatha Bashereka... kuelekea ndani

Dada Liberatha akinoa "Ahsante".....Neno hili huashiria shukrani kwa kutendewa jambo fulani au kupewa kitu fulani.Wachache sana hulitumia neno hili japokuwa ni neno muhimu sana.Mtu anapokutendea jambo au kukupa kitu fulani,ni vyema kumwambia 'ahsante'.Mtu huyo atafurahia kwa kuwa umeonesha tabia nzuri na Wema uliotukuka...

Kwa niaba yake na kwa niaba ya familia anaendelea kutoa shukrani kwa watu wote waliowaunga mkono...Neno ahsante lina maana kubwa sana katika maisha ya kila siku ya hapa duniani.

Mama Totos 'Kamama' akishow love na Dada yake mpendwa Bi

Moja kati ya picha ni Mzee Robart Matungwa na rafiki yake Mzee Cathbert Basibila

Muendelezo wa picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu..

Mama Mdogo pichani akicheck na Camera yetu

Katika hili na lile...

Mwalimu Mugango akipotezea mara baaada ya kuwajibika...

Baada ya Ibada na kutoka eneo la kaburi hivi ndivyo mambo yalivyoendelea,Matanga ya Mpendwa Baba yetu Mzee Paul Bashereka..Wanakwaya wakiwajibika vyema kwa nyimbo na muziki mtakatifu Wakitumbuiza...
Next Post Previous Post
Bukobawadau