UMATI WAMLILIA BEATRIX MADONNA BAIKIRIZA
Nyota imezimika mapema,familia ya Bwana George Kakembwe imepata pigo,tangulia Beatrix tupo nyuma yako.
Jeneza lenye Mwili wa mpendwa wetu Marehemu Beatrix Madonna Bairikiriza mara baada ya kuwasili nje ya Kanisa Katoliki la Rutabo,Kamachumu.
Hajjath Zahra akiwa ameungana na waombolezaji wengine pamoja na wanafamilia wakiwa kushiriki Ibada ya mazishi ya mpendwa wetu Beatrix Madonna Baikiriza,mtoto wa Ndugu George Kakembwe pichani kulia...
Waombolezaji wakiwa nje ya Kanisa kabla ya Ibada ya Mazishi ya mpendwa wetu Beatrix Madonna Baikiriza
Taswira nje ya Kanisa Katoliki Parokia ya Rutabo
Misa ya Mazishi imeongozwa na Askofu wa Jimbo Katoliki la Bukoba Mhashamu Desderius Rwoma
Idadi kubwa ya Mapadre na watawa wakiongozwa na Mhashamu Baba Askofu Deoderius Rwoma wameweza kushiriki Ibada ya mpendwa wetu Beatrix Madonna Baikiriza..
Beatrix Madonna wa Ukoo wa Muyegkazi, alizalwa tarehe 14/7/1991 katika hospital ya Ndolage Kamachumu na kupata ubatizo Parokia ya Rutabo tar 12/3/1992 namba ya upatizo 44412 mbatizaji wake akiwa fr John Joseph chini ya usimamizi wa Maregemu Bibi yake mpendwa
Marehemu Beatrix Madonna pichani enzi za uhai wake,Taarifa ya familia inasema;Marehemu Beatrix wakati akiwafanya Mtihani wake wa Masters ,ghafla alipoteza Uoni wa macho na hivyo kushindwa kumaliza mitihani yake,jitihada nyingi zimefanyika za kimatibabu kujaribu kurudisha uoni wa Macho yake bila mafanikio na kadri muda ulivyo ongezeka tatizo hilo lilipelekea ulegevu na kupoteza nguvu mwilini mpaka mauti unamkuta akiwa anapata matibabu katika hospitali ya Mhungula iliypo Kahama.
Umati wa waombolezaji nje ya Kanisa la Rutabo kabla ya Ibada ya mazishi ya mpendwa Beatrix Madonna Baikiriza
Endelea kufuatilia ukurasa huu kwa mtitiriko mzima wa matukio yaliyjiri katika Mazishi ya Mpendwa wetu Beatrix Madonna George
Paroko wa Parokia ya Rutabo katika Ibada ya Mazishi ya Beatrix Madonna Baikiriza
Mhashamu Baba Askofu Deoderius Rwoma akiendelea kuongoza Ibada ya Mpendwa Beatrix Baikiriza
Waumini wakiendelea kushiriki Ibada..
Ibada ikiendelea...
Mhashamu Baba Askofu Deoderius Rwoma akiongoza Ibada hiyo iliyofanyika katika katisa la Rutabo,Kamachumu.
....Muendelezo wa matukio ya picha Msiba wa Beatrix George.
Jeneza lenye mwili wa Mpendwa wetu likiingizwa kaburini
Jeneza lenye mwili wa Mpendwa wetu likiingizwa kaburini
Mama Beatrixmachozi yakimtoka wakati Jeneza likiingizwa Kaburini.
Mzee George Kakembwe na Mke wake wakiwa tayari kuweka shada la maua kwenye kaburi ya Binti yao mpendwa Beatrix Madonna
Wazazi wa beatrix wakiweka shada la maua
Mhashamu Baba Askofu Deoderius Rwoma akiweka shada la maua
Askofu Rwoma alipokuwa akiweka shada la Maua katika kaburi la mpendwa wetu Beatrix
Utaratibu wa kuweka mashada ya maua ukiendelea kwa kuzingatia makundi mbalimbali
Raha ya Milele Umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie Apumzike kwa Amani Mpendwa wetu Beatrix..
BWANA alitoa, na BWANA ametwaa; jina la BWANA lihimidiwe Ameen.
Mwenyezi Mungu ampe pumziko na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Ameen; Salamu za pole kutoka kwa Hajjath Zahra pichani kushoto
Salaam za rambirambi kutoka kwa Bwana Saulo..
Makundi mbalimbali yakiendelea kutoa salaam za rambirabi
Mwakilishi ya Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Muleba Kaskazini Charles Mwijage akikabidhi rambirambi kwa baba Mzazi wa Marehemu Beatricx.
Muendelezo wa matukio ya picha...
Mtaalam Njoka pichani ni mmoja kati ya waombolezaji.
Pole sana wafiwa Mungu...awape subira na uvumilivu ni wakati mgumu sana kwenu..
Pole sana wafiwa Mungu...awape subira na uvumilivu ni wakati mgumu sana kwenu..
Umati wa waombolezaji wajitokeza katika kanisa la Rutabo na baadae kijijini Nyumbani 'Amchwezi' kwa Bwana George katika misa ya wafu ya mazishi ya Beatrix Madonna Baikiriza.
Familia inatoa shukrani za dhati kwa wapendwa wote walioshiriki kwa namna moja ama nyingine katika kutetea maisha ya Mpendwa Beatrix George Kakembwe katika safari yake ya maisha hapa Duniani.
Mwenyezi Mungu awabariki sana, Raha ya Milele Umpe ee Bwana, na mwanga wa milele umwangazie Apumzike kwa Amani Beatrix.
Umetangulia Beatrix ,tunaamini ataendelea kufurahia aina ya maisha katika nyumba yako ya Milele...
Mwalimu Russeta ni miongoni mwa waombolezaji walioshiriki Ibada ya Mazishi hayo.
Muendelezo wa matukio ya picha kutoka msibani hapo.
Viunga vya mji mdogo wa Kamachumu msafara mkubwa wa Magari ukielekea kanisani.
Eneo la maegesho
Msafara wakati ukielekea Kanisani Rutabo.
Taswira mbalimbali mara baada ya Mazishi ya Mpendwa wetu Beatrix Madonna Baikiriza (1991-2020)