Bukobawadau

VILIO NA MACHOZI MAZISHI YA PROF BAREGU

Mamia ya waombolezaji, wanazuoni ,watu mashuhuri na viongozi wa vyama vya siasa wameshiriki ibada ya Mazishi ya nguli wa siasa,msomi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Mwesiga Nyumbani kwake Kijijini Maruku Bukoba.

Mjane wa hayati Prof  Baregu na watoto wake wakionyesha kupokea neno kutoka kwa msemaji wa Familia. 

Viongozi wa Chadema wakiongozwa na M/kiti wa Chadema Taifa, Mhe Freeman Mbowe wakiwa wameshiriki Mazishi ya nguli wa siasa,msomi na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Mwesiga Nyumbani kwake Kijijini Maruku Bukoba.


Muendelezo wa matukio ya picha
Taswira mbalimbali msibani Nyumbani kwa Prof.Baregu

Mama Bayona pichani akiendelea kushiriki Ibada ya mazishi ya mpendwa wetu Prof Baregu

Muendelezo wa matukio ya picha

Saimon Baregu akifuatilia kinachojiri
Pichani ni watoto wakuzaliwa na Prof Baregu

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa , Freeman Mbowe akitoa neno na Salaam za rambirambira Msiba wa Prof Baregu

Salaaam za rambirambi kutoka kwa
Freeman Mbowe ,Mazishi ya Prof Baregu Kijijini Maruku Bukoba.
Salaam za rambirambi zikiendelea .....

Salaam za rambirambi kwa niaba ya Umoja wa Wana Maruku waishio nje na ndani ya nchi
Hii ndiyo hali halisi kwa kila aliyemuelewa vyema mpendwa wetu Prof Baregu.
Hakika ni Uchungu vilio na Machozi....Mazishi ya Prof Maregu.

Salaam za rambirambi kutoka Stanbic Bank Tanzania .

Marafiki wa karibu wa familia wakiendelea kutoa Salaam za rambirambi
Poleni sana kwa msiba uliowapata. Mungu awafariji wafiwa,na kuwatia nguvu

Ndugu wafiwa Mwenyezi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu na ampuzishe  kwa Amani mzee wetu Jemedali wetu.
Mwakilishi wa Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Mendeleo Chadema Mkoa Kagera akitoa salaam za rambirambi kwa niaba ya Wanawake wa Chadema Kagera na kwa niaba ya Baraza la Wanawake wa Chadema - BAWACHA

Profesa Gelase Mutahaba akiteta jambo kabla ya kutoa salaam za rambirambi kwa familia ya Profesa Baregu
Kwa namna ya pekee Prof Mtahaba ameonyesha kugushwa na Msiba huu wa rafiki yake wa karibu,Mtu wake na Swahiba yake Prof Baregu

Nasi tunaungana na Watanzania wote kutoa pole kwa familia na na Wanakagerawote. Mema yako kwa nchi yatakumbukwa daima ,kwaheri BABA kwaheri Prof.Baregu
Mzee Masasi akitolea jambo ufafanuzi
Bukobawadau tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu na kurasa zetu mbalimbali za Instagram na facebook pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote pale wasiliana nasi kupitia namba 0754 505043/ 0784 505045
Freeman Aikaeli Mbowe na John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),wakifatilia kinachojiri kulingana na ratiba,mazishi ya Prof.Baregu

Mchungaji Rwankomezi akiongoza Ibada ya Mazishi ya Prof.Baregu
Muendelezo wa matukio ya picha,Mazishi ya Prof Baregu.
Msemaji wa Familia Prof Kaijage akitoa neno.
Kaka wa Mjane wa Marehemu Prof Baregu akitoa neno

Wasifu wa Prof. Mwesiga Laurent Baregu ukisomwa na Kijana wake  Mwombeki Mwesiga Baregu
KUZALIWA
Prof Baregu alizaliwa tarehe 23 February 1944 katika Kijiji cha Maruku akiwa mtoto wa nne wa Laurent na Paulina Baregu.
Laurent na Paulina Baregu walikuwa wazazi waloilea watoto wao kwenye msingi wa kufanya kazi kwa bidii na kuwaheshimu watu. Kwa maneno mengine, walikuwa wazazi wakali ambao hawakupenda kuvumilia upuuzi. Familia ya Baregu ilikuwa na inajishughulisha na kilimo na miradi mbali mbali ikiwemo kilimo, duka, na mgahawa. Prof. Baregu alikuwa mtoto aliyependa kusoma vitabu.
ELIMU YA AWALI
Prof Baregu alipata elimu ya msingi katika shule ya Nyakatare Primary School mwaka 1954 na Kagondo Middle School mwaka 1958, na elimu ya sekondari katika shule ya Nyakato Government Secondary School mwaka 1962.
ELIMU YA MAKTABA
Mwaka 1964 Prof Baregu alihitimu cheti cha masomo ya maktaba ama “Certificate in Library Studies” (with Honors) kutoka Makerere University College na akaendelea na masomo hayo hapo Ealing Library School London 1965 – 1968.
ELIMU YA SIASA, UCHUMI, NA MAHUSIANO YA KIMATAIFA
Mwaka 1974 - 1976 Prof. Baregu alisomea na kuhitimu degree ya Bachelors of Arts kwenye uchumi na sayansi ya siasa kutoka chuo cha Brock University, Canada.
Mwaka 1977 – 1978 Prof. Baregu alisomea na kuhitimu degree ya Masters of Arts kwenye mahusiano ya kimataifa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Mwaka 1980 alianza kusomea degree ya PhD kwenye chuo cha Stanford University nchini Marekani ambapo mwaka 1983 aliandika kuhusu mahusiano ya kimataifa na mwaka 1985 alitunukiwa degree ya PhD kwenye masuala ambayo yalichanganya uchumi, siasa, na mahusiano ya kimataifa yaani “International Political Economy”.
Mwaka 1988 alipata shahada ya Post-Doctoral Diploma in Advanced

AJIRA
AJIRA YA MAKTABA
Baada ya kumaliza masomo ya maktaba mwaka 1968 aliajiriwa mwaka huo huo na Tanzania Library Services kama Rural Services Librarian mpaka 1971.
Mwaka 1971 aliajiriwa kama mtaalam wa masuala ya huduma za library vijijini, yaani Rural Libraries Expert na shirika la UNESCO katika mradi wa UNDP/UNESCO Literacy Project, Mwanza.
Prof. Baregu alijikita san ana mradi huu na alikuwa na mchango mkubwa katika kueneza huduma za maktaba kwenye vijiji mbali mbali Tanzania na kusaidia kusukuma elimu kwa watu wazima, kuongeza uwezo wa kusoma na kuandika, na kupunguza ujinga Tanzania. Mradi huu ulikuwa chocheo mojawapo ambayo iliwezesha Tanzania kutambulika dunia nzima kwa kupunguza ujinga kwa watu wazima yaani kwa kukuza adult literacy.
Prof. Baregu, akiwa ni mtu ambaye alikuwa anapenda kusoma tangu utoto wake, alijivunia sana mafanikio ya mradi huu uliopeleka vitabu vijijini.
AJIRA YA CHUO KIKUU
Mwaka 1978 akiajiriwa kama Lecturer kwy idara ya Sayansi ya Siasa (Political Science) katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Prof. Baregu alianza safari yake ndefu ya ajira kama mtafiti na mwalimu katika fani hiyo. Kuanzia mwaka 2003 hadi 2010 alitumikia chuo hicho kama Full Professor of Political Science kwenye International Relations.
AJIRA YA SAUT
Mwaka 2010 alijiunga na Chuo cha St Augustine University Tanzania (SAUT) kama Full Professor of Political Science, katika kituo cha Dar es Salaam.
UJUMBE KWENYE TAASISI MBALI MBALI NA TUME YA TAIFA YA KATIBA
Katika uhai wake Prof. Baregu ametumikia taasisi, asasi, na bodi mbali mbali zikiwemo Mo Ibrahim Index of African Governance, University of Dar es Salaam Academic Staff Assembly (UDASA), Pan African Movement (PAM), na zinginezo.
Lakini ujumbe wake kama Commissioner, kwenye Tume ya Taifa ya Katiba, ilikuwa mahususi kwake kama mbobezi wa sayansi ya siasa. Pamoja na mafanikio mengi ambayo tayari alishayapata kwenye taaluma ndani na je ya taaluma, alihamasika san ana kazi hii. Aliwahi kusema kwamba kazi ile ilimruhusu kutumia utaalam wake tofauti na ajira na ujumbe wake mwingine huko nyuma. Alifarijika sana na jitihada za tume hiyo. Binafsi aliwahi kunionyesha vitabu vya kazi na yatokanayo na kazi ya Tume kwa kuonyesha namna utaratibu wao ulikuwa wa kisayansi na uliweza kubaini masuala mbali mbali ya kijami



SIASA Prof Baregu alianza shughuli za kisiasa akiwa kijana mdogo. Alikuwa akimsindikiza baba yake kwenye vikao vya maendeleo ya kata (ward development council meetings) tangu hata kabla ya uhuru. Akiwa miongoni mwa kizazi ambacho kilikuwa ndiyo vijana wakati wa uhuru alikuwa mtu mwenye matumanini mengi ya jamii huru ya kiafrika na jamii ya dunia vile vile. Pale ambapo mfumo wa vyama vingi vilipoingia Tanzania ikawa ni vugu vugu lenye mvuto mkubwa kwake. Mwaka 1995 alikuwa mshauri kwenye chama cha NCCR Mageuzi na halafu akawa Wwenyekiti wa kampeni wa chama hicho kwa uchaguzi wa wabunge na uraisi. Mwaka 2004 akawa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Maendeleo na Demokrasia (CHADEMA). FAMILIA Prof Baregu alikuwa na familia kubwa kiasi. Kwa mke wake wa kwanza, walipata watoto watatu, kwa mke wa pili, alipata mtoto mmoja, na kwa mke wa tatu walipata watoto watatu. Prof. alikuwa mwalimu kazini na nyumbani. Mara nyingi alikuwa aki-share maoni na masomo yake na wanafamilia. Watoto walisikia kuhusu harakati mbali mbali za ukombozi Afrika na mengineyo. Tuliziita “lectures”. Alihimiza Watoto wafanye kazi kwa bidi ama ni za mkono ama za kufikiri. Watoto wake walifanya vizuri sana katika masomo. Tulikuwa na chumba cha library pale nyumbani Chuo Kikuu. Siku moja nikiwa kijana mdogo wa takriban miaka 15 alipeleka katika chumba hicho akawa ananionyesha vitabu vingi vilivyopo pale akaniambai “urithi wako utakuwa ujuzi sio hela” akasema kama hautakuwa unasoma na kukusanya ujuzi kama yeye alivyofanya yeye basi usishangae haujaambulia urithi mwingine. Mimi nilimuelewa na wote tulimuelewa. Prof. alipenda sana watoto na wajukuu wake. Watoto wengine walivyokuwa na wahama nyumbani na kuwa na makazi yao na ule ukali wake ukawa unapungua na Zaidi kuwa rafiki mzuri wa watoto wake. Wajukuu wake wengine wakampa jina “Babu Professor” na walipenda kumsomea vitabu vyao. UGONJWA Prof. Baregu alipata kiharusi ambayo ilichangiwa na presha ya damu kuwa juu, mnamo February 2019. Alijitahidi na kupata unafuu mpaka akawa anatembea mwenyewe lakini baada ya mwezi akapata stroke nyingine ambayo ilimdhoofisha zaidi. Alikuwa akipata matibabu hospitali ya Muhimbili na alienda India kwa matibabu zaidi. Kuanzia mwezi wa tatu mwaka huu hali ya Prof ilipata changamoto ya magonjwa miguu kumsumbua, kifua na presha. Tarehe 29 Mei akalazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupata huduma ya matibabu. Hata katika hali yake ya ugonjwa kwenye siku za mwisho, Prof. Baregu aliweza kutupa sisi faraja. Siku moja, tukiwa hospitali, baada na kikao na daktari kuhusu tiba iliyokuwa inaendelea tulienda

UGONJWA
Prof. Baregu alipata kiharusi ambayo ilichangiwa na presha ya damu kuwa juu, mnamo February 2019. Alijitahidi na kupata unafuu mpaka akawa anatembea mwenyewe lakini baada ya mwezi akapata stroke nyingine ambayo ilimdhoofisha zaidi. Alikuwa akipata matibabu hospitali ya Muhimbili na alienda India kwa matibabu zaidi.
Kuanzia mwezi wa tatu mwaka huu hali ya Prof ilipata changamoto ya magonjwa miguu kumsumbua, kifua na presha. Tarehe 29 Mei akalazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kupata huduma ya matibabu.
Hata katika hali yake ya ugonjwa kwenye siku za mwisho, Prof. Baregu aliweza kutupa sisi faraja. Siku moja, tukiwa hospitali, baada na kikao na daktari kuhusu tiba iliyokuwa inaendelea tulienda
Mama Adventina Matungwa katika kuwajibika
Chief Kalumuna akitoa heshima zake za mwisho kuaga mwili wa Prof.Baregu
John Mnyika, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),akitoa heshima zake za mwisho.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa , Freeman Mbowe akitoa heshima za mwisho kuaga mwili wa Prof.Baregu

Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiewa unaendelea
Heshima za mwisho.
Ni huzuni,Simanzi vilio na machozi kwa wanafamilia
Pichani katikati anaonekana Mzee Ramadhani King akiwa ameungana na waombolezaji wengine kushiriki maziko ya mpendwa Prof Baregu  yaliyofanyika Kijijini Maruku Bukoba.
Sehemu ya Watawa wa Kikatoliki waliohudhuria mazishi ya Prof.Baregu.
Endelea kuwa nasi kwa mtiririko mzima wa matukio
Muendelezo wa matukio ya picha

Pumziko la milele tunakutaki....
Mama Mjane wa Marehemu Prof Baregu akitoa heshima zake za mwisho
Umetangulia Baba,Mzazi,Mlezi na mshauri .#Tutaonanabadae
Mwisho Bukobawadau tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo katika mtandao wetu na kurasa zetu mbalimbali za Instagram na facebook pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote pale wasiliana nasi kupitia namba 0754 505043/ 0784 505045
Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiendelea....
Utaratibu wa kutoa heshima za mwisho ukiendelea....
Last Lespect....
Paroko akitoa heshima za mwisho
Muonekano wa Jeneza lenye mwili wa Mpendwa wetu Prof Baregu
Hii ndiyo Safari ya Mpendwa ya Prof Baregu
Nenda Baba nenda! Umevipiga vita vilivyo vizuri Mwendo umeumaliza Mzazi wetu,mlezi wa wengi Prof.Baregu
Wanafamilia wakiweka Udongo kwenye kaburi.
Mwombeki Mwesiga Baregu akiweka udongo kwenye kaburi la Baba yake mpendwa Prof Mwesiga Baregu
Mchungaji akisimika msalaba kwenye kaburi la Prof Baregu
Ndugu wa marehemu Prof Baregu wakiweka Shada la maua
Prof Kaijage na
Freeman Aikaeli Mbowe wakiweka mashada ya maua
Mama Mtahaba akiweka shada la maua
Utaratibu wa kuweka mashada ya maua ukiendelea kwa kuzingatia makundi mbalimbali
Hii ndiyo nyumba ya milele aliyolazwa Prof.Baregu
Mwisho maombi ya pamoja
Muendelezo wa matukio ya picha kwa ajili ya kumbukumbu na Bukobawadau
Mwisho Bukobawadau tunapenda kukufahamisha kuwa tunao uwezo wa kukupa nafasi ya matangazo
katika mtandao wetu na kurasa zetu mbalimbali za Instagram na facebook pia kwa taarifa au shughuli yotote ili kufikia idadi ya watu unaotaka kokote pale wasiliana nasi kupitia namba 0754 505043/ 0784 505045
 

 







Next Post Previous Post
Bukobawadau