Bukobawadau

Kuumwa kwa wachezaji 16 wa Simba kwapelekea mechi yao na Kagera Sugar kuahirishwa

Kuumwa kwa wachezaji 16 wa Simba kwapelekea mechi yao na Kagera Sugar kuahirishwa

Mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara baina ya Kagera Sugar dhidi ya Simba SC uliyopangwa kupigwa  kwenye dimba la Kaitaba mjini bukoba umehairishwa.

Mchezo huu ulio kuwa umepangwa kuchezwa hapo jana tarehe 18 mwezi december 2021, kwenye uwanja wa Kaitaba mjini bukoba umeahirishwa. Taarifa rasmi iliyo tolewa na bodi ya ligi (TPLB) imedai kuwa ni kwa sababu za kuumwa kwa wachezaji wa simba.

"Sababu za kuahirisha mchezo huo ni taarifa ya kitabibu kuwa wachezaji 16 wa simba kati ya 22 waliosafiri kwenda bukoba, wameonekana kuwa na dalili za mafua na kukohoa hali inayochangiwa na mabadiliko ya hali ya hewa (Seasonal influenza) kama ilivyo tokea katika miaka ya nyuma." imeeleza taarifa hiyo.

Unaweza kuisoma taarifa yote kamili hapa chini.

Kuumwa kwa wachezaji 16 wa Simba kwapelekea mechi yao na Kagera Sugar kuahirishwa

Next Post Previous Post
Bukobawadau