Bukobawadau

JENGO LA MAMA NA MTOTO KUKABIDHIWA MWEZI MACHI MWAKA HUU

Muonekano wa nje ya jengo jipya la Mama na Mtoto katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa - Sekou Toure linalojengwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) ambao ujenzi wake umefikia asilimia 94. Jengo hilo linagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 10.1 na kutarajiwa kuanza kutumia mwezi Machi, 2022.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya, akizungumza na Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza, Dkt. Thomas Rutachuzibwa, wakati akitoka kukagua ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika hospital ya Rufaa ya Mkoa - Sekou Toure linalotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mkoani Mwanza.

Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya, akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mkoa wa Mwanza Eng. Moses Urio, alipokuwa akikagua ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa  - Sekou Toure linalotekelezwa na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), Mkoani Mwanza.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Majengo Tanzania (TBA), mkoa wa Mwanza Eng. Moses Urio, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Eng. Godfrey Kasekenya, wakati alipokagua maendeleo yaliyofikiwa ya ujenzi wa jengo la Mama na Mtoto katika Hospital ya Rufaa ya Mkoa  - Sekou Toure linalotekelezwa na Wakala huo, mkoani humo.


PICHA NA WUU

Next Post Previous Post
Bukobawadau