Bukobawadau

MAKAMU WA RAIS MH .DKT MPANGO AZINDUA KAMPENI YA UPANDAJI MITI Palm trees) BUKOBA MJINI

Makamu wa Rais Mheshimiwa, Mhe. Dkt. Philip Mpango akipanda Mti aina ya Palm tree katika uwanja wa Uhuru Mjini Bukoba Mkoani Kagera wakati wa mkutano wake wa hadhara na wananchi ikiwa ni Uzinduzi wa Kampeni inayoendelea Mjini Bukoba kwa lengo  kutunza Mazingira na kupendezesha  Mji huo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango  akipanda Palm Tree ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Kampein ya Upandaji Miti hiyo kwenye Manispaa ya Bukoba yenye lengo la kutunza Mazingira na kupendezesha  Mji wa Bukoba.
Viongozi wa Dini wakishiriki kupanda Miti ya Palm, kushoto ni Askofu Abednego Keshomshahara wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini Magharibi akiwa na Sheikh Yusuph Kakwekwe Sheikh wa Manispaa ya  Bukoba, wakiwakilisha Viongozi wengine wa Dini.
Baadhi ya WanaKamati ya Mradi wa Upandaji wa  Palm Tree Bukoba wakishiriki kupanda Mti huo, pichani katikati ni Naibu Waziri wa Nishati Wakili Stephen Byabato (Mb) ambaye pia ni mjumbe wa kamati. hiyo  Picha zote na Dulla Uwezo
Mkuu wa Mkoa Kagera Meja Jenerali Charles Mbuge akishiriki kupanda Mti wake wa Palm katika uzinduzi wa Kampeini ya Upandaji wa Palm Tree Mjini Bukoba.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Kagera Mama Costancia Buhiye akishiriki zoezi la upandaji Palm, akisaidiwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Palm Tree Planting Bwana Seif  Mkude Mwenyekiti wa Kamati ya Upandaji Palm tree Mjini Bukoba
Kampeni ya Upandaji Palm Tree Bukoba ,Lengo ni Mkoa Kuongoza kwa usafi na muonekano dunia kama Kigali na Nchi ya Tunisia) Usafi ni jambo muhimu, linalotazamwa kuanzia kwa mtu binafsi, nyumbani, ofisini, jamii ama taifa. Na watu wanaoishi kwenye eneo safi kwa mujibu wa wataalamu wanatajwa kuwa na maisha marefu zaidi kuliko wale wanaoishi kwenye mazingira machafu.
Maji safi, hewa safi, utunzaji mzuri wa taka na usafi wa mazingira ni mambo muhimu yanayoweza kuathiri afya ya mwanadamu.
#BukobawadauUpdates #BukobaYaPalmTree
#BukobaMpya #Bukobawadau 

 

Next Post Previous Post
Bukobawadau