Bukobawadau

RC CHARAMILA AKUTANA NA WATUMISHI WA TANESCO KAGERA

Bukoba:Mkuu wa Mkoa wa Kagera Albert Charamila  akizungumza na watumishi wa shirika la Umeme Tanesco Mkoa wa Kagera katika kikao cha kujitambulisha kwa watumishi hao, Mkuu wa mkoa wa Kagera Albert Charamila amesema kuwa, shirika hilo likifanya vizuri katika kuwahudumia wananchi na itakuwa ni jambo la kushangaza, akitokea mtumishi wa shirika hilo kubainika kapokea rushwa au kashindwa kusimamia vizuri mali za shirika hilo.

Mh Chalamila pia amewataka wafanyakazi washirika hilo, wahakikishe wanaondoa malalamiko yote ya wananchi ambayo yapo ndani ya uwezo wa shirika, ili wananchi waendelee kuwa na imani na shirika hilo, kwani fedha nyingi zimetolewa ili kufanikisha na kuboresha miradi ya umeme.

Kaimu Meneja wa Tanesco Mkoa wa Kagera Bw. Pembe Jeverino pichani akizungumza katika kikao hicho 

Kwa upande wake, Kaimu Meneja wa shirika hilo mkoa wa Kagera Bw. Pembe Jeverino, amemuhakikishia mkuu wa Mkoa kuwa maelekezo yote aliyoyatoa yatafanyiwa kazi kwa weledi, na ufasaha na miradi mbali mbali mikubwa na midogo inaendelea kufanyiwa kazi, ndani ya mkoa wa Kagera kwa kusimamiwa na wataalamu wa shirika hilo. 

Mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Kagera akizungumza katika kikao hicho amesema, jeshi hilo litaendelea kushirikiana na shirika hilo katika kuwabaini wote watakao hujumu mali za shirika, na kuwafikisha katika vyombo vya kisheria. 

Muendelezo wa matukio ya picha.
Picha mbalimbali kwa ajili ya kumbukumbu
Watumishi wa Tanesco Mkoa Kagera katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe.Albert Chalamila ,Kamanda TAKUKURU Kagera  Joseph John, Kaimu RPC SSP Amos Mimata pamoja na Kaimu RAS Projectus Rutabanzibwa
Watumishi wa Tanesco Mkoa Kagera katika picha ya pamoja na Mkuu wa mkoa wa Kagera Mhe.Albert Chalamila ,Kamanda TAKUKURU Kagera  Joseph John, Kaimu RPC SSP Amos Mimata pamoja na Kaimu RAS Projectus Rutabanzibwa
Muendelezo wa matukio ya picha.
 

 

Next Post Previous Post
Bukobawadau